Acha kujidanganya pesa sio kila kitu

Pesa inasaidia sana lakini haikusaidii kutatua changamoto zote. Kama pesa ingekuwa Kila kitu basi huyo mwanamfalme asingepata ajali yaani pesa zingemuepusha na ajali.

Cc Demi
 
Mtoe hapo kwenye hizo mashine uone kama neema ya Mungu itamuacha hai.

Acha kula ili neema ya Mungu isikuue kwa njaa.

Mnaongea pumba wakati hao wachungaji wenu na masheikh wanaowalisha matangopori wanatembelea V8 na kulala chini ya ulinzi mkali KK Security na mbwa. Neema ya Mungu ni kwa sisi walalahoi.
 
kawiyo ukiwa lofa hizo changamoto hazikupati?
 
Nimekosana na wazazi leo hii hii kisa Pesa

Amenambia maneno magumu mpk nahitaji kumuona mwanasaikolojia private nilipie huduma niende nikaeleze yanayo nisibu Kwa kulia ili moyo wangu usije ukabadilika huku mbele.

Pesa imenionesha kuwa pamoja na uanaume wako unaweza kuaibika vibaya sana Endapo utaitafuta usiikose.

Mkuu ngoja niishie hapa ila nasema PATA PESA KWANZA NDIYO USEME HAYO

Kwa Sasa tunza maneno.
 
Kwa nini pesa hazikumuepusha na ajali?
So controversial brother/sister, haya ni maswali ya kati ya kuku na yai kilianza nini! Hutapata jibu la moja kwa moja. Lakini ukiwa na pesa umesolve zaidi ya 90% ya changamoto za maisha then inabaki 10% ambayo ni kama hizi halafu umesema mwenyewe ni ajali! Kuna ajali inazuilika? Unaweza pata ajali ukiwa umelala kitandani, lakini ajali zinawapata zaidi wasio na pesa kuliko wenye fweza!
 
Wanamtesa tu Yote ya nin hayo anaweza kuamka na akafarik mda huo huo
Hawamtesi sababu hajitambui. Technically huyo mtu anaishi kwa raha kuliko 80% ya Watanzania.

Sababu hana feelings kuumizwa kihisia, hateseki kutafuta kodi wala chakula, haamki asubuhi kudandia daladala na kurudi usiku kutembelea nyumbani kwake kwenye mafuriko, hawazi ada na stress za mapenzi.

Unaweza kuta tunamhurumia humu ilhali yeye ndio angeweza angetuhurumia sisi
 
Karma
 
Watu maskini tunapenda sana kujustify umaskini wetu kwa kuonyesha mali sio kitu wakati mioyoni kwetu tunamwaga machozi tupate uwezo hata kijipasenti kadhaa
 
Watu maskini tunapenda sana kujustify umaskini wetu kwa kuonyesha mali sio kitu wakati mioyoni kwetu tunamwaga machozi tupate uwezo hata kijipasenti kadhaa
Pesa ina thamani hakuna anayekataa Shida ni Nyie maskini mnadhani kwmaba mkipata pesa matatizo yote yataisha. Hizo ndio hisia za kimaskini.

Matajiri tunajua Pesa inatatua njaa tu😀😀😀
 
Umeongea vizuri sana.
Pesa ni muhimu sana kuwa nazo lakini haziwezi kuepusha na baadhi ya changamoto hivyo tusipende kusema pesa ni Kila kitu bali tuseme pesa zinasaidia sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…