ACACIA yatangaza udhamini mnono kwa Stand United ya Shinyanga, ni wa miaka miwili

ACACIA yatangaza udhamini mnono kwa Stand United ya Shinyanga, ni wa miaka miwili

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
_DSC0629.jpg

Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United ya Shinyanga, Amani Vincent akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

Kampuni ya uchimbaji madini ijulikanayo kwa jina la Acacia Mining imetangaza nia ya kuidhamini timu ya Stand United kwa misimu miwili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Akizungumza jijini jana, MenejaMkuu wa Kitengo cha Huduma za Maendeleo ya jamii ya kampuni hiyo, Asa Mwaipopo alisema kuwa hatua hiyo ni moja ya kuendeleza shughuli za kampuni yao katika shughuli za kijamii.

Mwaipopo alisema kuwa timu ya Stand United imeundwa na wanajamii wa Shinyanga na wanaamini kuwa udhamini wao kwa klabu hiyo utaleta tija na kufanya vizuri katika ligi kuu ya Tanzania Bara.

Alisema kuwa kampuni yao ina migodi miwili mkoani Shinyanga ambayo ni Bulyahulu na Buzwagi na hivyo ni maeneo muhimu ya biashara yao.

Alifafanua kuwa wamekuwa wakifanyakazi pamoja na timu ya Stand united kwa muda mrefu na sasa wameamua kukuza uhusiano wao ambao utakuza vipaji vipaji, kuifanya timu hiyo kujitegemea na kufanya vizuri katika ligi.

"Mpira wa miguu ndiyo unaoongoza kupendwa duniani, mchezo huu unawapa fursa watu wa rika tofauti kukutana na kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo, tunaamini timu ya Stand United itatumia fursa hii kwa manufaa na si vinginevyo," alisema Mwaipopo ambaye hata hivyo alikataa kusema kiwango cha fedha ambacho watatumia kuidhamini timu hiyo. Mkataba wa udhamini utasainiwa katikati ya mwezi ujao.

Mwenyekiti wa Stand United Amani Vincent aliishukuru kampuni hiyo kwa kutangaza nia hiyo ya kuwadhamini na kuifanya timu yao kuwa bora hapa nchini.

"Tunaamini kwa kupitia udhamini huu, timu yetu itafanya vizuri katika ligi na kutwaa ubingwa, tutasajili wachezaji bora na vile vile kuhimarisha benchi letu la ufundi," alisema Vincent.

Vincent alisema kuwa wachezaji wengi vijana na nyota sasa watataka kujiunga na timu hiyo ambayo wanatarajia kuwa miongoni mwa timu shindani katika ligi kuu ya Tanzania Bara.

"Timu yetu itakuwa mingoni mwa bora hapa nchini, kikwazo kikubwa cha mpira wa miguu ni fedha, tunatarajia kupata udhamini mnono ambao utatuwezesha kusajili wachezaji wazuri mbali ya kupata walimu wazuri," alisema Vincent.

Chanzo: DewjiBlog
 
Wangeinunua kabisa kama ilivofanya kampuni ya azam, dawa ni hiyo tuu hakuna namna nyingine
 
Ndo mana wamepata na ubavu kumleta Prof. Patrick Lewig kua head coach wao.. Kila la la kheri "wakokaya".
 
Back
Top Bottom