Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 581
Mwanahabari Absalom Kibanda
TAARIFA ZA AWALI
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na Dimba, Absalom Kibanda amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake wakati akiingia nyumbani kwake Mbezi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kibanda alivamiwa majira ya saa sita usiku wa kumkia leo Tar March 6 2013, akitokea kwenye majukumu yake ya kila siku. Inadaiwa kuwa alichomolewa kwene gari, akapigwa na vitu vyenye ncha kali kichwani, ametobolewa jicho lake la kushoto pamoja na kunyofolewa kucha na baadhi ya vidole na hatimaye kutupwa mbali kidogo kutoka nyumbani kwake.
Baada ya hapo wasamalia wema walijitokeza na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambako alipokelewa vizuri na madaktari na kumpatia tiba ya awali na baadaye kumhamishia Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) ambako mpaka sasa anaendelea na matibabu.
Watu waliomfanyia madhara hayo, hawakuweza kuchukua kitu chochote kwenye gari ambapo kulikuwemo Laptop, simu na nyaraka zingine.
Absalom Kibanda akiwa hospitali.
APELEKWA AFRIKA KUSINI
Tasnia ya habari nchini Tanzania kwa mara nyingine imetingishwa baada ya mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini humo, Absalom Kibanda kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jumatano nje kidogo ya jiji la dara es salaam.
Kibanda tayari amesafirishwa jioni hii kwa ndege maalum kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ambapo kwa mujibu wa taarifa za awali za kitabibu, amejeruhiwa kichwani ambako alipigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni nondo. Jicho lake la upande wa kushoto limeathirika kwa kudhaniwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali, kucha katika kidole cha mkono wa kulia kung’olewa na meno mawili kung’olewa pia huku washambuliaji wakiwa hawajaondoka na kitu chochote.
Tukio la kujeruhiwa mweyekiti Kibanda limekumbusha tukio zito lililowahi kutoke akatika tasnia ya habati nchini Tanzania mwishoni mwa mwaka jana baada ya mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha channel ten kuuwawa katika mkutano wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema mkioani Iringa.
Neville Meena ni katibu mkuu wa jukwaa la wahariri amekemea kuhusu tukio hilo akisema kuwa linatishia waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa uhuru.
Katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako Kibanda alikuwepo kabla ya kusafirishwa kwa matibabu, nje ya nchi viongozi mbalimbali wa serikali vyombo vya habari na wanasiasa walifika kumjulia hali akiwemo bwana Reginald Mengi ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa vyombo vya habari Tanznania, MOAT.
Bwana Kibanda ambaye kwa sasa ni mhariri mtendaji mkuu wa kampuni ya New Habari inayomiliki magazeti kadhaa hapa nchini miezi michache iliyopita alikuwa mhariri mtendaji katika gazeti la Tanzania daima linalomilikiwa na familia ya mwenyekiti wa chama cha demokrasai na maendeleo CHADEMA, bwana Freeman Mbowe.
Mkurugenzi wa idara ya habari, maelezo hapa nchini Bwana Assah Mwambene alikuwepo pia hospitalini muhimbili.
Kamanda wa kanda maalum Suleimano Kova katika mkutano wake na waandishi wa habari amesema kwa kushirikiana makao makuu ya polisi wameunda jopo la wapelelezi kumi kwa ajili ya kuchunguza kuvamiwa na kushambuliwa na hatimaye kujeruhiwa kwa mwenyekiti huyo wa jukwaa la wahariri Absalom Kibanda ambapo amekiri kwamba vitendo vya mashambulizi yanayoonekana ya kulipiza kisasi vimeshamiri kwa sasa.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dakta Gharib Bilal naye alikuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu aliyefika kumjulia hali bwan Kibada akiwa muhimbili kabla ya kusafirishwa nchini Afrika Kusini.
PIA, SOMA:
- Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana
- Si ufisadi, ni urais 2015 (2) na Absalom Kibanda
- Asa Mwambene: Absalom Kibanda hana vigezo vya kuwa mhariri
- Absalom Kibanda akamatwa!
- Absalom Kibanda: Mgombea Urais mmoja hakutaka nifike huu mwaka wa Uchaguzi
- Kikwete, Serikali ichunguzwe suala la Absalom Kibanda
- Waraka wa Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Ndg Absalom Kibanda kwa Rais Jakaya Kikwete
- Kikwete visits TEF chairman Mr Absalom Kibanda in South Africa
- Absalom Kibanda ni Nani?
- Absalom Kibanda: Sasa sitaogopa kitu na sina cha kupoteza, nitafichua kila kitu
- Mtanzania kwafukuta, Absalom Kibanda kupewa likizo ya lazima kupisha uchaguzi Mkuu
- Mateso ya Absalom Kibanda yasitutishe, yatutie nguvu za kupambana kwa umakini zaidi
- Absalom Kibanda Aliteswa wakati ana Kesi ya Uchochezi (Inayohusu Polisi)
- Mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Azory Gwanda apotea siku 10 na hajulikani alipo
- Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano
- Mhariri Mtendaji wa Gazeti la MwanaHALISI, Saed Kubenea avamiwa na kumwagiwa tindikali akiwa ofisini kwake
- Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA
- Mchora katuni Opptertus John Fwema ashikiliwa na Polisi kwa Makosa ya Mtandao
- Mwandishi wa Mwananchi Jesse Mikofu ashambuliwa na askari akitekeleza majukumu yake
- Mwandishi wa Watetezi TV mbaroni kwa madai ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni juu ya watuhumiwa kulazimishwa kulawitiana Kituo cha Polisi
- Mwandishi wa Habari, Kazimbaya Makwega ashikiliwa na Polisi, asafirishwa kutoka Mwanza hadi Dodoma
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana
~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana