Acha kutafuta pesa kwa kuwatumikisha watoto

Hapa naongea katika Roho
Kuna watu wanakusanya watoto wa maskini kutoka kijijini na kuwatumikisha kwa kuuza vitu vidogo vidogo kama mayai ya kuchemshwa, kandoro au miwa.

Mtu anakuwa na vijana 5 au zaidi anawaweka kwenye chumba kimoja anawafanya watumwa wake huku watoto wake mwenyewe akiwasomesha kwa jasho la watoto wadogo hawa anaowafuga.

Kwakuwa watoto wametoka kijijini kwenye familia maskini wanaona sawa tu , mwisho wa mwezi anawapa elfu 50, 60, 70 au 80.

Unajilaani wewe na kizazi chako, unakipalia moto kizazi chako. Acha. Mungu mtetezi wa yatima na maskini yu hai , kama sio wewe basi watoto wako au wajukuu zako watalipwa kwa uchungu.

Huwezi kuwasaidia waache huko kijijini waishi kwa amani na furaha. Sio unawadaa kuwa kuna kazi Dar then wanafika huku unawatwika mayai.

Acha
Comrade, huu ndiyo Ubepari sasa! Kwenye hii dunia ya sasa hakikisha unapambana vilivyo. Ukiendekeza haya mawazo yako ya Ujamaa, utaufa masikini.

Kama hiki ulichokiongea kingekuwa na mashiko, basi watu wenye ngozi nyeupe mpaka muda huu wangekuwa wamelaaniwa!

Kwenye hii dunia ya Ubepari, usipowatumikisha wengine; utatumikishwa wewe. Na hizo laana zitabakia tu kuwa kama zile za dua la kuku.
 
Comrade, huu ndiyo Ubepari sasa! Kwenye hii dunia ya sasa hakikisha unapambana vilivyo. Ukiendekeza haya mawazo yako ya Ujamaa, utaufa masikini.

Kama hiki ulichokiongea kingekuwa na mashiko, basi watu wenye ngozi nyeupe mpaka muda huu wangekuwa wamelaaniwa! Maana hawa ndiyo wanyonyaji namba moja duniani!! Badala yake unajionea mwenyewe! Wanazidi tu kusomba raslimali zetu kwa kushirikiana na viongozi wetu wabinafsi; na hivyo mwisho wa siku kutuacha katika hali ya umasikini.
Bora nisipate pesa kuliko kuwa na pesa za kutumikisha vitoto vya watu
 
Hapa naongea katika Roho
Kuna watu wanakusanya watoto wa maskini kutoka kijijini na kuwatumikisha kwa kuuza vitu vidogo vidogo kama mayai ya kuchemshwa, kandoro au miwa.

Mtu anakuwa na vijana 5 au zaidi anawaweka kwenye chumba kimoja anawafanya watumwa wake huku watoto wake mwenyewe akiwasomesha kwa jasho la watoto wadogo hawa anaowafuga.

Kwakuwa watoto wametoka kijijini kwenye familia maskini wanaona sawa tu , mwisho wa mwezi anawapa elfu 50, 60, 70 au 80.

Unajilaani wewe na kizazi chako, unakipalia moto kizazi chako. Acha. Mungu mtetezi wa yatima na maskini yu hai , kama sio wewe basi watoto wako au wajukuu zako watalipwa kwa uchungu.

Huwezi kuwasaidia waache huko kijijini waishi kwa amani na furaha. Sio unawadaa kuwa kuna kazi Dar then wanafika huku unawatwika mayai.

Acha
kumbe wanalipwa 50,mpaka 80 mkuu, hao unaowaita watoto hizo kazi wanazitafuta wenyewe hakuna anayeenda kuwateka na kuwafanyia hivyo, na wao wako kazini na hizo 70 au 80 wanatumaga kwao zinawasaidia
 
Bora nisipate pesa kuliko kuwa na pesa za kutumikisha vitoto vya watu
Comrade, ukitaka uyafaidi maisha ya hapa duniani! Au ukitaka kuheshimiwa na kila mtu, kiasi cha kufikia hatu ya kuitwa Mtukufu, Mheshimiwa, Boss, nk. Miliki tu moja ya hivi vitu viwili hapa;
1. Pesa (Money)
2. Madaraka (Power)

Kinyume na hapo, hata watoto wako wa kuwazaa! Achilia mbali mke wako! Watakudharau.
 
