Acha kujidhulumu kumbuka tunaishi mara moja, Ishi kikamilifu

Acha kujidhulumu kumbuka tunaishi mara moja, Ishi kikamilifu

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Ninaumia sana kila ninapokumbuka kuwa "nikitolewa kila kitu nilichojifunza na kufundishwa ninayebakia ni Mimi" kauli hii inanifanya nijione kama nimejidhulumu sana katika maisha yangu. Ulishawahi na wewe kujiuliza swali kama hili? Kama ndivyo basi huenda na wewe ukahisi jambo fulani umekuwa ukijikosea.

Kati ya zawadi muhimu tulizojaliwa ni zawadi ya kuishi na kati ya mitihani migumu tunayokutana nayo ni kuishi kikamilifu. Tunaishi maisha ambayo sisi wenyewe hatumo ndani yake. Uhuru wetu wa uwepo umekandamizwa na itikadi, imani, elimu, misimamo, falsafa n.k mambo ambayo kwa kiasi kikubwa siyo sisi ila tumeaminishwa hivyo.

Siyo jambo la ajabu kumkuta mtu Mzee wa umri lakini bado hajaishi kwa sababu ipo tofauti kati ya kuishi na kuwepo. Wanadamu wengi tupo ila hatujaweza kuishi kabisa kutokana na mipaka mingi tuliyowekeana inayotufanya kuwepo bila kuishi.

Tunaishi kama watu wenye makovu miwili mzima, tukihofia kutoneshwa na kuwatonesha wengine. Tumejawa na hofu na tunawaogopesha wengine. Tunaogopana, tunachukiana, tunachukia mafanikio ya wengine, tunapenda kunufaika kupitia maumivu ya wengi. Na hata tunaposhirikiana na wengine tunaonesha unafiki tu ila ndani yetu kunafukuta maumivu.

Mtu akifanikiwa mafanikio yoyote yale tunaona kama tumenyang'anywa ya kwetu, tunachukia. Tunaishi kwa ukizani mkubwa kati ya utu wetu wa ndani na kile tunachokionesha nje yetu " tunaigiza kuishi". Tukiumia ndani tunajioazimisha kuonesha nje kuwa hatujaumia, tukifurahi ndani tunaonesha nje kuwa tumeumia. Kwa kifupi hatuoneshi tafsiri halisi ya hali zetu.

Maisha yamejawa na uchovu usiosemekana, Ukweli unaoitwa uongo na uongo unaitwa ukweli kwa makusudi. Maisha kwa asili yake yameumbwa kuelekea ukweli jambo ambalo ni kitanzi cha maumivu kwetu. Tunajua lakini tufanye nini?.. Inaumiza sawa lakini ndiyo hivyo tena....

Tumefika hatua ya kusema mambo ndivyo yalivyo hakuna namna. Hatua hii si tu hatua ya kukata tamaa ila ni hatua ya kuacha kuishi na kuingiza igizo kuu la kidunia " Kivuli kinaishi"
 
Ninaumia sana kila ninapokumbuka kuwa "nikitolewa kila kitu nilichojifunza na kufundishwa ninayebakia ni Mimi" kauli hii inanifanya nijione kama nimejidhulumu sana katika maisha yangu. Ulishawahi na wewe kujiuliza swali kama hili? Kama ndivyo basi huenda na wewe ukahisi jambo fulani umekuwa ukijikosea.

Kati ya zawadi muhimu tulizojaliwa ni zawadi ya kuishi na kati ya mitihani migumu tunayokutana nayo ni kuishi kikamilifu. Tunaishi maisha ambayo sisi wenyewe hatumo ndani yake. Uhuru wetu wa uwepo umekandamizwa na itikadi, imani, elimu, misimamo, falsafa n.k mambo ambayo kwa kiasi kikubwa siyo sisi ila tumeaminishwa hivyo.

