Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Kibanda kakaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!! Si jana tu ulikuwa ukiwapamba majemadali wetu wakati ukiwa ndani ya Tanzania daima?! sasa hata makala zako ndani ya gazeti hilo hazijafutika tayari umekuwa kama chatu na kuvaa ngozi nyingine kana kwamba wewe si yule wa jana? Duh kweli kaka acha pesa iitwe mwana haramu. Kwaheri kaka, tukutane njia panda 2015.
 
Great Thinkers,
Baada ya kuisoma makala hii ya Absalom Kibanda Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, nimejikuta napata mashaka sana na zaidi kupoteza imani na uzalendo wake. Pia nimejikuta nikiamini maneno niliyokuwa nikiyapata kijiweni kwamba Kibanda ni mmoja wa beneficieries wa Ufisadi kutoka tasnia ya Habari nchini


NAMUOGOPA ABDURAHMAN KINANA

Na Absalom Kibanda

Kwa mara nyingine tena, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeandika historia mpya baada ya kufanya mabadiliko mazito katika safu yake ya uongozi wa kitaifa.

Ni mabadiliko mazito si kwa sababu tu yamefanywa na CCM ambayo imekuwa na rekodi ya kubadili sura za watendaji wake kwa namna na kwa njia tofauti, bali kutokana na ukweli kwamba safari hii mabadiliko hayo yamehusisha watu wazito, wenye historia ya kipekee katika medani ya uongozi ndani na nje ya chama hicho.

Ingawa kwa mtazamo wa haraka haraka, mabadiliko hayo yanaweza yakaonekana kuwa ni ya kuyabeza au kuyapuuza kama ilivyotamkwa na baadhi ya wadadisi wa mambo wakiwamo wachambuzi wa masuala ya siasa na hata wanazuoni, ukweli unabaki pale pale kwamba kile kilichofanywa na CCM kinaweka alama ya kipekee katika mwenendo wa siasa za kitaifa za siku zijazo.

Wasifu mzito na historia za kutukuka za baadhi ya wateule wanaounda timu ‘mpya’ ya viongozi watendaji wa CCM kwa kiwango kikubwa ndicho kitu kikubwa pekee kinachosababisha mtu yeyote makini ajikute akipata shida kuyabeza yale yaliyofanywa na chama hicho tawala mwishoni mwa wiki kule Dodoma.

Msuko mpya wa safu ya wakuu wa idara za CCM uliotangazwa na Rais Jakaya Kikwete ukiwajumuisha wanasiasa wasiojua mizaha wawapo kazini kama alivyo Philip Mangula, au makada wa muda mrefu wa chama hicho wa kariba ya Muhammad Seif Khatib na Zakia Meghji una kila sababu ya kutafutiwa dawa mahususi na makamanda wa kambi ya upinzani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipambana kuing’oa CCM madarakani.

Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Kwa muktadha wa makala ya leo na kwa kuzingatia nafasi kuu ya utendaji aliyopewa, nitazungumzia kwa sehemu tu wasifu wa Kinana, mtu ambaye naamini anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na wakati mwingine kudhibitiwa ili kasi yake ya kukijenga chama alichopewa dhamana ya kukinusuru isije ikasababisha kuyumba kama si mauti ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.

Ni wazi kwamba, kuteuliwa kwa Kinana kuwa Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa, akirithi mikoba iliyomshinda, Wilson Mukama, kumetutia ganzi baadhi yetu ambao kwa muda mrefu tumekuwa ‘mashabiki’ au waumini wa kuchagiza kwa njia ya kalamu na wakati mwingine katika mijadala ya wazi kwamba, taifa lilikuwa na haja ya kutafuta mabadiliko ya uongozi kutoka nje ya chama tawala.

Sitaki kuwa miongoni mwa wapenda mabadiliko ambao kwa njia za kujifariji au za kujipa matumaini hewa wameingia katika mkumbo wa jumla jumla wa kumbeza Kinana kwa namna wanayotaka kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba, mtu huyo anaweza akasukumwa kirahisi kwa namna ile ile ilivyopata kuwa kwa watangulizi wake kadhaa waliopata kushika wadhifa huo.

Hupaswi kuwa na akili nyingi kutambua kwamba, umahututi wa CCM kisiasa, kulikokifikisha chama hicho tawala kufikia hatua ya kupoteza dira na kuanza kuliona kaburi la kupoteza madaraka ya dola ndiko kulikorejesha hekima za usikivu kichwani mwa Kikwete hata akalazimika kuwarejesha akina Kinana, Mangula, Seif Khatib na Meghji katika kilinge cha siasa za ushindani mkali ndani na nje ya CCM.

