Dada yangu Tina,
Samahani sana, napata mashaka na usahihi wa hii taarifa yako uliyoileta humu chini ya "habari mpasuko!".
Kwanza hukuweka source, ila kwa vile ni lady, kutoweka source kunahalalisha uwezekano wa connection fulani, kama member tuu mwenzake wa jf, mshirika wake newsroom, rafiki wa kike, mke, etc, that is understandable!, na tumevumilia kwa ahadi ya kupatiwa update!. Lakini tangu ilipopost ile first post, tunaelekea masaa 6 baadaye na hakuna update yoyote!.
Mara baada ya kuisoma humu, nilitembelea zile kumbi ambazo Kibanda huwa anashinda, sikukuta kitu, hii inamaana wewe Tina ndio the first to know hata barazani kwake wasijua, ilhali unadai ametekewa nyumbani kwake?!. Kutekwa ni kuhamisha toka sehemu moja hadi nyingine, kuna kuvamiwa nyumbani na kutekwa, lakini huku kuvamiwa nyumbani, kutekwa, kujeruhiwa na kupelekwa Muhimbili kunatia mashaka sana!.
Mode!.
Nashauri tuweke vigezo maalum vya "habari mpasuko", ili kupata uhakika wa habari mpasuko yoyote ambayo ni shoking, 1. lazima mleta habari atoe source, na kama ni yeye na ameshuhudia then
2. Aweke contact ili modes mumpigie simu ku verify hiyo habari, vinginevyo mtu yoyote anaweza kuleta uzushi wowote na kusail through hivyo kuligeuza jukwaa letu hili adhimu kuonekana kama kijiwe fulani, au genge la wazushi na wote kuonekana hatuna maana!.