Watanzania bana...sijui kwanini mchawi wetu alituachia akili za kuvuka barabara tu..
Mtu kaweka nafasi ya kazi. Katoa details za mshahara, aina ya employment (Part Time), na sehemu ya kazi (Dar au Iringa). Lakini kwa sababu zisizo za msingi watu mnabeza "oh sijui kwa mshahara huo utawapata wahasibu wenye njaa. oh sijui kwa mshahara huo, lazima mhasibu acheze na transaction. Oh sijui blah blah blah."
Kwa nini lakini? Mbona tuko hivi? Yaani badala ya watu kudadisi kuhusu job functions ya hiyo position (kabla ya kushambulia kiwango cha mshahara), mnakejeli. Yaani kusoma neno "Accountant" tayari mmehusisha na "heavy duty" procedures. Au ni hiyo term P/L na volume ya 100m ndio imewafanya mfikirie kuwa ni lazima itakuwa kazi ya kutoa jasho kwelikweli? Ni vipi ikiwa kazi ya journal entry/data entry (yes kazi nyingi za journal entry wanazipa title ya accountant) au Accounts Receivable/Payable job, bado mtataka mlipwe nusu milioni kwa mwezi?
Halafu mwingine anaomba afafanuliwe kama mshahara uko kwenye currency ya $, Tshs, Kshs or other. Yaani nini kimekufanya ufikirie kuwa hiyo namba inaweza kuwa kwenye currency nyingine zaidi ya Tshs? Je ni Accountant, P/L, or 100m, TRA, VAT or Computer literate???
Tuache hizi tabia za kukimbilia kuzodoa. Zinabomoa. Swali la msingi la kumuuliza aliyepost hiyo kazi ni kuorodhesha job functions kwanza. Then tutajadili kutoka hapo (kama ikibidi).