Siyo siri hata kidogo kwamba, hekima hii mpya ya Kikwete ya kumrejesha Kinana ulingoni, ambaye siku chache tu zilizopita alitangaza kustaafu siasa huku akisema alikuwa akikusudia kuwaachia vijana kusukuma gurudumu la uongozi, inahusisha kichwa zaidi ya kimoja kutoka ndani na nje ya CCM.

Kama ilivyo kwa wengi wengine nilianza kulisikia jina la Kinana likihusishwa na ukatibu mkuu wa CCM miaka miwili au mitatu iliyopita hali ambayo ilipata kusababisha nifikie uamuzi hata wa kumuuliza yeye mwenyewe kuhusu taarifa hizo.

Jibu ambalo Kinana mwenyewe alipata kunipa kwamba alikuwa akipenda kuona akiendelea kupata fursa ya kukitumikia chama chake kama mshauri na kwa nyakati mahususi kama zile za kampeni na si kwa nafasi ya ukatibu mkuu lilikuwa likinipa sana faraja.

Kilichokuwa kikinipa faraja si kingine chochote bali fikra zangu (sahihi au potofu) ambazo siku zote zilikuwa zikinifanya niamini kwamba, ukatibu mkuu kwa Kinana ilikuwa ni silaha moja ya maangamizi kwa vyama vya upinzani ambavyo naamini vinapaswa kuendelea kupewa fursa ya kuaminiwa na kukomaa.

Katika mazingira ambayo CCM imeweza kuepuka zahama ya kumeguka vipande viwili kwa kuzingatia maono aliyokuwa nayo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwangu mimi Kinana wa zama hizo alikuwa na anaendelea kubakia kuwa tishio kubwa kwa ustawi wa upinzani ambao ni rutuba muhimu kwa maendeleo ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

Hili ndilo ambalo naamini wapinzani wanapaswa kulitazama na kulitafakari nyakati hizi wanapoendesha harakati zao za kukabiliana na maguvu ya dola na haya mapya ya hoja ambazo aghalab zitaongozwa na Kinana nyakati hizi taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa miaka mitatu ijayo.

Haitoshi kwa kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Dk. Willibrod Slaa na Zitto Kabwe kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko alivyokuwa ‘utopia’ Mukama anayeamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.

Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.

Wachambuzi wa mambo, nikiwamo mimi mwenyewe ambao siku zote tumekuwa tukiiona CCM kuwa chama kinachokufa kwa maana ya kuchungulia kaburi, tunapaswa kuanza kutafakari upya mawazo yetu hayo, nyakati hizi Kinana alipopewa dhamana ya kuwa mtendaji wake mkuu.

Tutakuwa wendawazimu iwapo tutamlinganisha Kinana na Mukama na kusahau kwamba huyu aliye kilingeni leo ndiye aliyemuongoza Benjamin Mkapa katika mapambano makali ya kisiasa mwaka 1995, zama Augustine Mrema alipokuwa tishio la kwanza la kweli dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Alikuwa ni Kinana aliyefanya kazi kubwa katika kipindi chote cha kampeni akiratibu na kuongoza kampeni zote za Mkapa zilizomjumuisha pia Mwalimu Nyerere katika mazingira ambayo wengi walikuwa wakiamini CCM ilikuwa katika mwelekeo wa anguko la kihistoria.

Kinana ambaye kabla ya mwaka 1995 alikuwa tayari amepata kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi alitumia vyema mbinu za medani na zile za kidemokrasia na kiplomasia kumjengea uhalali Mkapa ambaye wakati huo alikuwa mwanasiasa ambaye hakuwa akijulikana sana.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, siku chache tu baada ya kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1995, kwa sababu ama ya ulevi wa madaraka au kwa kutingwa na kazi za kimamlaka, Mkapa alisahau kazi kubwa aliyofanyiwa na Kinana.

Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam nikiwa nimeongozana na mhariri wangu, Muhingo Rweyemamu, ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

Tangu wakati huo hadi wakati wa kampeni za mwisho za mwaka 2010, niliendelea kukutana kwa nyakati fupi fupi na Kinana na mara kadhaa nikawa mtu wa kufuatilia na kuzisikiliza kwa makini, habari zake kutoka ama kwa marafiki au maadui zake wa kisiasa.

Sikushangazwa hata kidogo niliposikia tena kwamba, Mkapa alilazimika kumuangukia tena Kinana na kumuomba aongoze tena kampeni zake mwaka 2000 kabla ya Kikwete naye hajafanya kile alichofanya mtangulizi wake alipomuomba mwanasiasa huyo adhibiti joto la kiti cha urais mwaka 2010.

Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

Lakini pengine kubwa katika yote hayo anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995. Huyu si mtu wa kumpuuza au kumbeza hata kidogo.