Hapa naongea katika Roho
Kuna watu wanakusanya watoto wa maskini kutoka kijijini na kuwatumikisha kwa kuuza vitu vidogo vidogo kama mayai ya kuchemshwa, kandoro au miwa.

Mtu anakuwa na vijana 5 au zaidi anawaweka kwenye chumba kimoja anawafanya watumwa wake huku watoto wake mwenyewe akiwasomesha kwa jasho la watoto wadogo hawa anaowafuga.

Kwakuwa watoto wametoka kijijini kwenye familia maskini wanaona sawa tu , mwisho wa mwezi anawapa elfu 50, 60, 70 au 80.

Unajilaani wewe na kizazi chako, unakipalia moto kizazi chako. Acha. Mungu mtetezi wa yatima na maskini yu hai , kama sio wewe basi watoto wako au wajukuu zako watalipwa kwa uchungu.

Huwezi kuwasaidia waache huko kijijini waishi kwa amani na furaha. Sio unawadaa kuwa kuna kazi Dar then wanafika huku unawatwika mayai.

Acha
Kijakazi yeyote ni mtumwa kwa bwana wake aliyempa ujira.. asiye fanya kazi na asile.

Sasa vijana wachague wachague kati ya kubaki kua masikini vijijini na kuja mjini kutumikishwa na mabepari kwa lengo la kujipatia kipato kidogo kipi bora
 
Hapa naongea katika Roho
Kuna watu wanakusanya watoto wa maskini kutoka kijijini na kuwatumikisha kwa kuuza vitu vidogo vidogo kama mayai ya kuchemshwa, kandoro au miwa.

Mtu anakuwa na vijana 5 au zaidi anawaweka kwenye chumba kimoja anawafanya watumwa wake huku watoto wake mwenyewe akiwasomesha kwa jasho la watoto wadogo hawa anaowafuga.

Kwakuwa watoto wametoka kijijini kwenye familia maskini wanaona sawa tu , mwisho wa mwezi anawapa elfu 50, 60, 70 au 80.

Unajilaani wewe na kizazi chako, unakipalia moto kizazi chako. Acha. Mungu mtetezi wa yatima na maskini yu hai , kama sio wewe basi watoto wako au wajukuu zako watalipwa kwa uchungu.

Huwezi kuwasaidia waache huko kijijini waishi kwa amani na furaha. Sio unawadaa kuwa kuna kazi Dar then wanafika huku unawatwika mayai.

Acha
Ni ugumu tu wa maisha watoto wanaopitia kijijini huko ila Mungu awalinde tu.
 
Mimi mtazamo wangu hapo ni tofauti,si watu wote wanaenda shule,suala ni je huyo anayekufanyia kazi zako naye ananufaika? kama una msichana wa kazi akipata mchumba unamsaidia ili naye awe na kwake?
Je,anapoumwa unamsaidia kumtiibia au unamtaka atumie mshahara wake huo mdogo kujitibia n.k
Nakubaliana na wewe kuwatendea mema uliowaajiri, tujiulize wanaofanya kazi kwenye taasisi kubwa zenye majina
mfano kwa mo na baresa wanalipwa sawasawa na jasho lao wanalotoa? tusiangalie hawa wauza miwa wanaopewa chakula na malazi.
Halafu mbona serikali iko kimya tu?
 
Hata ninyi wazazi/walezi mnaowatumia watoto wenu wadogo kwenye biashara zenu muache, wapeni uhuru watoto wa kucheza na watoto wenzao.
Unamkuta dogo wa miaka 7 au 8 anauza karanga za mama/baba, hiyo sio sawa.

Mwache walau hata afike 14yrs aisee.
 
Hakuna laaana wala nini,, kwangu wamepita wengi na wanaendelea kuletana wanafundishana kazi na wanatoboa.... Wengine ni mafundi wakubwa manispaa niliyopo kiufupi wana umoja wao wanajiita watoto wa mama wawili. Sasa endelea na fikra zako za kilaana laana.
 
Back
Top Bottom