ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Ndugu zangu,
Nawapa salam...
Hivi karibuni kwa masikitiko jamii ilipokea taarifa ya kifo cha daktari wa Moyo, Dr. Masau ambeye alianzisha huduma hadimu ya upasuaji wa moyo nchini.
Taarifa hii ya kifo ilichochea mjadala ambao ulifanyik kwa kirefu zaidi mwaka 2008 hapahapa JF.
Kwa bahati mbaya, mijadala hiyo imeelekezwa zaidi kwenye kulalamika na kukatishana tamaa badala ya kufunguana macho na kuonyeshana njia.
Lengo la thread hii, ni kuonyesha fursa iliyopo katika uwekezaji kwenye sekta ya afya.
Kiujumla, kila kunapokuwa na uhaba wa kitu basi hiyo ni fursa kwa mwekezaji au mfanyabiashara.
Huduma za afya nchini zinapatikana kwa uhaba wa hali ya juu au kwa ufasaha zaidi huduma BORA za afya zinapatikana kwa uhaba wa hali juu. Kwahiyo, utoaji wa huduma BORA ya afya ni fursa ya kibiashara.
katika hadithi ya Dr. Masau tumeona kuwa dr. alikuwa na matatizo makubwa mawili ambayo ni 1. Kupata jengo la kutolea huduma na 2. kupata wagonjwa wenye uwezo wa kulipia huduma.
Matatizo haya mawili yote ni fursa kwa wawekezaji "wenye macho". Tuanze kuliangalia tatizo la jengo.
Sasa hivi kila kona ya jiji majengo yanaota kama uyoga. Majengo haya mara nyingi chini huwekwa "frame" za biashara na juu hupangishwa. mengi ya majengo haya yanamilikiwa na watu binafsi wenye uhuru wa kuamua jinsi ya kuyatumia. Wakati habari za Dr. Masau ziliposikika, mtu anayemiliki jengo binafsi angeweza kuingia ubia nae ili wafanye biashara ambayo ingewanufaisha kifedha na pia kuinufaisha jamii kiujumla.
Kwa bahati mbaya, hatjaona jitihada ya wawekezaji walioamua kutaka kuingia ubia na Dr. Masau. Hizi guest house/hoteli nyingi zimejazana Sinza na mitaa mingine watu "wanafanya matusi" tu zingeweza kutumika kwa manufaa zaidi iwapo zingegeuzwa hospitali. Kwa bahati mbaya jamii imekaa ikilalamika tu bila kuchuku hatua stahiki!
Jambo hili sio kuhusu Dr. Masau tu. Mpaka sasa wapo madaktari wengi sehemu mbalimbali nchini ambao wanafikiria kuanzisha utoaji huduma BORA za afya lakin wanakwamishwa aidha na mtaji au miundombinu kama majengo na vifaa. wawekezaji wetu badala ya kununua dalaldala tu anzeni kuwekeza kwenye huduma BORA za afya.
Katika hili, si sahihi kuitupia tu lawama jamii. Madaktrai nao wanatakiwa kutangaza utayari wao wa kuingia ubia na wenye nia ya kuwekeza kwenye huduma BORA za afya. Kwahiyo hapa tukiombe chama cha madaktari Tanzania-MAT kibuni utaratibu wa jinsi wawekezaji hao watakavyopata taarifa ya fursa zilizopo za kushirikiana na madaktari katika uwekezaji kwenye sekta hii muhimu.
Uchaguzi ni wetu kama tutakuwa tunalalamika tu au tutaanza kuwekeza kwenye huduma hii muhimu. Kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa kwenye sekta ya elimu. Uwekezaji umetanuka sana kwenye sekta ya elimu, lakini katika afya bado TUMELALA. Tusiwaachie madaktari peke yao, tushirikiane nao kuinua uwekezaji kwenye sekta ya afya.
Labda hapa nitoe mfano mmoja halisi: Mara ya mwisho nilipotembelea duka la ANUDHA linalouza vifaa vya huduma za afya nilikuta mashine nzuri ya ultrasound inaweza kupatikana kwa USD 28,000 hii ni sawa na shilingi milioni 45. Shilingi milioni 45 ni pesa ya kununua coaster moja (dala dala) iliyokuwa kwenye hali nzuri. Sasa tufananishe mapato ya huduma ya ultrasound na dalala. Mtu mmoja analipa sh. elfu 20 kufanyiwa ultrasound. Ukitoa huduma kwa watu 20 tu kwa siku ni kipato cha sh. laki nne. ukimlipa daktari (mtaalam wa ultrasound) shilingi laki moja kwa siku unabaki na shilingi laki tatu. Iwapo gharama za uendeshaji ni arouns sh. elfu 30 kwa siku unabaki na sh. 270,000. je, kuna daladala inayoweza kukuingizia sh. 270,000 kwa siku? Kumbuka kuwa ultrasound unahitaji kachumba kadogo tu na sehemu ya wagonjwa kusubiri. Wapo madaktari (wataalam) wengi wenye ujuzi wa kufanya ultrasound lakini hawana uwezo wa kununua mashine ya sh. milioni 45. badala ya kununua daladala kwanini usikae chini na mtaalam huyu mkakubaliana aina fulani ya ubia? Wataalam wanakaa bure kwenye hospitali za serikali ambazo mashine hizo zimeharibika au hazipo! WATUMIENI kijasiriamali...
Kuhusu tatizo la pili ambalo ni kupata wagonjwa wenye uwezo wa kulipia huduma.
Watanzania wanaotibiwa nje ya nchi sio wale wanaopelekwa na serikali tu. Kadri siku zinavyosonga ndovyo idadi ya watanzania wanaoweza kumudu gharama za huduma BORA ya afya inavyoongezeka. Kinachotakiwa ni kuwafikishia watu hawa taarifa kuwa huduma inapatikana na kuwahakikishia kuwa kiwango chake ni kilekile wanachokifuata Afrika Kusini, Kenya, India, Uingereza, Ujerumani au kwingineko.
Hii inamaanisha kwamba katika sakata la Dr. Masau kulikuwa na opportunity ya mtu kuoofer huduma ya marketing ya huduma za Dr. Masau. Hii ni fursa ya uwekezaji ambayo badala ya kulalamika ingeweza kutumika kuokoa mradi wa THI na kutoa chanzo cha mapato kwa mwekezaji.
Tukumbushane tu kwamba marketing ya huduma ya afya inafanyika kwa kufuata utaratibu tofauti na marketing ya huduma kama za biashara nyingine. hata hivyo mada hii iko nje ya malengo ya chapisho hili.
Hitimisho: Jumuiya ya Madaktari Tanzania - MAT ni chombo muhimu chenye uwezo wa kuunganisha wataalam wa kutoa huduma za afya (madaktari) na wawekezaji.
Jumuiya hii ibuni na kutangaza utaratibu wa ubia kati ya wataalam na wawekezaji, kwa sababu wawekezaji watakuwa na imani zaidi wakiunganishwa na jumuiya inayotambulika kuliko kumfuata daktari mmoja mmoja.
Tutumie muda mwingi zaidi kufikiria utatuzi wa changamoto tunazokumbana nazo kuliko muda tunaoutumia kulalamika.
R.I.P Dr. Masau...