Siyo jambo la ajabu kamkuta mtu Mzee wa umri lakini bado hajaishi kwa sababu ipo tofauti kati ya kuishi na kuwepo. Wanadamu wengi tupo ila hatujaweza kuishi kabisa kutokana na mipaka Mungu tuliyowekeana.

Tunaishi kama watu wenye makovu miwili mzima, tukihofia kutoneshwa na kuwatonesha wengine. Tumejawa na hofu na tunawaogopesha wengine. Tunaogopana, tunachukiana, tunachukia mafanikio ya wengine, tunapenda kunufaika kupitia maumivu ya wengi. Na hata tunaposhirikiana na wengine tunaonesha unafiki tu ila ndani yetu kunafukuta maumivu.

Mtu akifanikiwa mafanikio yoyote yale tunaona kama tumenyang'anywa ya kwetu, tunachukia. Tunaishi kwa ukizani mkubwa kati ya utu wetu wa ndani na kile tunachokionesha nje yetu " tunaigiza kuishi". Tukiumia ndani tunajioazimisha kuonesha nje kuwa hatujaumia, tukifurahi ndani tunaonesha nje kuwa tumeumia. Kwa kifupi hatuoneshi tafsiri halisi ya hali zetu.

Maisha yamejawa na uchovu usiosemekana, Ukweli unaoitwa uongo na uongo unaitwa ukweli kwa makusudi. Maisha kwa asili yake apyameumbwa kuelekea ukweli jambo ambalo ni kitanzi cha maumivu kwetu. Tunajua lakini tufanye nini?..

Tumefika hatua ya kusema mambo ndivyo yalivyo hakuna namna. Hatua hii si tu hatua ya kukata tamaa ila ni hatua ya kuacha kuishi na kuingiza igizo kuu la kidunia " Kivuli kinaishi"
Umeandika jambo lenye tafakari kubwa. Nami napitia kipindi kigumu kinachonifanya nijitafakari sana. Kama kuna mwenye uwezo wa kunisaidia hata TSh 5,000 kwa ajili ya chakula leo, nitashukuru sana. Mungu awabariki wote wenye moyo wa kusaidia.
 
Wengine wamejikuta katika mazingira siyo sahihi wao kuishi kutokana na watu waliowazunguka. Ogopa sana mtu mwenye wivu ule mbaya wa mafanikio yako. Wivu ule anatamani urudi nyuma ili muwe sawa au chini yake.
Hiyo ni hatua ya juu kabisa ya mtu kuacha maisha yake na kuamini wengine ndiyo wanaoishi ni kwa hasara yake, ni hatua ya ukichaa na mawanda ya chini ya upendo na ni daraja muhimu la tabia za uchawi mweusi.

Ukimuona mtu anaishi kwa mtindo huo jambo la kwanza ni kumuonea huruma sana kwa sababu tayari ameshaipoteza nafasi yake ya kuishi yeye kama yeye kikamilifu, anapitia maumivu makali sana ndani yake inagawa hasemi tu.

Hali ya ndani ya mtu asiyeishi kikamilifu ni sawa kabisa na kuishi ndani ya moto, watu wanaungua ndani hawasemi tu ila kwa hakika hali inasikitisha sana. Ndani ya mtu mwenye wivu ni moto usiozima, moto unaowashwa na ukweli unaotaka kujifunua, matamanio yasiyofikiwa, udhaifu unaojidhihirisha, uwezekano unaoonekana pengine, msukuomo wa kuacha kujiliwaza "escaping comfort zone".

Hitaji la marekebesho ya ndani yetu "inner engineering" ni la muhimu sana katika zama hizi ambazo kwa hakika ukichaa mwanadamu kutaka uhuru wake wa asili dhidi ya mipaka mbalimbali ya kidini, kielimu, kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k umeshika hatamu.

Asante, naweza nikaihisi huruma yako juu ya mateso tunayopitia
 
Tamaduni inapaswa kulishwa na asili, tunaishi katika zama ambazo asili ndiyo inayolishwa na utamaduni.
 
Back
Top Bottom