Uchaguzi 2020 Acha kulalamika, nawe kachukue fomu

Uchaguzi 2020 Acha kulalamika, nawe kachukue fomu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Salaam,

Za masiku wandugu...

Nimeona humu kuna watu wanalalamika na kulialia kuhusu baadhi ya watu wanaoenda kuchukua fomu za kugombea ubunge hususan kwenye Chama Cha Mapinduzi.

Watu wanalalamika sijui Babu Tale kachukua fomu, Nabii gani naye sijui kachukua, mara Gwajima naye kachukua, n.k.

Sasa ni hivi, kila Mtanzania aliye na sifa, ana haki ya kugombea.

Wewe uliyeko humu JF acha kulialia ukiona wenzio wanajitosa kuchukua fomu ili wagombee.

Kama unaona hao wanaochukua fomu hawafai, uamuzi wa kuwa wanafaa au hawafai, utafanywa na wananchi kwenye sanduku la kura.

Nawe, badala ya kushinda JF kutwa kucha huku ukinung’unika, kachukue fomu ugombee huo uteuzi, kama unajiona una uwezo zaidi kushinda hao watangaza nia.

Zaidi, waweza pia himiza watu wengine uwaonao kuwa wanafaa, kwenda kuchukua hizo fomu ili waweze kugombea.

Muda wa kutenda ndo huu, kama kweli vilio vyenu ni vya dhati.

Kinyume na hapo, itakuwa ni kelele za mtandaoni tu.

Acha kulialia JF. Tinga ofisi za chama ukipendacho katika jimbo lako, uchukue fomu.
 
Too low Mtani….hukuwa na haja ya kunianzishia uzi. Nina wasiwasi hujaelewa nilichoandika, umekurupuka tu.
Wacha pressure, hata mimi nilipinga, napinga, na nitapinga siku zote Gwajima na watu wengine wanaojiita wa Mungu kuonesha dalili za kuitamani siasa, wale tayari wana jukumu la kuwachunga kondoo zao, hawawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, hata maandiko matakatifu hayataki jambo hilo.
 
Wacha pressure, hata mimi nilipinga, napinga, na nitapinga siku zote Gwajima na watu wengine wanaojiita wa Mungu kuonesha dalili za kuitamani siasa, wale tayari wana jukumu la kuwachunga kondoo zao, hawawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, hata maandiko matakatifu hayataki hilo jambo.
Kwan siasa nayo ni bwana?
 
Inawezekana watu wanalalamikia hao kua awafai kwakua nao awafai!
 
Wacha pressure, hata mimi nilipinga, napinga, na nitapinga siku zote Gwajima na watu wengine wanaojiita wa Mungu kuonesha dalili za kuitamani siasa, wale tayari wana jukumu la kuwachunga kondoo zao, hawawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, hata maandiko matakatifu hayataki jambo hilo.
Mchungaji Migwa as point of view.
 
Back
Top Bottom