King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Hongera sana kwa kununua gari.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ushauri bora kuliko wote.Jaribu kuangalia haya mambo mawili utapata jibu sahihi juu ya hiyo shida..
La kwanza washa gari yako harafu funua bonet washa ac angalia kama ile clutch ya compresorr ime engage na inazunguka..kama NO haizunguki basi shida inaanzia hapo..
Kama haizunguki basi kuna mambo mawili yanayoweza kusababisha
La kwanza shida upande wa umeme?? Umeme haufanyi kazi au haufiki kubana compressor??..
La pili gari haina gesi..gari ikiwa haina gesi compressor haiwezi kubana..
Kutambua kama gari ina gesi ni rahisi kwenye pipe ya ac huwa kuna kuwa na kifuniko fungua chukua kijiti bonyeza uone kama kuna gesi hapo kuwa makini na macho usielekeza macho hapo hapo unapo bonyeza..pili yatakiwa gesi itoke na sio hewa ya pressure..
Na kama gari ina shida ya gesi imekwisha nenda kwa fundi sio akujazie gesi bali akafuatilie sehem yenye likage na sio kujaza tuu gesi..maana gesi huwaga haiishi ikiisha basi kuna mahali inavuja
Hapana...swali lina msingi tu kwa anayeweza kulijibu...Wewe sasa una yako.
Mkuu hilo swali yawezekana sio size yako na sio swali la kawaida bali lina mantiki na technical za kifundi ndani yake gesi ya ac kwenye gari haiishi kama yanavyoisha mafuta.au vilainishi kwenye gari..Nenda kajazie fundi ndiyo atakuambia inachukua muda gani.
Umeongea kisomi kabisaaJaribu kuangalia haya mambo mawili utapata jibu sahihi juu ya hiyo shida..
La kwanza washa gari yako harafu funua bonet washa ac angalia kama ile clutch ya compresorr ime engage na inazunguka..kama NO haizunguki basi shida inaanzia hapo..
Kama haizunguki basi kuna mambo mawili yanayoweza kusababisha
La kwanza shida upande wa umeme?? Umeme haufanyi kazi au haufiki kubana compressor??..
La pili gari haina gesi..gari ikiwa haina gesi compressor haiwezi kubana..
Kutambua kama gari ina gesi ni rahisi kwenye pipe ya ac huwa kuna kuwa na kifuniko fungua chukua kijiti bonyeza uone kama kuna gesi hapo kuwa makini na macho usielekeza macho hapo hapo unapo bonyeza..pili yatakiwa gesi itoke na sio hewa ya pressure..
Na kama gari ina shida ya gesi imekwisha nenda kwa fundi sio akujazie gesi bali akafuatilie sehem yenye likage na sio kujaza tuu gesi..maana gesi huwaga haiishi ikiisha basi kuna mahali inavuja
Habari.
AC katika gari yangu haitoi ubaridi kabisa. Inatoa upepo kwa nguvu tu, ila upepo hauna ubaridi wowote.
Mfano, jana nilijaribu kuwasha feni hadi mwisho nikiwa nimezima AC na nikiwa nimewasha AC. Hakuna utofauti kabisa.
Kama haitoshi, nikiwa nimewasha feni hadi mwisho, nikaongeza joto hadi mwisho (32 Degrees of Celsius) lakini sikuona utofauti wowote na nikiweka baridi hadi mwisho (16 Degrees of Celsius).
Kwa kifupi, feni inatoa upepo vizuri tu, lakini ubaridi hakuna kabisa.
Gari langu ni jeusi kwahiyo na joto ili la Dar (mfano jana niliona 36 Degrees) jumlisha na foreni, raha ya gari siioni sana.
Msaada wa mawazo, fundi au ushauri wowote.
Location: Ubungo, kama aina ya gari ina matter ni Runx 2002.
Bro.
Nimeangaika mafundi wanasema inavuja ila wapi. Nimeishia kujaza gesi na kusubiri iishe nijaze tena.
Sijaenda kwa Makofia mzee.
Kweli...gari nying za leo zinatumia gas 134a kwa ajiri ya ac... So huyu jamaa kitendo cha ac kutoa barid kunasababu kadhaa, mfano gas kuisha kutokana na leakage, ac clutch kuto-ku-engage, kuharibika kwa pressure sensors, compressor yenyewe kufa, expansion valve kutofanya kazi, peleka kwa fund anaejua nin anatakiwa kufanya...kwa kutumia gages kupata readings unaweza pata majibu.. Fundi hatakiwa ku-overfill or underfill the system.. Pia wakat wakufanya re-gasing anatakiwa ajue pressure reading hutofautiana kulingana na temperature ya wakat huo.. So nivema kujua pressure range kwa kila range ya prevailing atmospheric temperature.Mkuu
Mkuu hilo swali yawezekana sio size yako na sio swali la kawaida bali lina mantiki na technical za kifundi ndani yake gesi ya ac kwenye gari haiishi kama yanavyoisha mafuta.au vilainishi kwenye gari..
Ac huwa haiishi na ukiona inaisha ujue gari yako ipo na shida ni sawa na gesi kwenye fridge.unaweza nunua gari mpaka inakufa 20yrs unakula tuu kiyoyozi lkn ukiona umeanza sound za kupungua nenda kafanye service ya ac na sio kujaza gesi..lazima kuna sehem kuna shida..
Pili kwenye magari kuna aina tofauti za gesi hili 99% watumiaji wa magari na mafundi wengi hawafaham pia wao wanajaza tuu magesi ya kichina .hapo ndio shida zaidi huongezeka fundi gesi anajaza gesi hata gauge hana zaidi yeye anaangalia kaubaridi kakianza tuu kutokeza kwa ndani basi anachomoa mtungi..
Baada ya miezi miwili mitatu imezingua tena gesi zingine feki na sio sahihi kwenye magari matokeo yake ni shida tupu.