KERO AC zilizopo kwenye mabasi ya Mwendokasi zimebakia kuwa mapambo? Hazifanyi kazi, abiria tunateseka na joto

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Licha ya awali usafiri wa Mwendokasi kuvutia watu wengi lakini kwa siku za hivi karibuni abiria wengi wamekuwa wakilalamikia changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza kwa nyakati tofauti.

Kwa kipindi kirefu kidogo (wastani wa miezi sita) niliamua kujipa jukumu la kizalendo kufuatilia suala la miundombinu ya ufanyaji kazi wa miundombinu ya AC ambazo zimefungwa kwenye magari.

Kufuatia udadisi wangu wa kina nimebaini magari mengi ya Mwendokasi, AC hazitumiki, kuna magari ambayo yana AC hadi nne lakini hakuna moja ambayo inaonekana kufanya kazi.

Suala hilo nimelibaini katika magari yote ambayo nimeyapanda mara kwa mara katika kipindi cha miezi sita ambayo nilijipa muda wa kufuatilia changamoto hiyo.

Kutokana na miundombinu hiyo kutotumika imechangia kwa kiwango kikubwa abiria wengi wanatumia usafiri huo kuathirika kutokana na hali ya joto kwenye magari mengi.

Kutokana na uhaba wa magari ambao unapelekea mabasi yaliyopo kupakia abiria wengi kwa wakati mmoja, suala hilo linasababisha uwepo wa joto ambalo kama AC au feni zingekuwa zinafanya kazi lingeepukika kwa kiwango fulani.

Kwa mara kadhaa kutokana na joto baadhi ya abiria wamekuwa wakidondoka ndani ya usafiri huo kisha kupepewa na abiria wanaojitolea, lakini pia changamoto ya joto imekuwa ikiwapa mazingira magumu wajawazito na kufanya usafiri huo kutokuwa rafiki kwao.

Suala hili linanifanya nihoji juu ya uwajibikaji wa mamlaka zinazosimamia mradi huo, kama zimeshindwa kuzingatia usalama wa afya za abiria wao kwa kutumia miundombinu hiyo au nini kipo nyuma ya pazia?

Inafahamika kulingana na mazingira ya Jiji la Dar es salaam kwa mara nyingi kiwango cha joto kinakuwa juu, kutokana na hali hiyo sidhani kama mamlaka husika zinashidwa kuhakikisha miundombinu hiyo inafanya kazi stahiki.

Nitoe wito kwa mamlaka za juu kufuatilia suala hilo kama miundombinu imeshindikana kufanya kazi basi hata zifungwe feni kama njia ya dharura ambazo zitasaidia kupunguza joto kama hali ilivyo sasa.
 
Yaani Waafrika hakuna tunachoweza kusimamia na ndiyo maana jamii zingine zinatuona wajinga wa kutupwa kabisa. Hapa usikute wafanyakazi wao wenyewe ndiyo wamaua hizi A/C ili waibe spea na wako kazini mpaka hivi sasa wanachekelewa tu kwa kuitia serikali hasara.
 
Hayo mabasi hayana mfumo wa AC ....ILA KUNA VENTS NA FENI NDOGO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…