My Take:
-Hapo kwenye RED
naona Kibanda kajikita katika kueleza kifo tarajiwa cha upinzani kwa kumezwa na rekodi ya kinana tu bila hata kuzingatia nyakati zilizopo za kisiasa, kupwaya kwa ushindi wa JK kwneye matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na zaidi mchoko wa kimaisha walionao watanzania sasa. Kibanda amejaza mahaba binafsi kwa Kinana pasipo kuzingatia muktadha wa kisiasa uliopo nchini.

Lakini pia Kibanda amejikita katika kusisitiza hatari ya upinzani kufa kutokana na Kinana kuwa GS wa CCM bila kueleza ni kwa vipi anaweza kupambana na hoja zinazotoka kambi ya upinzani hasa CDM au ni Uluteni wake tu Jeshini ndiyo utamfanya aue upinzani.

Aidha, Kibanda anatumia Umeneja Kampeni wa Kinana kwa wagombea wa urais wa CCM bila hata kusumbua kichwa chake,kwamba kuwa meneja haina maana unakuwa incharge wa ushindi wa mgombea bali timu nzima ya kampeni ya Chama ndiyo hufanya kazi hiyo. Mathalan, utamsifu vipi Kinana kwa ushindi wa Mkapa mwaka 1995 wakati Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kivuri chake kilikuwa bado kinaishi ndani ya mioyo ya watanzania? Ni kweli hili si la kubeza lakini si la kumpa credit kubwa kiasi anachotoa Kibanda

-Kwenye Blue,
Kibanda kawa kipofu kiasi kwamba kwakwe yeye tuhuma za ufisadi zinazomkabili Kinana na baadhi ya wana safu wa Sekretarieti mpya ya CCM anaziona nyepesi na zisizo na mashiko. Kwake yeye (Ufisadi ni mwepesi na si hoja kwa sasa) bali hoja ni Kinana na rekodi yake tu tena ya huko nyuma.

Tujadili kwa pamoja hii makala.

yani watu wengine hakuna kitu ..mnapenda kusifiwa tu cdm..mtu akitoa maoni tofauti au akikisifia ccm au serikali huyo kahongwa anahongwa... sasa siasa za wapi hizo ndugu zangu cdm..... mi nawaapia kama uongozi na wanachama wa cdm ndo hawo kila kitu kupinga hata penye ukweli hakwa nani mi nasema kuchukua nchi hii msahau ...na mnataka msifiwe msifiwe tu...

hongera kibanda kwa mtazamo wako wa kweli na ulioko wazi..kwa sasa CCM imezaliwa upya kabisa kabisa kama zahabu basi wamechimba na kuipata kweli
 
Bado naendelea kusoma michango ya wadau kwenye hii makala iliyo ibua mjadala murua kabisa kufuatilia..

Huu hapa ni mchango wa mwandishi wa kujitegemea na wakili wa mahakama kuu Bw Nyaronyo kicheere (AMBAYE PIA ALIKUWA MGOMBEA WAMUBUNGE KUPITIA CHADEMA BAADA YA KIFO CHA CHACHA WANGWE)kwenye moja ya mitandao kuhusu makala ya Kibanda.

"... Kwanza lililosahaulika ni kwamba wakati wa loliondogate (enzi za mwandishi katabalo) ilidhihirika dhahiri shahiri kuwa kinana aliwasindikiza waarabu hadi kia wakisafirisha twiga, fisi, nyumbu, pundamilia hai na mizoga. kasomeni gazeti la mtanzania la miaka hiyo.

Pili, kinana na wenzake akina mwinyi na ole njoolai, na hata meghji walionekana mara kadhaa wakienda kuswali swala ya jamaa loliondo siku mwarabu mwenye mapesa akiwepo loliondo akiwinda. sasa usiniulize njoolai mkiristu na rais mstaafu wanakwenda ijumaa kuswali!
.

t".




DU.... Haya maneno kayasema kweli Ndugu yangu Nyaronyo?


Kweli fikra za kifashisti zimepata nyumba na nyumba yenyewe ni CHADEMA. Hii inanikumbusha yale ya Mzee Malecela kuitwa Jumanne. Halafu watu wakiambiwa wana gamba la Udini na Ukabila wanakimbilia kuwashutumu wanaowasema kuwa wao ndio wadini. Statement kama hizi ndio viashiria vya gamba hilo la Udini na Ukabila. Kukimbilia kugeuzia kibao wenzenu hakusaidii kuondoa gamba.

Kuna mwengine naona amekimbilia kumshutumu kuwa kitendo cha Kinana kuenda kuripoti CCM akiwa amevaa kanzu (kama vile kuvaa vazi hilo ni kosa) ni njia ya kuwadanganya aliowaita wajinga (waislamu) kuwa CCM ni chama cha Waislamu. Akaendelea zaidi kuwaonyesha wema wa Mchungaji Msigwa wa CHADEMA ambaye hivi karibuni alienda Ujerumani na zawadi pekee aliyokuja nayo ni filamu ile ya kuwatukana waislamu iliyoleta balaa dunia nzima na kufanya maonyesho kadhaa kwa wapiga kura wake...

