Wanajamvi, Salaam.
Leo nakuja kwenu jamvini baada ya kukerwa na tabia ya Mwenyekekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Absalom Kibanda kutumia kuteswa na kutekwa kwake kama biashara. Amekuwa anaongea kwa ndimi mbili.
Mara ya kwanza alizungumzia kutekwa kwake kwa namna ambayo ingefanya jamii itafsiri kana kwamba Mwajiri wake wa zamani Gazeti la Tz Daima kupitia wamiliki wake ndio walihusika.
Alipohamia New Habari Cooperation akaishambulia Chadema mpaka tukaaminishwa kuwa huenda Chadema walihusika. Aliwahi kumtaja moja kwa moja Bw. Ludovick Joseph kama mmoja waliomteka.
Huyu Ludovick alikuwa kada wa Chadema katika kesi kigaidi ilipikwa pamoja na mwandishi uchwara Denis Msacky ambayo ilimlenga mkurugenzi wa Ulinzi na usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare, ambayo inasemekana Zitto Kabwe pamaoja na Chama cha Mapinduzi wakiwa wabia muhimu.
Kwa sasa vita ya urais ndani ya CCM imepamba moto. Kibanda ni mhariri mkuu wa gazeti la Mtanzania. Hili gazeti lina kazi maalum ya kumpamba Eddo na kuchafua wenzake.
Juzi Kibanda ameibuka na tuhuma mpya kabisaa, Anamtuhumu mgombea urais mmoja kama mhusika wa tukio la kutekwa na kuteswa kwake. Huyu mgombea urais anatokea mikoa ya kusini, mwandani wa familia ya mkuu wa kaya. Chaguo la mama wa taifa.
Kwa kuwa huyu ndiye mpinzani mkuu wa Eddo, ni dhahiri kuwa Kibanda kwa maagizo ya waajiri na pia kwa utashi wake binafsi, amekubali kutumia kutekwa na kuteswa kwake kama Chanzo kipya cha mavuno.
Yupi mtekaji na mtesaji halisi wa Kibanda, ikiwa na yeye mwathirika amekubali kuuza utu wake kama bidhaa?