Acha kulalamika, wekeza kwenye afya...

Acha kulalamika, wekeza kwenye afya...

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,040
Reaction score
7,303
Ndugu zangu,

Nawapa salam...

Hivi karibuni kwa masikitiko jamii ilipokea taarifa ya kifo cha daktari wa Moyo, Dr. Masau ambeye alianzisha huduma hadimu ya upasuaji wa moyo nchini.

Taarifa hii ya kifo ilichochea mjadala ambao ulifanyik kwa kirefu zaidi mwaka 2008 hapahapa JF.

Kwa bahati mbaya, mijadala hiyo imeelekezwa zaidi kwenye kulalamika na kukatishana tamaa badala ya kufunguana macho na kuonyeshana njia.

Lengo la thread hii, ni kuonyesha fursa iliyopo katika uwekezaji kwenye sekta ya afya.

Kiujumla, kila kunapokuwa na uhaba wa kitu basi hiyo ni fursa kwa mwekezaji au mfanyabiashara.

Huduma za afya nchini zinapatikana kwa uhaba wa hali ya juu au kwa ufasaha zaidi huduma BORA za afya zinapatikana kwa uhaba wa hali juu. Kwahiyo, utoaji wa huduma BORA ya afya ni fursa ya kibiashara.

katika hadithi ya Dr. Masau tumeona kuwa dr. alikuwa na matatizo makubwa mawili ambayo ni 1. Kupata jengo la kutolea huduma na 2. kupata wagonjwa wenye uwezo wa kulipia huduma.

Matatizo haya mawili yote ni fursa kwa wawekezaji "wenye macho". Tuanze kuliangalia tatizo la jengo.

Sasa hivi kila kona ya jiji majengo yanaota kama uyoga. Majengo haya mara nyingi chini huwekwa "frame" za biashara na juu hupangishwa. mengi ya majengo haya yanamilikiwa na watu binafsi wenye uhuru wa kuamua jinsi ya kuyatumia. Wakati habari za Dr. Masau ziliposikika, mtu anayemiliki jengo binafsi angeweza kuingia ubia nae ili wafanye biashara ambayo ingewanufaisha kifedha na pia kuinufaisha jamii kiujumla.

Kwa bahati mbaya, hatjaona jitihada ya wawekezaji walioamua kutaka kuingia ubia na Dr. Masau. Hizi guest house/hoteli nyingi zimejazana Sinza na mitaa mingine watu "wanafanya matusi" tu zingeweza kutumika kwa manufaa zaidi iwapo zingegeuzwa hospitali. Kwa bahati mbaya jamii imekaa ikilalamika tu bila kuchuku hatua stahiki!

Jambo hili sio kuhusu Dr. Masau tu. Mpaka sasa wapo madaktari wengi sehemu mbalimbali nchini ambao wanafikiria kuanzisha utoaji huduma BORA za afya lakin wanakwamishwa aidha na mtaji au miundombinu kama majengo na vifaa. wawekezaji wetu badala ya kununua dalaldala tu anzeni kuwekeza kwenye huduma BORA za afya.

Katika hili, si sahihi kuitupia tu lawama jamii. Madaktrai nao wanatakiwa kutangaza utayari wao wa kuingia ubia na wenye nia ya kuwekeza kwenye huduma BORA za afya. Kwahiyo hapa tukiombe chama cha madaktari Tanzania-MAT kibuni utaratibu wa jinsi wawekezaji hao watakavyopata taarifa ya fursa zilizopo za kushirikiana na madaktari katika uwekezaji kwenye sekta hii muhimu.

Uchaguzi ni wetu kama tutakuwa tunalalamika tu au tutaanza kuwekeza kwenye huduma hii muhimu. Kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa kwenye sekta ya elimu. Uwekezaji umetanuka sana kwenye sekta ya elimu, lakini katika afya bado TUMELALA. Tusiwaachie madaktari peke yao, tushirikiane nao kuinua uwekezaji kwenye sekta ya afya.

Labda hapa nitoe mfano mmoja halisi: Mara ya mwisho nilipotembelea duka la ANUDHA linalouza vifaa vya huduma za afya nilikuta mashine nzuri ya ultrasound inaweza kupatikana kwa USD 28,000 hii ni sawa na shilingi milioni 45. Shilingi milioni 45 ni pesa ya kununua coaster moja (dala dala) iliyokuwa kwenye hali nzuri. Sasa tufananishe mapato ya huduma ya ultrasound na dalala. Mtu mmoja analipa sh. elfu 20 kufanyiwa ultrasound. Ukitoa huduma kwa watu 20 tu kwa siku ni kipato cha sh. laki nne. ukimlipa daktari (mtaalam wa ultrasound) shilingi laki moja kwa siku unabaki na shilingi laki tatu. Iwapo gharama za uendeshaji ni arouns sh. elfu 30 kwa siku unabaki na sh. 270,000. je, kuna daladala inayoweza kukuingizia sh. 270,000 kwa siku? Kumbuka kuwa ultrasound unahitaji kachumba kadogo tu na sehemu ya wagonjwa kusubiri. Wapo madaktari (wataalam) wengi wenye ujuzi wa kufanya ultrasound lakini hawana uwezo wa kununua mashine ya sh. milioni 45. badala ya kununua daladala kwanini usikae chini na mtaalam huyu mkakubaliana aina fulani ya ubia? Wataalam wanakaa bure kwenye hospitali za serikali ambazo mashine hizo zimeharibika au hazipo! WATUMIENI kijasiriamali...