Sitashangaa kuwa aliyeandika haya ni Mchungaji Msigwa mwenyewe!

CHADEMA jiangalieni sana, matamshi na maandiko kama haya ni moja ya mambo yanayowashitaki na sio propaganda za washindani wenu kama mnavyopenda kujitetea..
 
mwandishi asiyeweza kuisimamia misimamo yake ni mwandishi hatarishi .mfano huyu kibanda ukimuuliza baada ya miezi kadhaa kupita hakumbuki tena,aliandika nini kwa sababu hufuata maslahi ya wakati huo na hili hatasahau alivyolipwa vizuri ,namtakia kazi njema hapo alipo hivi sasa ila ajue kalamu anayotumia itamuuliza alitetea nini demokrasia ,taifa na aliwapa wananchi taarifa gani .
 
Huyu jamaa ama anataka afutiwe kesi au anatafuta cheo. Si muda mrefu atafukuzwa kwenye hilo gazeti na atahamia gazeti la uhuru. Subiri tuone!

kesi inayomkabili kibanda inamsumbua si ajabu amehaidiwa kusaidiwa ktk hy kesi. Pili inaelekea huyu jamaa ni mtaalamu wa kucheza na vinara vya siasa ili apate mshiko na nahisia alishakua na cheo ktk safu ya Chadema Arusha ila sijajua kama bado yupo na hicho cheo. Alikua mstari wa mbele sana kupinga mwenendo wa uchaguzi Igunga na kulaani matumizi ya mabavu yalikua yanafanywa na viongozi wa CCM pamoja na jeshi la Polisi lakini sasa kajeuka kuwa mpaka mafuta wa Kinana. Kinana aliwaambia waandishi wa habari kipindi cha uchaguzi 2010 kuwa Kikwete angeshinda kwa kishindo akiwa kama meneja kameni wake lakini matokeo yakawa tofauti tena baada ya kuchakachua kura ambapo hata mpaka sasa jamaa ushindi wake bado ni utata mtupu. Ama kweli pesa inaweza ikakufanya uwe mke wa mtu hata kama wewe ni mwanaume. Kibanda keshalipiwa mahari na wenye hela na sasa si mzalendo tena ila ni mchumia tumbo.
 
Kibanda ni kibaraka wa mafisadi tu hana jipya. His days are numbered na kinachofuata ili makala zake zipendwe itabidi aandike udaku kama kina SHIGONGO vinginevyo itabidi aamie gazeti la UHURU kabla ya 2015.
 
Tatizo la wana JF wengi humu jamvini ni kutaka kila atakayeleta uzi au kutoa mawazo yafanane na yawe uniform. Ukiwa na wazo tofauti basi shida moja kwa moja. Kibanda ametoa mawazo yake na amejaribu kueleza anavyomfahamu Kinana. Kinachotakiwa kama kuna mtu anamfahamu Kinana tofauti na alichoeleza Kibanda atueleze kwa ushahidi ili tulinganishe alichokisema Kibanda na huo ushahidi mpya. Kuendelea kupuuzana tu bila kuwa na facts si jambo zuri wala hatupati cha zaidi katika JF labda matusi mapya tu.

Inawezekana kabisa Kibanda yuko positive kwa ajili ya ku-alert kutodharau mabadiliko haya mwisho yakaleta negative impact kwenye upinzani. Sio lazima kila kitu tuchukue negative, we sometimes allow our minds to take some issues positively.
 
Mtoi
Hebu nifahamishe tenda aliyojipa mwenyekiti wako Mbowe ya tshs mil. 350 aliidhinishwa na vikao gani? Kama sio ufisadi? Kamanda inaonekana una mapenzi ila mambo ya ndani huyajui! Miezi michache iliyopita mlifanya ghafla kubwa ya kuchangia M4C hivi mpaka sasa hivi umeshapewa mchanganuo wa matumizi ya pesa hizo? Jiulize Lema anahusika vipi na mambo ya fedha wakati yeye si bwana fedha wa chama?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Kibanda kakaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!! Si jana tu ulikuwa ukiwapamba majemadali wetu wakati ukiwa ndani ya Tanzania daima?! sasa hata makala zako ndani ya gazeti hilo hazijafutika tayari umekuwa kama chatu na kuvaa ngozi nyingine kana kwamba wewe si yule wa jana? Duh kweli kaka acha pesa iitwe mwana haramu. Kwaheri kaka, tukutane njia panda 2015.


