Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Benki ya 'Access Microfinance Bank Tanzania (AMBT)' yenye makao makuu imeuzwa kwa kampuni ya kitanzania ya Selcom kama mwanahisa mkubwa zaidi na sasa itajulikana kama 'Selcom Microfinance Bank'. Uwekezaji wa Selcom unaifanya benki hiyo kufikisha mtaji wa zaidi ya Sh 8.6 bilioni.
Kampuni ya Selcom Tanzania ilianzishwa mwaka 2001 kwaajili ya kusambaza vocha za malipo kabla za kampuni ya Celtel(sasa Airtel). Kwasasa Selcom inamiliki mtandao mkubwa zaidi wa mashine za malipo(POS) zinazokadiriwa kufikia ishirini na tano elfu na kuziunganisha zaidi ya benki 40 kwenye 'mobile banking' na wafanyabiashara zaidi ya 100,000 kwenye 'SelcomPay'