Achana na kamati za harusi kodisha Events management company

Achana na kamati za harusi kodisha Events management company

Labda kama hufanyi hiyo shughuli kibongobongo, unapanga harusi with grand ceremony kwakutegemea mifuko ya watu aka Michango.

Hivyo basi ndugu hawataona aibu kutoa pleadge zao, na kuzikamilisha. kuwalazimisha kuja kwenye vikao ni njia Moja wapi ya kuwatisha na kuwafanya waone aibu Hata kama hawataki kuchanga, ila wakifikiri na wao yatawakuta inakuwa hakuna jinsi tena.

Ila kama ni familia Bora au zote zinazokula keki ya Taifa ni wazi jema kabisa. Kwa sherehe na misiba acha Hela ifanye kazi.
 
It works kama tu muoaji au familia yake wapo well-off. Hawatategemea hela ya mtu kufanikisha sherehe.

Otherwise vikao na kamati ni sehemu ya uwezeshaji mochango, haikwepeki.
 
Hizo event management Co zinaweza kufanya vizuri kwenye misiba, huwa tunatoa tu bila kuvutwa mashati.
 
Labda uwe full mkoko mfukoni na usitegemee mifuko ya watu. Ishakuwa taabu kufanya sherehe kwa kutegemea mifuko ya watu. Unaoa jibebe mwenyewe, turudi nyuma hapo watu walikuwa wanajitegemea kufanya harusi kwa gharama zao wenyewe
 
Punguza stress na kutafutana maneno na ndugu. Ukitaka kuoa kodisha kampuni ya event management wakuandalie sherehe
Mkuu akili zako zinakutosha mwenyewe tu- usijaribu kutugawia ujinga- Event Manager haji na hela ila kamati inatafuta hela na kuzila yenyewe huku ukishuhudia zinateketea
 
Changamoto, muoaji/muolewaji anategemea kufanikisha lengo lake kwa michango ya watu, inawezekana yeye kianzio ana laki 5 tu. Je atawezaje kukodisha?​
 
Mkuu akili zako zinakutosha mwenyewe tu- usijaribu kutugawia ujinga- Event Manager haji na hela ila kamati inatafuta hela na kuzila yenyewe huku ukishuhudia zinateketea
Akili za kimaskini hizo
 
Back
Top Bottom