Mkuu Miwatamu umekosea. Hujayalewa vizuri makala ya Kibanda. Kwa mtizamo wangu, Kibanda ameweka ushahidi kwamba anamuelewa vizuri Kinana kuliko Watanzania walio wengi. Na hilo linatosha kwa yeye Kibanda kutoa angalizo kuhusu nini kiwe mategemeo ya Watanzania kuhusu Kinana katika nafasi aliyopewa.

Wilson Mukama ni Mtaalam wa Utawala wa Kiraia. Kinana ni Mtaalam wa Utawala wa Kijeshi. Badiliko hili la Mtendaji Mkuu katika CCM si kitu cha kubeza, hata kama limetokana na Mukama mwenyewe kukataa kuendelea na kazi aliyopewa, ama kama utakuwa ni uleule utizamo wa kuweka Waislamu katika kila safu nyeti ya CCM.

Wapambanaji katika vyama vya upinzani wawe na mtizamo kuwa huyu mshindani si mtu wa mzaha, na kwamba upo sasa ulazima wa kujipanga vizuri zaidi kupambana na Administrator mwenye mawazo ya Kijeshi.

Kibanda umeweka angalizo muhimu sana katika haya makala makini.

Naomba kuwasilisha.
 
ambae sio wa kawaida anayestahili kutishia ni yupi?!
Haa JF wote tuo sawa lakini ukitoa Mada kuikosoa CHADEMA utakosolewa na mitusi juu.
Kwa hiyo Monyiaichi sio halali kabisa leo kumuona Kibanda hafai na kumshatkia kwa Mbowe afukuzwe kazi Tanzania Daima ni ujinga na utoto kumkosoa mwenzenu aliyeko katika dhana ya Demokrasia
Kuna Toic ngai za Absolom Kibanda za kuikosoa CCM zinaungwa mkono lakini leo upepo unaashiria mabadiliko mnataka yasiandikwe
 
Last edited by a moderator:
Hivi huyu anaeitwa le mutuz ni mpuuzi kutoka wapi? Hivi tz unaweza kuongelea viongozi waasherati bila kumtaja mzee wa kaya? Go to hell le mutuz
 
Absolom Kibanda!Absolom Kibanda! Absolom Kibanda!

Watu husema ushahidi ni mara 3. Nimelitaja jina la huyu mwandishi mara 3 kama ushahidi kwamba alichoongea hapa hakika ni ujinga.ujinga na ujinga mtupu! Kwa watu makini hapa wanaona Bwana Kibanda umeamua KUJIKOMBA KWA KINANA PENGINE KWA KUTEGEMEA KUPEWA CHEO AIDHA KWENYE CHAMA HIKI CHA MAJAMBAZI NA MAFISADI AU CHEO KATIKA SERIKALI INAYOONGOZWA NA THE SAME PARTY!!! HUO NDO UKWELI! If you read between the lines kile alichoandika Kibanda ni kujipigia debe la KUTAFUTA U-DC na ndiyo maana amelitaja Jina la Muhingo RWEYAMAMU kwa msisitizo kuonyesha kwamba huyo ni mwenzake ambaye tayari ni DC wa Handeni baada ya kuiandika vizuri CCM. Sishangai pale mwana vikaragosi maarufu kutoka Kenya BWANA GADO alipochora kikatuni cha Wanahabari wa Tanzania WAKIRAMBA MIGUU YA RAIS KIKWETE WAKTI WA UCHAGUZI MWAKA 2010. Haya ndiyo matokeo yake. KIBANDA AMEAMUA KURAMBA MIGUU YA KIKWETE KWA KUJIKOMBA KWA KUJIKOMBA KWA KINANA!!!!!

Napenda kumwuliza Bwana Absolom Kibanda KWANINI AMEAMUA KUIDHALILISHA TAALUMA YA UANDISHI WA HABARI kwa kujaribu kumpamba mtu asiyapambika Bwana ABDULHAMANI KINANA???Kwa sifa zipi hasa ambazo wewe Kibanda umeamua kumsifia huyu jamaa mpaka kupiliza kiasi hiki? WHO IS KINANA BY THE WAY IN THIS COUNTRY??ANA SIFA GANI HASA MPAKA UMSIFIE KIASI HICHI. Je, yawezekana pengine kwa sababu majina yenu yaani KIBANDA NA KINANA yana mizania fulani za kufanana? Yaani ABsolom KIbanda na ABdurhamani KInana! Kila jina la mhusika na ubini wake lina anza na HERUFI ZINAZOLINGA yaani AB na KI, yawezekana huyu jamaa yetu anaona ulinganifu huu wa mwanzo wa majina kama kitu fulani cha kutaka kufanana na hivyo kwa fikira dhaifu kujaribu kujifananisha na KINANA kwa kumsifia na kumpamba!

