Mjomba kwenye miaka ya 70 alipata safari ya masomo nchini Urusi,kipindi hicho alikuwa na miaka 25 hivi,.akiwa kule alikuwa kila jpili anakwenda kwenye makanisa kuabudu mungu wake lkn alikuwa anajikuta kijana yupo peke yake kanisa zima,warusi wakawa wanamshangaa sio kwa sababu ya rangi yake bali kwa umri wake wakawa wanamuuliza kama anatatizo lolote,.ujue ni nadra sana kumkuta kijana makanisani kwenye miaka ile sijui kwa sasa,yeye alikuwa anawajibu kuwa hana tatizo lolote,.
Siku moja wazee wa kanisa ikawabidi wamuwekee kikao ili wamuhoji,akaitwa jmosi moja usharikani na kumuhoji sana baada ya kuridhika kuwa hana tatizo bali ni utamaduni ambao huku kwetu ndo tumeuzoea,.wazee wale wakamuambia kuwa,.kawaida wao kule huenda kanisani kutubu kwa madhambi waliyoyafanya kipindi cha ujana wakati wanatafuta,.
Wakamuambia kuwa kijana katika kutafuta unaweza kukutana na mambo mengi sana ya hatari ambayo wengine wanadiriki kuua bila kukusudia ilimradi kupata,kupokea rushwa,kuiba,kudhurumu kwa mtindo wa viji NGO'S,.wakamuambia tafuta hela kwanza kwa staili yoyote ile then njoo utubu kwa kutoa sadaka uzeeni,.