Kuhusu tatizo la pili ambalo ni kupata wagonjwa wenye uwezo wa kulipia huduma.

Watanzania wanaotibiwa nje ya nchi sio wale wanaopelekwa na serikali tu. Kadri siku zinavyosonga ndovyo idadi ya watanzania wanaoweza kumudu gharama za huduma BORA ya afya inavyoongezeka. Kinachotakiwa ni kuwafikishia watu hawa taarifa kuwa huduma inapatikana na kuwahakikishia kuwa kiwango chake ni kilekile wanachokifuata Afrika Kusini, Kenya, India, Uingereza, Ujerumani au kwingineko.

Hii inamaanisha kwamba katika sakata la Dr. Masau kulikuwa na opportunity ya mtu kuoofer huduma ya marketing ya huduma za Dr. Masau. Hii ni fursa ya uwekezaji ambayo badala ya kulalamika ingeweza kutumika kuokoa mradi wa THI na kutoa chanzo cha mapato kwa mwekezaji.

Tukumbushane tu kwamba marketing ya huduma ya afya inafanyika kwa kufuata utaratibu tofauti na marketing ya huduma kama za biashara nyingine. hata hivyo mada hii iko nje ya malengo ya chapisho hili.

Hitimisho: Jumuiya ya Madaktari Tanzania - MAT ni chombo muhimu chenye uwezo wa kuunganisha wataalam wa kutoa huduma za afya (madaktari) na wawekezaji.

Jumuiya hii ibuni na kutangaza utaratibu wa ubia kati ya wataalam na wawekezaji, kwa sababu wawekezaji watakuwa na imani zaidi wakiunganishwa na jumuiya inayotambulika kuliko kumfuata daktari mmoja mmoja.

Tutumie muda mwingi zaidi kufikiria utatuzi wa changamoto tunazokumbana nazo kuliko muda tunaoutumia kulalamika.

R.I.P Dr. Masau...
 
Ni wazo zuri sana bwana Zemarcopolo nategemea mazingira ya kwetu si rahisi sana kufungua heart surgery ikiwa ata serikali yenyewe imeshindwa kuweka vifaa vya kisasa na madawa kwenye hospitali zake!! Labda madaktari malipo yao yangekuwa mazuri kama wanasiasa,tujifunze kutoka india ambapo mawaziri na wanasiasa wao wanatumia vitz kama nyenzo ya usafiri lakini wamewekeza kwa kiasi kikubwa sana katika afya,Heart surgery kwa UK ni pound 30,000/ na 60,000/ Usd kwa USA lakini ni 13,000/usd kwa India(Apollo Hospital)mwaka uliopita 2012 kulikuwa na wagonjwa toka nje 500,000 waliokwenda India kupata matibabu mbalimbali.Mwezi wa pili mwaka huu meneja wangu alitaka huduma ya fibroid tumor USA ilikuwa $30,000/lakini India ilikuwa $9000 tu pamoja na cost zote za hosp..hapa kazini wahindi wakiugua ni lazima wapande ndege waende pata matibabu kwao ni cheap na mazuri,sina uhakika kwa Tz
 
Bima ya afya inaweza kukata mzizi wa fitina...
 
Mheshimiwa, ZeMarcopolo; unaongea mambo ya msingi sana. Kwanza nikushukuru kwa kuwa na mtazamo mpana na chanya. Kuna options nyingi nyingi sana zinawezekana kwenye hii sector ya afya.
Kwa mfano nina concept ya weekend health camp - (do not google, this is my idea...). Madaktari wanaweza kuwasiliana nami nikawapa idea ambayoitawawezesha kupata mshiko mrefu bila kuwa na pressure na kwa kutekeleza kazi zao nyingine kwa uadilifu bila ya massive investments.
 
Sawasawa mdau. Tafadhali wasiliana na uongozi wa MAT kupitia email hii doctorsmat@gmail.com

Si mbaya pia kama utashare mawazo yako kwenye jukwaa hili ili kupanuana mawazo kama ilivyo tamaduni ya JF.