Kwa kifupi tu napenda kusema kuwa KINANA SI CHOCHOTE SI LOLOTE. Ule msemo wa kuwa KANZU MPYA SHEHE NI YULEYULE UTAFAA SANA UTUMIKE KWENYE HUU UTEUZI WA SEKRETARIATI YA CCM! Watu wasitegemee lolote jipya kutoka safu hii ya MIZEE YA CCM ILIYOCHOKA,MIFISADI NA MIDIKTETA!!!

Kinana hana ubavu wowote wa kuibadili CCM hata kama angelikuwa na akili gani. Kinana huyu huyu ndiye aliyekuwa MENEJA wa Kampeni za CCM mwaka 2010.Hakuna siri kuwa huyu jamaa ALICHEMSHA na isingelikuwa kuchakachua matokeo kwa kuwatumia UWT(Usalama Wa Taifa) Rais Kikwete mwaka 2010 angeisikia IKULU kwenye magazeti tu!Huo ndiyo ukweli! Kinana alistaafu na cheo cha Kanali kutoka JWTZ mwaka 1972 WAKTI WA UONGOZI WA RAIS MAKINI NA BABA WA TAIFA HILI marehemu JK NYERERE. Just ask thyself huyu KINANA kama kweli alikuwa ni kichwa na kiongozi makini kwanini Baba wa Taifa hakuwahi kumpa huo UKATIBU MKUU wa TANU miaka ile na au mwaka 1977 baada ya CCM kuzaliwa????

Naamini Baba wa Taifa alikuwa mtu makini sana na ndiyo maana aliwahi kumteua marehemu EDWARD MORINGE SOKOINE kuwa Waziri Mkuu mwaka 1977-1980 na 1983-1984! Je, Kinana wakti huo alikuwa wapi? Kwanini asingepewa hata huo u-PM ukiachilia mbali U-KATIBU mkuu wa Chama cha Mafisadi????

Kinana hana sifa wala historia yoyote ya mafaniko katika nchi hii zaidi ya Kampeni za KIBABE za CCM mwaka 2005 na 2010!!!Katika kampeni za 2010 CCM ilishindwa vibaya sana mpaka ikalazimu watumie udanganyifu wa KUIBA KURA chini ya KINANA na hakika kama wasingetumia mbinu za wizi wa kura CCM walikuwa wamepigwa chini. Kushindwa kwa Kikwete au kushuka kwa matokeo ya kura za Watanzania kwa KIwete ilikuwa ni dalili tosha kuwa CCM walishindwa na kwahiyo ilikuwa kushindwa kwa KINANA kama Meneja Kampeni na ataendelea kushindwa hata akiwa Katibu Mkuu. Mwaka 2015 iyo mbali. Tusubiri halafu watu wataelewa kile ninasema!

Rais Mstahafu wa Afrika Kusini Bwana Thabo Mbeki katika ziara ya kuitembelea Tanzania AMEICHANA CCM KWA KUWEKA BAYANA KWAMBA TANZANIA HAIENDELEI NA HAITAENDELEA kwa vile inaongozwa na WAZEE WALIOCHOKA KIAKILI,KIMWILI NA KIROHO. They shall NEVER deliver anything to this country and all Tanzanians zaidi ya KUENDELEA KUIFISADI NCHI HII!!!

Huu ni ukweli mchungu kwa CCM na lazima waukubali ili wabadilike. Kuendelea kung'ang'ania madaraka huku wakiwalaghai vijana kuwa ni Taifa la kesho ambayo haifiki ni uhuni,usanii na ubabaishaji uliopitiliza.

Nitaendelea
 
KWA wapenzi wa nyimbo za injili, watakuwa wanamfahamu mwimbaji mahiri nchini aitwaye Rose Mhando. Na kwa wapenzi wa nyimbo zake, bila shaka watakuwa wanaufahamu mmoja ulio katika albamu yake ya mwisho uitwao ‘Woga wako'.

Katika moja ya makala zake miezi kadhaa iliyopita, Mhariri Mtendaji wa gazeti hili, Absalom Kibanda, aliutumia wimbo huo wa Rose Mhando kuchambua utendaji wa Rais Jakaya Kikwete.

Aliiandika makala hiyo wakati wa mwanzo wa vuguvugu la kumtaka Rais Kikwete afanye mabadiliko ya Baraza la Mawaziri kutokana na wengi wao kuonekana na jamii wanayoitumikia kuwa wamepwaya.

Maudhui ya makala hiyo ya Kibanda yalilenga katika kumwonya Rais Kikwete kuwa woga wake katika kufanya hilo linalodaiwa na jamii ndilo tatizo kubwa kuliko hata kupwaya kwa mawaziri ambao anapaswa kuwashughulikia.

