Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

"...kwa mujibu wa taarifa toka kwa Kamanda K, waliohusika na tukio hili ni majambazi aina ya NINJA toka nchi jirani ya Malawi!!!" Tusishangae kusikia hili kwa maana wameishiwa ya kusema...

My poor country - a Mafioso state...

POLE Kibanda, ni gharama ya mapambano hii...
 
Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.

kumbe alitokea huko, ohooooo, visasi hivyo.
 
Mwita Maranya unatuangusha mkuu, Usalama wa taifa alizikwa nao Mwl. Nyerere, na hivyo kutafuta jina sahihi la TISS ambalo ni UHASAMA WA TAIFA.

Mambo ya visasi ni magumu sana mkuu, huyu KIBANDA alitimuliwa kule Tanzania daima, sasa kama kuna misuguano imeendelea kuwepo baina yake na huyo mwajiri wake wa zamani lazima mambo kama haya yatarajiwe.
 
Mkuu unatarajia nini endapo walio mteka ndo hao hao wanao takiwa kufanya uchunguzi ? Kweli nime amini hiki kizazi cha tume ni problem.
Mkuu kama ndiyo hao hao waliomteka ndiyo wafanya uchunguzi, basi hakuna uchunguzi kwa vile wanakijua kilichofanyika.

Kwa nini nchi itake uchunguzi wakati inafahamu fika chanzo na malengo ya kutekwa na ikizingatiwa ni nchi inayoongozwa na sheria (bunge, serikali na mahakama).
 
Ametekwa na kujeruhiwa nyumbani kwake??? How come utekwe hapo hapo na ujeruhiwe hapo hapo na ukimbizwe hospitali?
Je ni nani aliye mteka, na ni naliyemkimbiza hospitali na ni nani aliye muokoa?


......

Acha maswali magumu bwana Watz hatujazoea hayo maswali hauni ndo maana round abouts ni nyingi?
 
mmh..so funny! Ulimbokalism has emerged as a threatening big monster in tanzania!

......

sisi tunahesabu tu wanyakyusa wanvyo malizwa, kumbuka jaji mwakibete,prof Mwaikusa,Prof.Mwandosya,Mwakyembe,Ulimboka,Mwangosi,Mwakiteleko sasa abuu kibanda,tafakari!
 
usipindishe mjadala, huyu aliondoka tz daima kama mhariri mkuu na kwenda new habari coop. Wachapaji wa magazeti ya mtanzania na rai, waliomdhuru ni huko alikotoka. Uchunguzi ufanywe na yeye aeleze watu ambao alikuwa na kisa nao

......


Fikra fupi kama hizi ndizo zinazo sababisha serikali kufanya unyama itakavyo, tujikumbushe swaga la aliyekua Mbunge wa Tarime:-

Huyu bwana alikua na mgogoro na viongozi wenziye pale CHADEMA, wakati amesimamishwa uongozi kabla hata mwezi haujapita, Chacha Wangwe akakumbwa na umauti (kwa ajali ya gari) watu wengi walipiga sana kelele kwamba uchunguzi makini ufanyike lakini wapi, hakuna kilichofanyika, nadhani mzee mwanakijiji aliandika makala ndefu sana akionesha mashaka yake na kifo kile, lakini bado hakuna aliyetaka ufanyike uchunguzi.

Kumbuka mwenye amri ya kuleta wachunguzi independent ni serikali, hadi leo kimya, watu wenye akili finyu wakasema atakua Mbowe na CDM, sababu ikiwa ya kitoto sana, eti dereva alikua ni Mchaga kama mwenyekiti wa CDM, kesi ilifanyika, yule aliyekua dereva wake akawekwa ndani kwa miaka 3.

Kabla hajamaliza adhabu ile, rais aliyekua madarakani akamfungulia, utafiti binafsi ukaenda mbali zaidi ikaja julikana kwamba dogo yule amewahi kwenda Libya kwa mafunzo maalumu chini ya UVCCM.

Kwenye msiba, Mbowe alitahadhalishwa eti asiende kwani Wakulya wangemuua, wapi bwna, Mbowe alikwenda na akapokelewa na jamii ya watu wa pale kama kiongozi wa marehemu Mbunge wao, uchaguzi ulipo rudiwa wana Tarime walimchagua tena Mbunge toka CDM, hapo ndio ukawa mwanzo wa kitu inayoitwa leo, Opearation Sangara.

Napenda tu nikwambie mkuu serikali hii inaweza kufanya kitu ili tu asingiziwe mwingine, kwani issue ya Daud Mwangosi ilikuaje? si walisema CDM, picha sasa za mnato na za video ndio zikawaumbua, usiwe na akili fupi, ngoja uchunguzi makini ufanyike, you will see.
 