Tuendelee kuwa pamoja...
 
mkuu ZeMarcopolo kwa uzoefu wangu, ni wachache wanaofanikiwa wakiwekeza kwenye afya pasipo wao kuwa madaktari. Hii nayo ni changamoto kubwa (ila sijui kwa nini) na kwa kiasi kikubwa imewafanya wasio madaktari wasifikirie kuwekeza huko
 
Kwakweli sina kumbukumbu za watu waliowekeza kwenye afya tukiacha huduma za pharmacy. Katika chapisho hili nimeeleza kuwa jumuiya ya madaktari MAT ichukue nafasi kwenye coordination. Biashara ya huduma za kitaalam inahitaji utaalam, mtaji na akili za biashara. MAT inaweza kuwa kama daraja kati ya utaalam wa madaktari na mtaji na akili za biashara za wawekezaji.

Kila mshiriki kwenye hili hapaswi kujiona muhimu zaidi ya mwenzake.

Additionally hii pia ni fursa ya uwekezaji kwa MAT kwa sababu katika kufanya coordination wahusika watataikiwa kutozwa service and maintenance charges. MAT inaweza kuingia mkataba na mwanasheria ambaye atakuwa maalum kwa ajili ya mikataba ya ubia.

Na hii sio kwa madaktari na non madaktari bali hata baina ya madaktari. Mara nyingi madaktari bingwa kila mmoja anaanzisha kituo chake cha huduma. Kwa kiasi kikubwa wangeboresha huduma zao iwapo wangetengeneza networks za kupeana ushirikiano na wangeweza kuwa na maabara moja inayokidhi viwango vya ISO.

Hivi vitu ni lazima kuwe kuna body inayocordinate ambapo MAT ina nafasi nzuri zaidi ya kuplay that role...
 
Mwaka jana siku kama ya leo nilikutana na Mwarabu mmoja Chennai alinieleza mambo mengi na namna Wtz wengi wanavyoenda India kutibiwa India .Alinidokeza kuhusu kuanzisha medical tourism hapa nchini ,alinidokeza kuwa gharama za matibabu India ni chini sana .Alishangaa Wtz wengi kupendelea Appolo ilhali kuna hospitali nyingine bora na zenye wataalamu na gharama zao ni chini kuliko Appolo alitolea mfano Hosp ya MADRAS UNIVERSITY pale Chennai na Gorverment hosp ya jimbo hilo! Tuliongea mengi ila kilichonitokea pale hosp kilifuta mazungumzo hayo kwani nilipoteza contact zake!
unachosema ni kweli tunahitaji kuwekeza katika afya ,si umeona Appolo wameona Wtz ni deal sasa wanaleta hospitali yao hapa DAR!
 
Ni kweli kuwa watanzani asio kama hawana uwezo. Wapo watu wengi wenye uwezo na wanakosa huduma. Huduma ikishakuwepo nchini hata yule asiyekuwa na uwezo au taarifa ya jinsi ya kuifuata nje ataweza kuipata.

Apollo hospitali yao wanataka kufngua wapi?
 
zemarcopolo chukua tano, umeongea point, kupanuka kwa bima za afya kunafungua uwekezaji katika afya maana watu wengi wanaweza kuafford quality medical services. tatizo ni mitaji na financing options kama lease financing etc. DSM inahitaji hospitali na diagnostic centers nyingi. kuna mjerumani mmoja aliniuliza TZ kuna CT scan ngapi? nkamwambia less than 10, akaniambia jiji la Hamburg pekee zipo 80
 
Ni kweli mkuu.

Kama wingi wa daladala za Dar es Salaam unaendana na idadi ya watu, hakuna sababu kwanini CT scan ziwe chache. Wawekezaji wakipewa taarifa zaidi jinsi ya kuwekeza kwenye afya tutafanikiwa. Mtu kama Bakhresa ukika naye chini ukamuonyesha hesabu zinazoonyesha net profit uaweza kumconvince kuwekeza kwenye afya. ANaweza kufungua diagnostic center ya kisasa kwa viwango ambavyo tunavifuata India.
 
Ni kweli kuwa watanzani asio kama hawana uwezo. Wapo watu wengi wenye uwezo na wanakosa huduma. Huduma ikishakuwepo nchini hata yule asiyekuwa na uwezo au taarifa ya jinsi ya kuifuata nje ataweza kuipata.

Apollo hospitali yao wanataka kufngua wapi?
wanafungua jengo la Mwalimu Nyerere Pensioners Tower Block B ilipo Wizara ya kazi ,tayari ukarabati unafanyika na nasikia hapo ni kwa muda tu watajenga sehemu nyingine
 
wanafungua jengo la Mwalimu Nyerere Pensioners Tower Block B ilipo Wizara ya kazi ,tayari ukarabati unafanyika na nasikia hapo ni kwa muda tu watajenga sehemu nyingine

asante kwa taarifa.

Uwepo wao pia ni opportunity ya biashara kwa watanzania. Tuzitumie...
 
Back
Top Bottom