Acha Baadhi ya Marafiki wako Waondoke Usiogope

Acha Baadhi ya Marafiki wako Waondoke Usiogope

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Haya maisha raha sana, mwaka huu baada ya kutembelea Tunduru miezi kadhaa ilopita, nikarudi town, punde baada ya kurejea sikupata simu, meseji, wala chats toka kwa baadhi ya marafiki wa karibu.

Nilijiuliza sana sana niliona kama masihara vile, baada ya siku tatu Mama mchungaji Lt akanipigia simu.

Akasema mwanangu nikuulize swali, nikajibu ndio, akasema vipi mahusiano yako na marafiki zako uliowazoe yanaendeleaje?Nikajibu hayako vizuri hawanitafuti wananikwepa na wako kimya.

Akasema ndio majibu ya yale maombi mwanangu, usiogope hata shambani tunafanya parizi, tunatoa magugu, Mungu ametenda hao ndio waliokuwa ngedere katika maisha yako. Usiogope mwanangu hawatarudi tena kwenye maisha yako.

Basi ninashukuru sana na nina amani tele. Mungu yupo tumpe nafasi nafsini mwetu.

Best wishes Usiogope kupoteza marafiki wabaya Mungu anatenda.

Good day!
 
angemalizia ......hao marafiki watakuja tu msibani kuaga na kuzika ......

ipiganie familia yako, sio marafiki wote ni wema sanaa ata ka mpo mwaelezana kila kitu mfanyacho hamfichani
Guys I tell you kuna watu wanakuwa karibu na wewe Kwa Nia mbaya Mungu akiwafukuza kwako ni Nuru turufu ya mlango wa maisha mazuri amini hilo.
 
Wanasema "small circle" ni kwa wakishua tu, Kama ni mwenzetu na sie, usije ukajiweka mbali mzee, utajuta. Rasilimali watu inamatter sana hasa kwa maisha ya kibongo bongo.
My friend hii ipo kiimani zaidi, amini Ibilisi akitoka acha aende maana ni kusudi la Mungu
 
Guys I tell you kuna watu wanakuwa karibu na wewe Kwa Nia mbaya Mungu akiwafukuza kwako ni Nuru turufu ya mlango wa maisha mazuri amini hilo.
Well said.. wanataka kumonitor kila hatua ya maisha yako... ili wapate upenyo wa kupandikiza mabaya..
 
Watu wengi waliofanikiwa na wanaofanya MICHONGO pamoja wengi sio MARAFIKI ila ni watu ambao Wana mindset moja yakujiongeza kimaisha ...ila KAMWE MARAFIKI WAKO usiwatenge JUMLA walisiliana NAO kwenye ishu za msingi...Yaan Sherehe na misiba hata kama unaona wanakurudisha nyuma usiwatenge kabisa
 
Naomba ushauri kidogo nina marafiki ila tuanze na huyu tunapiga nae kazi fresh tu yeye ndo ananiita vikazi vikitokea, shida moja anadharau ndugu zangu na kusema vibaya wakati mi hajui naumia, kwa sasa nimekaa kimya, ila najua nayoongelewa huko sijui tu, au mimi ndo rafiki adui kichwa kinauma kwakweli
 
Sijawahi kujua nilimkosea nini rafiki yangu kipenzi Don

Utoto tulicheza wote , o_level alinibeba nikaitwa kichwa.

Siri yangu ilikuwa yake , advance ilianza kututenganisha kidogo mwisho chuo ikawa tunameet baadhi ya weekend .

Mwisho mawasiliano yakawa hafifu daily mimi ndiye wa kumtafuta .

Oya Don mimi mwanao bado naishi na sonona juu yako sijui ni kipi nilikukosea kama kipo nisamehe tena na tena .

Daily nikipiga nikikuuliza what's up mpaka umekuwa hivyo unasema hakuna lolote ila sio yule ninayemjua.

Sio kila rafiki akiondoka basi ni kheri wapo ambao ni ngumu kukubali aondoke maishani mwako ila unakuta yeye ndiye anajitenga unakubali huku ukiwa unaumia sana .

Ikiwa humo humu tell me what's up my Nigga.
 
Don njoo unaitwaa hapaaa,
 
Back
Top Bottom