Ogah,
Nafurahi kuwa mambo ya barabara unayafahamu. Maana baada ya kuona neno transition curves, nimeona kuwa kuna kalufundi ka barabara hapa.
Kwanza nianzie kuwa sijui kama nimekuelewa au wewe umenielewa. Ninaposema Lane ya barabara ni kuwa kipande kimoja cha barabara ambacho magari yanapita kwenda upande mmoja. Sasa upana wa 3.75m wa lane, huo uko kwenye high way pekee na Express Roads. Hizi nyingine zinakuwa chini ya hapo. Hii ni barabara maeneo ya Mikumi. Kama sikosei itakuwa na upana wa 3.5m kwa lane moja na upana wa barabara nzima ni 7.0m.
Ukiangalia hii kwa eneo hili inatosha sana. Kujenga double road hapa inakuwa kuongeza gharama za bure maana magari ni machache sana. Ila tu, hiyo inakwenda na kupunga speed kwa magari. Nafikiri kwa barabara kama hii inatakuwa kuwa 90km/hrs (maximum). Ila sitashangaa kusikia watu wanakwenda 150km/hrs speed ambayo nchi nyingi duniani hata kwenye highyway huruhusiwe. Ni Wajerumani pekee kama sikosei kwenye baadhi ya highway zao, unaweza kwenda speed ambayo ni akina Veyron, Ferrari, Porsche et el wanaruhusiwa kutumia lane ya ndani maana huko hakuna limit ya speed. Ukiingia wewe na sijui akina Toyota Celica, utawasikia jamaa wanavyokupigia horn, uondoe hilo tractor lako huko kwenye lane ya BIG BOYS.
Sasa ili wapunguze speed, hapo huwa hata Traffic wanasema wazi kabisa wakikumata "una bahati mbaya maana tunafahamu kuwa woote wanavunja max. speed limit". Sanasana wanaangalia nani kazidisha sana kile kiwango na huyo ndiyo wanamfukuza. Na magari yao Polisi ni kichekesho sana. Kuna kipindi kwenye TV nilishawahi kuangalia, gari la Polisi Opel Corsa ikaanza kuifukuza Ferrari. Jamaa akaona leo ngoja awaache kwenye mataa POLISI. Mama yangu, kile Ki-Opel kilikuwa kinakwenda hadi 350km/hr. Jamaa alivyosimama, akatoka nje na kuanza kuwauliza Polisi kama ile kweli ni Opel
🙂
Nakubaliana na wewe kitu kimoja, NI MARUFUKU kuweka kona kwenye bonde au mlima. Hapa wala haihitaji kuongeza upana wa barabara kwani HURUHUSIWI kulipita gari kwenye kona au mlima. Lile eneo la ile ajali, kuna bonde na kuna kona. Nashindwa kuelewa Mhandisi aliyeruhusu ujenzi wa hiyo barabara. Walau wangelizitenga kabisaaa hizo barabara kwa kuweka ukuta au fance katikati ili milele kuzuia watu ku-overtake kwenye maeneo hayo. Hiyo ya pili hapo chini ni nzuri sana kwani mnaweza kuindoa kwa muda na kuruhusu magari kutumia upande mmoja tu. Kuongeza upana wa Lane kunaongeza tu comfort ya kuendesha, ila hakusaidii sana kuongeza usalama. Lile eneo inatakiwa WALAZIMISHE madereva wafuate sheria. Kila njia itumie kuwalazimisha madereva. Hili la eti madereva wetu wazembe, si kweli. Binadamu ni kama Wanyama. Ukimpa mita moja, atachukua km1. Sasa dawa ni kumpa nini ili achukue 1m?