Lakini niliposoma, katika wiki mbili zilizopita, makala mbili za Kibanda akielezea umahiri wa Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, nikahisi kuwa naye ameingiwa na hofu.

Ingawa hofu yake siyo kama ile ya Rais Kikwete aliyoieleza katika makala zake za awali, lakini hata Kibanda mwenyewe alieleza katika makala yake ya awali kuwa hofu inaweza kuzaa madhara mabaya. Hivyo, hofu ya Kibanda kwa Kinana nayo inaweza kuwa na madhara makubwa.

Katika makala zake mbili za hivi karibuni, Kibanda anamwonyesha Kinana kama kiongozi mahiri ambaye kuwepo kwake ndani ya CCM, kunaweza kuleta mabadiliko makubwa chanya kwenye chama hicho ambacho katika miaka ya hivi karibuni kimekuwa kikipoteza mvuto kwa jamii.

Kibanda anaeleza kuwa, uongozi mahiri wa Kinana unaweza kukibadilisha chama hicho na kuwa makini na cha kuogopwa, hasa na vyama vya upinzani.

Nakubaliana na Kibanda kuhusiana na uhodari wa Kinana katika uongozi. Historia inamwonyesha kama mmoja wa viongozi wenye muono wa mbali kwa kila jambo analolifanya.

Siyo mtu wa kukurupuka, lakini kizuri zaidi kwake ni mtu ambaye haoni lawama za kujenga (constructive criticism) kuwa ni tatizo kubwa. Lakini hili halipaswi kumtia hofu Kibanda au mtu mwingine, na nitatoa sababu kadhaa katika kuelezea kwanini naamini hivyo.

Sababu ya kwanza ni kuwa Kinana ni mvinyo (kiongozi) mpya katika chupa (CCM) ya zamani. Kuwa katika hali hii kuna madhara mawili makubwa. Kwanza, kuna uwezekano mvinyo ukawa na nguvu zaidi kutokana na upya wake na zikashinda uimara wa chupa ile ya zamani. Hivyo, siyo ajabu chupa ikapasuka.

Lakini madhara mengine yanayoweza kutokea kutokana na hali hii ni kuwa, wapo watu ambao wanaiona chupa kwa nje kama walivyoizoea na wakashindwa kuuona mvinyo mpya uliotiwa ndani ya chupa.

Hali hii inaweza kushadidishwa na wahafidhina (conservatives) ndani ya chama. Matokeo yake kuna uwezekano jitihada za Kinana kutaka kuleta mabadiliko zikaonekana kama njama za kutaka kukiharibu chama, hasa kwa watu ambao wanaiona chupa ya mvinyo kwa nje bila ya kutaka kujishughulisha kujua ndani yake kuna nini.

Na hili linaweza kutokea kutokana na sababu ya pili kuwa, kuna kundi kubwa la wanaCCM ambao wanafaidika na hali ilivyo sasa. Pia, kuna kundi kubwa la wanaCCM ambao hata kama hawafaidiki na chama, wanakifahamu kilivyo hivi sasa.

Kwao hawa, kutaka kuibadilisha hali hii linaweza kuwa jambo ambalo halieleweki kirahisi. Itamuwia vigumu sana Kinana kufanya kazi katika mazingira haya.

Sababu ya tatu ni migawanyiko iliyopo CCM. Kinana anaweza kuwa kiongozi mahiri sana, lakini asipokuwa mwangalifu anaweza kujikuta katika hali ya kujitetea (defensive) zaidi kwa sababu ni dhahiri kuwa wale watakaoathirika na anayotaka kuyafanya ndani ya chama hawatakaa wakimwangalia akiwanyang'anya kitumbua chao mdomoni.

Na tangu kuasisiwa kwa mitandao ndani ya CCM, tumeshuhudia jinsi ambavyo watu wanavyotumia njia na mbinu mbalimbali kuhujumu wale ambao wanaamini kuwa ndiyo maadui zao ndani na nje ya chama.

Kinana anaweza kujikuta katika kundi hili la kuhujumiwa ndani ya CCM. Hii inatokana na kuwa, kuna makundi mengi ndani ya CCM ambayo yanatetea maslahi tofauti. Tatizo kubwa ni kuwa kati ya makundi hayo, ni kundi dogo sana linaamini katika CCM halisi (original).

Nne, umahiri wa Kinana unaweza usifue dafu kwa umahiri mwingine unaoonyeshwa hivi sasa na vyama na wanasiasa walio katika kambi ya upinzani. Hili litamuwia vigumu zaidi Kinana kwa sababu atakuwa pia na mpambano mwingine ndani ya CCM.

Haitawezekana kwa yeye kupambana na upinzani, huku CCM ikiwa imegawanyika. Hivyo, ni lazima ahakikishe kuwa anajenga umoja na mshikamano ndani ya CCM (jambo ambalo anaweza asifanikiwe) kabla hajaukabili upinzani kisawasawa.

