Acha kusumbua watu wakuchangie kwenye harusi yako

Ila hili la kufanya mambo kupita uwezo ni shida,anajikuta mtu anaingia kwenye madeni kwa shughuli ya siku moja,halafu unalipa madeni kwa miezi kadhaa mbele,kuna haja ya jamii kubadilika
Kobasi mko vizuri katika harusi na misiba kuliko Wagalatia. Harusi chai, maandazi, ubwabwa, na soda tu shughuli imeisha, mtu anaweza kupanga na kufanya ndoa/harusi kwa wiki moja au siku tatu tu😁, Wagalatia harusi inaandaliwa mwaka mzima.
 
Waswahili hawawezi kuelewa hili jambo, Kuna ujinga fulani wa kijamii na kitamaduni ni wa kudumu kwa Waafrika.
Kuna ambao hawawezi kukuelewa kweli, lakini haka kautamaduni kamekuwa kero kwa kweli. Ni utamaduni unaozidi kushamiri Tanzania, lakini si kwa Waafrika wote, maana najua jamii nyingi tu za kiafrika ambazo hazina utamaduni huu. Mtu anaanda bajeti ya harusi milioni 25 lakini yeye mfukoni ana mil 3. Zingine anategemea michango, tena ya kushinikiza watu....full stress
 
Waswahili hawawezi kuelewa hili jambo, Kuna ujinga fulani wa kijamii na kitamaduni ni wa kudumu kwa Waafrika.
Taratibu tutaachana na huo ujinga tu. Mimi nilishapiga marufuku suala la kuniunga kwenye makundi ya michango ya harusi. Nikiungwa naleft immediately, na namfata inbox alieniunga kumwambia sihitaji kuwepo kwenye hilo kundi.

Rambirambi nitatoa lakini michango ya harusi hiyo hapana, labda nipewe taarifa halafu niamue kuchangia kutokana na ukaribu wangu na muoaji/muolewaji. Nimeoa bila kusumbua mtu anichangie hata shilingi 1, vivyo hivyo na mimi sitaki yoyote anisumbue
 
Zaman nilikuwa nachanga ila ilikuwa too much unaweza ukawa na magroup ya whatsapp karibia 5 yote yanahitaji michango, nakumbuka nilipoteza simu mpaka Kuja kununua nyingine harusi zote zikawa zimepita na magroup yamefungwa, nikasema Yes hii ndo dawa
Mtu sasa hivi akiniadd kwenye group la Michango huwa silifungui mpaka harusi ipite.
siwezi kuwachangia watu wazima kisa Wanahalalisha kwenda Kutomberner
 
Wengne tulipokuja mjini ndo tukaona watu wanachangiwa sijui send off mara arusi

kule ukuryani kwetu unajitegemea kuanzia mahari hadi gharama ya harusi
hata zawadi zitokanazo na sherehe huwa ni ziada, tunachojali ni kuwa watu wale washibe
Huko ndio pazuri
 
Usiwadai watu mchango ila wakija pitisha kapu la sadaka kama kanisani
 
Ni njia moja wapo ya utafutaji wa mitaji michango yenu maharusi inawanufaisha sana.
Mfano single 30 double 50000
Single wakitoa watu 30= 900K
Double wayoe lbd 20=1000K
Bado mizawadi kedekede
Oyah kufunga ndoa ni source of income
 
Baadhi ya wabongo walivyo na akili mbovu, watakataa kuja wakisema "hajatuchangisha, anajifanya anazo"
 
Ndoa Lazima TuchANGIE , SABABU"-
1. Kutoa ni moyo usambe si utajiri.

2. Kila aliyesimama alishikwa mkono.

3. Kushiriki kwenye shida na Raha.

4. Kuunga Mkono na Kusaidia Gharama (Financial Support): Harusi ni shughuli yenye gharama kubwa (ukumbi, chakula, vinywaji, mavazi, n.k.), hivyo michango husaidia kupunguza mzigo wa kifedha kwa wanandoa.

5. Kujenga na Kudumisha Umoja/Udugu (Solidarity): Kuchangia ni ishara ya upendo, urafiki, na utamaduni wa kusaidiana katika jamii (Utanzania), ikionyesha umoja wa ndugu na marafiki.

6. Kuanzisha Maisha Mapya (Startup Capital): Michango mara nyingi huwapa wanandoa kianzio cha maisha (zawadi ya harusi) ili kuwasaidia kununua vifaa vya nyumbani au kuanza familia yao wakiwa na utulivu wa kifedha.

7. Reciprocity (Kushirikiana kwa Zamu): Ni utamaduni wa "kutoa ili utolewe". Watu huchangia wakijua kuwa siku zao za harusi wakihitaji msaada, na wao watachangiwa.

8. Kuheshimu na Kutambua Ndoa (Formalizing Union): Michango na vikao vya harusi ni njia rasmi ya kutambua na kuhalalisha muungano wa familia mbili, ikimpa heshima bwana na bibi harusi.

9. Kushiriki Furaha (Shared Joy): Kuchangia kunamfanya mchangiaji kujihisi sehemu ya tukio muhimu la maisha ya rafiki au ndugu yake

MUHIMU: Wenye hiria ya familia zisizo na bahati ya ndoa, wenye wivu na familia maskini, wenye husda, walio kata tamaa kuoa na kuolewa, waliozalishwa wakaachwa ndio wanaopinga michango.
 
Ndio maana mimi harusi huwa sichangii. Labda iwe ya mtu wa karibu
 
Kuna mambo ya kushikana mikono mfano misiba, ugonjwa n.k. Sherehe ya harusi ni anasa tu wala haina umuhimu wowote...ndio maana unatakiwa kufanya kwa kadri ya uwezo wako bila kusumbua watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…