Acha kujiaibisha kwa kuongea mambo ya ajabu ajabu. Yaani unaona udhaifu wa usalama wa taifa baada ya Kibanda kupigwa na vibaka. Mbona huwa huongei hayo dada zetu wanapoibiwa pochi kila siku pale ''mtego wa panya?''

.....

Hilo haliondoi ubovu wa usalama wa taifa! ni wabovu tangu asubuhi mpaka jioni.
 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Abdalom Kibanda, amekimbizwa Muhimbili baada ya kuvamiwa na kisha kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi.

Watu hao walimvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake.

Aliokotwa na majirani na kukimbizwa hospitalini Muhimbili kwa matibabu ya haraka.

Pamoja na kuumizwa hivyo, hakuna kitu hata kimoja kilichoporwa katika gari lake

attachment.php


Taarifa zaidi baadae...
hapo kuna tume itapata ulaji,maana nchi hii tume ni zaidi kwa kazi kuliko wale walioajiriwa kwa kazi yenyewe
 
Mbona mnapenda kuandika utani?fikria angekuwa ni ndugu yako ungeandika ujinga2?wa tz tuwe na huruma,
 
Wee mleta habari, hebu weka mambo sawa. Ametekwa au amevamiwa na majambazi nyumbani kwake? Tuambie wamechukua nini? Ukisema ametekwa ina maana walimpeleka kusikojulikana na kuanza kumshambulia? Hebu toa maelezo yanayojitosheleza bwana.

Ina maana wewe ni mtoto mdogo kutekwa sio lazima upelekwe sehemu isijulika hata chumbani kwako unaweza ukatekwa na ukafanyiwa mbaya hivyo kutekwa ni sehemu yoyote ile acha kejeli kama umeona mada imekukwaza si uachane nayo kwani lazima uchangie?
 
Mimi kawaida yangu humu mtu akifanya anajuwa sana kiingereza huwa namkabidhi kwa Kiranga tu.

Mwambie aje huyo Kiranga wako halafu njoo na wewe na wanao wanaosoma St. Mary's na yule demu wako anayefagia ofisi za British Council.
 
Mambo ya visasi ni magumu sana mkuu, huyu KIBANDA alitimuliwa kule Tanzania daima, sasa kama kuna misuguano imeendelea kuwepo baina yake na huyo mwajiri wake wa zamani lazima mambo kama haya yatarajiwe.
Hivi Uzushi unakusaidia nini wewe Kibwengo? Kibanda ameacha kazi mwenyewe Freemedia na kufuata maslahi zaidi Habari Corporation, hata kama huna akili lakini tumia hizo chache zilizosalia kichwani kwako zinazokusaidia kukumbuka kwamba kuna kuvaa chupi na kuchamba baada ya kuhara.
 
Last edited by a moderator:
Mwambie aje huyo Kiranga wako halafu njoo na wewe na wanao wanaosoma St. Mary's na yule demu wako anayefagia ofisi za British Council.
Yaani kukutajia tu Kiranga ghafla umeshajuwa na kuandika kwa Kiswahili!!?? kweli Kiranga ni tishio humu na ndio Dikishenari ya JF.
 


Its everyone's wish, kinana will help him as he has been promoting him
.

Kinana is in Kenya right now, but if he was here and decide to task his boys. Chances za kupatikana wahusika ningesema ni more than 80%.
 
sisi tunahesabu tu wanyakyusa wanvyo malizwa, kumbuka jaji mwakibete,prof mwaikusa,prof mwandosya,mwakyembe,ulimboka,mwangosi,mwakiteleko sasa abuu kibanda,tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

...mbeya kunani,aliyeuwawa na askari kule makete pia ni wa mbeya.......
Yes ni lango!
 
Nilisikia habari hiii, moja kwa moja nilihisi watu kama nyie mtakuja na mawazo kama haya. Ukitazama kwa undani inawezekana kwa asilimia nyingi waliompokea kutoka Tanzania Daima ndio waliomdhuru ili waje na mawazo kama yako. ila kwa mtu ambaye ana akili timamu haiwezi kumuingia akilini. Nadhani hamkujipanga. Rudini mjipange upya.

Mambo ya visasi ni magumu sana mkuu, huyu KIBANDA alitimuliwa kule Tanzania daima, sasa kama kuna misuguano imeendelea kuwepo baina yake na huyo mwajiri wake wa zamani lazima mambo kama haya yatarajiwe.
 
Back
Top Bottom