kabla ya kuanza kutoa maoni yangu juu ya jambo la matukio ya utekaji hapa Tanzania naanza na suala la Joseph Yona, Mwanaharakati huru, ambaye ametumia kitabu cha Dr. Slaa, katibu mkuu wa mstaafu wa CHADEMA, alichokiandika mwaka 2015, kinachoitwa Nyuma ya Pazia, Chadema iliyosalitiwa 2015.
Kwa mujibu wa maelezo yake inaonyesha kuwa masuala ya utekaji yana pangwa na Chadema (
View: https://www.youtube.com/watch?v=juEcMRwC0VU), kwa upande wa Chadema, Mbowe alisema kuwa utekaji unafanywa na Jeshi la Polisi na taasisi zingine
(
View: https://www.youtube.com/watch?v=j3tYtW7BXf8).
Kwa mawazo hayo mawili, upande wa Mbowe na upande wa Joseph Yona bado naona kama masuala ya utekaji yana sura ya kisiasa. Mimi binafsi Jeshi la polisi nalipongeza sana na naliamini kwa utendaji wake, mara zote Jeshi limekuwa likishughulikia masuala haya ya utekaji kwa uwazi .
Kwa mfano, taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kuhusu watu kupotea na kukutwa wameuawa huko Singida kwa mganga, huo ni uwajibika wa hali ya Juu.
Kwa mantiki hiyo, naomba tuondokane na dhana ya kuwa Jeshi la Polisi linaweza kuteka wananchi wake halafu liwatafute lenyewe.
Mimi ningependa sana badala ya kulaumu Serikali au Jeshi la wananchi kuhusu suala hili la utekaji kuna haja ya kuwaelimisha wananchi kuhusu majukumu yao ya msingi katika ulinzi wao binafsi na mali zao.
Mfano, mwingine taarifa ya kuhusu miili ya Ray na Liziki iliyofukuliwa kwa mganga Ligunga huko Tunduru (
View: https://www.youtube.com/watch?v=60-XcwGVK_s&t=4s), matukio haya ukweli yanaonyesha namna Jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla namna linavyotenda haki kwa mujibu wa sheria. Je, ni kweli kwamba polisi wanaweza kuwateka watu na kuwapeleka kwa waganga? wananchi wanatakiwa kuelimishwa na kujua uhalisia kuliko kufuata upotoshaji unaotolewa na baadhi ya viongozi wa dini na wanaharakati.
Pia, pitia taarifa za Jeshi la Polisi kuhusu taarifa za utekaji na namna lilivyoshughulikiwa kwa weledi (
View: https://www.youtube.com/watch?v=pxiIn0UMX34) na
View: https://www.youtube.com/watch?v=kBrUSvJfq3I