Acha ujinga kujifanya unalinda BRAND(JINA)

Acha ujinga kujifanya unalinda BRAND(JINA)

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
HIVI UNALINDA WADHIFA(BRAND,STATUS) AU UNALINDA UMASIKINI??? Etiiiii Etiiiii!!!!!!

Wengi wetu tunaishia kwenye kununua vitu ambavyo vitaendelea kutoa fedha mifukon mwetu badala ya kununua vitu ambavyo vitaingiza fedha mifukon mwetu. Nafikiri hili linaweza likawa JANGA la NNE la Taifa mana Ndio kikwazo cha wengi kuwa vilevile kwa zaidi ya Miaka lukuki, kila siku wanajipa moyo hadharani huku miyoni mwao kunaungua moto kwa kutosogea mbele kimapato.....

Tunapenda sifa kuliko hali zetu za maisha, TUNAPENDA watu watuone nje tuko vizuri kwa kipato kumbe ndani ya moyo ni MAJANGA......Masifa sifa tu ya kuvaa manguo ya bei kubwa, kunua mavitu ya thamani yasio na maana yeyote.....ETI unajiambia unalinda WADHIFA(BRAND) yako, Brand gani? Hiyo inayokufanya ufe maskini etiii?....

Mwengine anapendezesha nyumba kwa kununu Tv ya milioni 3 na kujipa moyo eti hata nikila dagaa ila kwangu papendeze! sasa unajiuliza hii tv italeta pesa mfukoni kweli?.. eeeti eeetii.

Nilishangaa pale nilipomuona Rafiki yangu mwaka mmoja baada ya kuanza kazi akachukua mkopo na kukunua gari la milion 10 na huku akiwa hana hata chanzo chengine za kuingiza pesa ya mafuta, huku gari iyo ikatumika kama gari ya kupigia misele badala ya kuifanya tax bubu, huku akiwa anapata mshahara nusu kutokana na mkopo kutoka kwenye lak 5.7 had 2.8, nilipomuuliza akaniambia

"Nataka nifanane na Uafisa" Daaah!!! Kuna raha gani ya kuwa ofisa machoni mwa watu kumbe moyoni mwake anajiona Kapuku tu kwasababu anaishi kiziki kuliko kawaida.

Nashangaa nilipomuona dada mmoja miez mitatu baada ya kuanza kazi za ndani mshahara wake wote wa miezi mitatu akaenda nunua smart fon, nilipomuuliza akaniambia "Namimi nataka nimuone Wema na Diamond" Shiiiiit!!!! Daaah!

Dada huyu angenunua mashine ya kupikia Tambi za Dengu na malighafi ya unga na vyombo vya kupikia, angekuwa ametumia pesa yake vyema na kuanza kuwekeza ili baada ya muda aje kununua simu kubwa zaidi ya ile kwababu pesa yake itakuwa imejizalisha katika biashara ya Tambi.

Siku moja niliulizwa kwanini vijana hawapendi kuwekeza kwenye biashara ndogondogo ambazo mitaji yake ni midogo ambayo wanaweza kuipata kwa urahisi, jibu likawa nikawajibu 'UBISHOO.' Akaniuliza kwa kustuka

"Ubishoo??", nikamjibu ndio ubishoo kwababu kila mmoja anataka kuonekana yupo online, yupo instagram ukoo anataka aonekane amepost picha ametinga tishert kali na raba kali akiwa yupo mlimani city, city mall, Pugu Mall, Quality Center.

Jiulize mtu huyu ataweza shika mavi ya kuku kweli? ataweza kuingia kwenye tope la vitunguu au mpunga? Serious bishoo uyu hawezi kazi za kushikashika uchafu, hizi ni kazi zetu sisi washamba wa mjini.

Dada zangu wengine kila wanapenda kulinda wadhifa wasiokuwa nao!!! Sasa wigi la laki 2 lanini wakati jana umetoka kuomba pesa kwa baba ya nauli. It shame, Nguvu na akili zinaenda kwenye wigi badala ya kwenda kwenye kamzunguko wa pesa ili ilete pesa.

WENGI wetu tunaogopa kuambiana ukweli na wakati uwo uwo tunataka kusifiana tu oooh umependeza na ilo wigi mara oooh umenoga na ilo gauni hata kama tunapotea, Daaah!. Sasa TV ya Milion 3 ya nini wakati ipo ya milioni 1 au ndo unalinda WADHIFA(BRAND)?,

La nini gari linalokula mafuta mengi wakati linalokula mafuta machache lipo au ndo unalinda Brand?, Yanini Simu ya Milioni 1 Wakati ya laki 5 ipo au ndo unalinda BRAND????.....ENDELEA Kulinda Brand wenzio wanalinda vitunguu na Viazi vyao uko kilombero na mihogo yao huko kisarawe na nyanya zao ilula na mahindi yao dabaga.......

ACHANA NA BRAND BRAND Izo wewe, wekeza pesa ili pesa iwe Brand inayojilinda yenyewe.....Sifa bila pesa ni sawa na Rimoti bila TV........

SORRY Kama nimekugusa ila ELEWA Hakuna DAWA Tamu.
 
Kuna mzee mmoja aliajiliwa kampuni fulani ya migodini na akawa anafanya mambo kama mtoto mdogo ya kihuni na kupoteza pesa nyingi sana.kibarua kilipoisha aliishiwa mpka akauza nyumba maana alitaka kuendelea kulinda BRAND mjini.familia ikaenda zake kwao shinyanga.huyo mzee kwa sasa anaishi kwa kufugwa kwa mtu tu jamaa yake mjini,na anadandia kupiga dei waka kama taxi driver mjini ilihali awali alikua na uwezo wa kua na taxi car zake za kutosha tu lakini akaishia kulinda BRAND,ajabu kabisa majuzi akapata trip fulani ya wazungu wakazunguka nae kama siku tatu na wakamlipa dollar kadhaa kama zawadi na alipochenji kwa pesa yetu akawa na laki mbili unusu nje na pesa ya gari maana yenyewe ni ya mwenye gari.lakini hiyo laki mbili na nusu badala hata aikimbize kwenye familia kule Shinyanga lakini ameenda kununua smart phone ya laki moja na themanini.kiukweli natamani nimchagulie tusi aisee.na jana amekuja muda wa jioni wa kutoka town kwenda majumbani akiniomba lifti eti hana hata shing mia 4 za kupanda town bus.sidanganyi nilimnyima lift,nasema nilimnyima kwa makusudi na si kwa roho mbaya bali kwa kumfundisha ajutie ujinga alioufanya.so mtoa mada uko sawa sana,tungeweza kuiga maisha kama ya wahindi tungeendelea sana

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Asante sana mleta mada, nilikutana na kaka mmoja amesoma business administration lakini hajapata ajira, mke wake alikuwa mwajiriwa. Yule kaka alinunua bread maker ilikuwa inakanda unga wa maandazi alikuwa anasupply maandazi ameyafunika na cling film ukiona utapenda. Mwisho order iliongezeka akawa anatoa kilo tano kwa siku
 
Hayo ndio mambo ya Asset na liability,Watu Wengi wana liability wakidhani kuwa wana Asset.Ngoja niwaambieni ,Kitu chochote ambacho hakikuingizii pesa hicho kitu ni liability,Asset ni kitu chochote kinachokuingizia pesa.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Aaaaaaah siwez acha kapendez it's my hobby nyie tafuten Pesa ntaomba kazi kwenu

Wa kishua
 
Back
Top Bottom