Acha kutafuta pesa kwa kuwatumikisha watoto

Comrade, huu ndiyo Ubepari sasa! Kwenye hii dunia ya sasa hakikisha unapambana vilivyo. Ukiendekeza haya mawazo yako ya Ujamaa, utaufa masikini.

Kama hiki ulichokiongea kingekuwa na mashiko, basi watu wenye ngozi nyeupe mpaka muda huu wangekuwa wamelaaniwa!

Kwenye hii dunia ya Ubepari, usipowatumikisha wengine; utatumikishwa wewe. Na hizo laana zitabakia tu kuwa kama zile za dua la kuku.
 
Bora nisipate pesa kuliko kuwa na pesa za kutumikisha vitoto vya watu
 
kumbe wanalipwa 50,mpaka 80 mkuu, hao unaowaita watoto hizo kazi wanazitafuta wenyewe hakuna anayeenda kuwateka na kuwafanyia hivyo, na wao wako kazini na hizo 70 au 80 wanatumaga kwao zinawasaidia
 
Bora nisipate pesa kuliko kuwa na pesa za kutumikisha vitoto vya watu
Comrade, ukitaka uyafaidi maisha ya hapa duniani! Au ukitaka kuheshimiwa na kila mtu, kiasi cha kufikia hatu ya kuitwa Mtukufu, Mheshimiwa, Boss, nk. Miliki tu moja ya hivi vitu viwili hapa;
1. Pesa (Money)
2. Madaraka (Power)

Kinyume na hapo, hata watoto wako wa kuwazaa! Achilia mbali mke wako! Watakudharau.
 
Kijakazi yeyote ni mtumwa kwa bwana wake aliyempa ujira.. asiye fanya kazi na asile.

Sasa vijana wachague wachague kati ya kubaki kua masikini vijijini na kuja mjini kutumikishwa na mabepari kwa lengo la kujipatia kipato kidogo kipi bora
 
Ni ugumu tu wa maisha watoto wanaopitia kijijini huko ila Mungu awalinde tu.
 
Halafu mbona serikali iko kimya tu?
 
Hata ninyi wazazi/walezi mnaowatumia watoto wenu wadogo kwenye biashara zenu muache, wapeni uhuru watoto wa kucheza na watoto wenzao.
Unamkuta dogo wa miaka 7 au 8 anauza karanga za mama/baba, hiyo sio sawa.

Mwache walau hata afike 14yrs aisee.
 
Hakuna laaana wala nini,, kwangu wamepita wengi na wanaendelea kuletana wanafundishana kazi na wanatoboa.... Wengine ni mafundi wakubwa manispaa niliyopo kiufupi wana umoja wao wanajiita watoto wa mama wawili. Sasa endelea na fikra zako za kilaana laana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…