Wakati atakapokuwa anaendeleza mapambano ndani ya CCM, huku upinzani utakuwa unazidi kukata mbuga. Pia, wakati akiiweka CCM sawa, mapambano yao ya ndani yanaweza kuzaa migawanyiko ambayo itaunufaisha zaidi upinzani.

Sababu ya tano kwa Kibanda kutokuwa na hofu kutokana na Kinana kupewa nafasi hiyo, ni kuwa pamoja na kuiweka sawa CCM na kuukabili upinzani, lakini ana mpambano mwingine na watendaji wa serikali.

Baadhi ya viongiozi wa juu wameshaonyesha hisia zao kuwa kuchukiwa kwa CCM kunatokana na baadhi ya watendaji serikalini kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Hata Kinana ameonyesha wazi kutoliunga mkono suala hilo kwa kiasi fulani. Hii inaweza kumuweka katika nafasi ya kuhujumiwa pia na baadhi ya watendaji wa serikali ambao hawatapenda kuona maslahi yao yakivurugwa.

Sababu ya sita ya kutokuwa na hofu ni kuwa mwamko wa wananchi wengi hivi sasa umefika mahali ambapo itachukua muda mrefu na kazi ngumu sana kuweza kuwarudishia imani na mapenzi yao kwa CCM.

Watu wamekatishwa tamaa kiasi kuwa ni vigumu sana wao kuiamini CCM au serikali yake. Waliaminishwa kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana, lakini kwa miaka takribani saba hivi, walichoshuhudia ni kuzidi kudidimia kwa hali zao za maisha.

Tumeshuhudia Kinana na wenzake wakiendeleza mtindo wa kutoa ahadi kwa Watanzania kuwa wamejipanga kubadilisha hali zao. Lakini wameshachoshwa na ahadi. Wanachotaka wao kukiona hivi sasa ni kuona haya mabadiliko yaliyoahidiwa.
Mwamko wa wananchi wengi umefika mahali ambapo siyo rahisi sana kuwarubuni.

Sababu ya saba ni kuwa kama Kibanda anaamini kuwa Kinana atafanikiwa katika hayo anayotaka kuyafanya, na iwapo atafanikiwa kweli, matokeo yake, kwa kiasi kikubwa itakuwa ni kuboreka kwa maisha ya Watanzania, na hilo ndilo ambalo linatafutwa siku zote.

Source: Tanzania Daima
 
Labda na mimi nina akili kama za samaki (AMK 2012) Ninaomba nitajiwe moja baada ya nyingine hayo mabadiliko MAKUBWA chanya wanayosemwa atayaleta Kinana ndani ya CCM ni yapi?

Maana mimi ninasikia mabadiliko, mabadiliko, mabadiloko, mabadi..... lakini ajabu hayo mabadiliko hayatajwi. Je ni yapi hayo? anayefahamu naomba anieleze ili ndiyo iwe YARD STICK ya kupima huo UMAHIRI wa Kinana.

Tunajua YARD STICK ya Mukama ilikuwa KUJIVUA GAMBA baada ya kushindwa kuliondoa gamba amefurumushwa. Je Mabadiliko Makubwa ya Kinana ndani ya CCM ni yapi?!
 
Kinana mabadiliko atakayoleta ni kuongeza nguvu ya kuua Tembo na meli zake kusafirisha meno ya tembo kupeleka mashariki ya mbali
kwa biddii zote kusaidia wahamiaji haramu wa kisomali na kutengeneza network nzuri ya kuwalinda wakiingia Arusha

kwa bidiii zote kusaidia kudhulumu maisha ya wananchi kwa kuficha rushwa na madhambi ya viongoi wa CCM
tutarajie mengi
 
Hizi ni sarakasi za kisiasa. Kinana hawezi kufanya lolote chanya iwe la kuisafisha au kuihuisha CCM. Ni msemo wa "nikune mgongo wangu nami nikukune wa kwako"

Sasa hii media frenzy ni a calculated game to fool the masses. Hawa akina Kibanda na wenzao wamenunuliwa kwa dau kubwa tu - hii ni plan A. Plan B ikiwa CCM haitaweza kuwanunua wahariri na vyombo vya habari vya kutosha, then watatumia vitisho na hata wengine watapoteza maisha.
 
Njaa mbaya sana, wakati mwingine huwalazimu Waandishi wetu kukosa haya...kibanda alipotoka period...
 
Njaa mbaya sana, wakati mwingine huwalazimu Waandishi wetu kukosa haya...kibanda alipotoka period...

Mlisema kuwa tarehe mosi disemba bwana kibanda ataripoti new habari corporation , je taarifa hizi zimefikia wapi
 
Back
Top Bottom