Achana na kusave pesa bank

mkuu upo sahihi katika hilo maana banki inazipunguza ila kwenye hisa zinaongezeka pia kunafaida likuki ukilinganisha na bank
 
Hivi vikundi ni vizuri

Vinanishinda sehemu moja tu, kuhudhuria kila wiki na usipofanya hivyo eti unapigwa penati
 
Kabisaa mkuu, mtu ana dunduliza 50,000 kila mwezi kwa kusave bank, ukitaka kujua ni balaa weka 50,000 iache miezi sita bila kuongezea, utakuta inepungua,
Kwa serving account haipungui, ila inaongezeka kiduchu sana
 
Hivi vikundi ni vizuri

Vinanishinda sehemu moja tu, kuhudhuria kila wiki na usipofanya hivyo eti unapigwa penati
Lakin ile faini badae ndo inaongeza faida za kikundi sasa
 
Hivi vikundi ni vizuri

Vinanishinda sehemu moja tu, kuhudhuria kila wiki na usipofanya hivyo eti unapigwa penati
Duuu hiyo ya kila wiki too much... mara moja kwa mwezi inatosha sana. Faini muhimu kwa wachelewaji na wasiohudhuria. Unapotaka kufanikiwa lazima uwe na nidhamu. Hizi penati zinaongeza pia mapato ya mfuko. Kuna penati ya kuchelewa kikaoni, kutofika na kuchelewa kutuma fedha.
 
Ubarikiwe sana, nataman vijana wengi wangetambua hii opportunity, kabla mm sijaanza kutumia Vikoba na Succoss pesa ndogo ndogo inje ya mshahara sikuona kama ni mhimu kusave, lakini sasa hivi najua kila week au mwwzi lazima niwe na hisa, lakin pia Succoss mtu unaweza kopa hadi m10, bila hata ya mashariti magumu magumu kivile.
Kwa wanaume kama hata ww hujaona kikundi mulize hata mkeo maana wengi wamo, tumia kikundi cha wife uwe unanunua hisa, trust me zile elf 30,50,70, tunazotumia weekend kama hii utaziona faida yake. Fikiria kila week unaweka hata 15,000 ni tofali 15 hizo.
 
yan tatizo ribaaaaaaaaa yan hata ukaniambia chukua 1ml urejeshe na riba ya 500 ushanikosa.......napambana kivyangu....kuna mtu kasepa na laki 9 za wanakikundi yeye ndio mweka hazina.......mwingine kasepa na 300000 hawa wa kibati (mchezo)......huko saccos sijui ila naonaga tu wakibambuana vitanda na vyombo.....mwingine anauza deki anadaiwa marejesho......huyu nae anacheza mchezo huku hana kazi so anategemea ela ya matumizi sijui ndio anaibana kibajet.....do it for ur own risk.......kuna walinufaika navyo mf bodaboda wengi hapa kitaa walikuwa na pikipiki za mkataba/kipande now wamenunua zao.......do it but anything can happen
 
Mkuu kila kitu kina risk nyuma yake, kwa mfano kwa walio makazin, kuna maofisi mengine wana succoss ambazo mwanachama anakatwa direct toka kwa salary, hizi nzuri sana maana pia unaweza ongeza akiba utakavyo. Kwa vikoba ni mhimu sana kuangalia wanachama wengi source zao nn, inasaidia sana kuchoose the right one.
 
Mkuu, kwani kuna shida gani let's say mimi nanunua hisa kama kawa na contribution nyingine natoa lakini siwezi kuhudhuria vikao

Hiyo inakuwa inamaanisha kuwa nipo tayari kufanyia kazi maamuzi watakayotoa wenzangu waliohudhuria kwenye vikao
 
Vikoba, vibrifkesi pamoja na saccos vyote vinaweza kuwa na faida endapo kila mtu ana chanzo cha kueleweka cha mapato. Aidha una biashara inayokuingizia kipato flani kila siku ama una kazi ambayo unaeza chukua sehemu ya mshahara wako ukawa unazungushia huko vikobani!
Kinyume na hapo mtatiana hasara tu maana kuna wataoweka wengine washindwe kupeleka hela kwa wakati!
 
Vicoba na saccos ni big no kwa imani yngu mambo ya riba tena...ntapambana kumpata mbia mwenza ktk shuguli zangu zoote zakiuchumi ikijengwa na uaminifu zaid huku tukifanya kazi kwa malikauli ikiambatana na mikataba madhubuti kuepusha janja janja
 
Mkuu, kwani kuna shida gani let's say mimi nanunua hisa kama kawa na contribution nyingine natoa lakini siwezi kuhudhuria vikao

Hiyo inakuwa inamaanisha kuwa nipo tayari kufanyia kazi maamuzi watakayotoa wenzangu waliohudhuria kwenye vikao
Hizi mambo huwa zipo beyond financial matters. Kuna kusaidiana member anapopata tatizo au anapokua na jambo la kheri.
Sasa wewe ukitoa tu michango na kushiriki remotely siku ukiwa na suala lako haitakua na uzito wenzio kushirikiana na wewe.
Lakini pia huwa kuna masuala ya kikundi hua yanahitaji ideas na majadiliano ya members wote. Mfano inaweza ifike sehemu muamue interest mnayopata kwenye kikundi mnunue mamshamba, viwanja au hata mfanye mradi. Inapendeza wote mtoe maoni otherwise wewe utakua unaendelea kwa kufaidi tu mawazo ya wengine wakati hushiriki.
Hawa wanaohudhuria na kushiriki si kwamba hawana majukumu mengine na wao wasihudhurie but hiyo ndo discipline na commitment inayotakiwa ili kikundi kisiyumbe.
 
Hahaha upo sahihi sana.. Lazima wewe utakuwa mwanakikundi mzoefu
 
Unajuwa nimewahi hapa ndani ili nijue kuhusu hisa, wapi papo pouwa kununua hizo hisa, analysis makini ulizozifanya na kwa kuwa unazaidi ya miaka 2 ushakuwa mzoefu unaweza kutunyambulia faida kamili ya hisa (may be minimum ni % ngapi ya nilichokiweka kitakuwa faida)

Ukifanya hivyo itakuwa pouwa sana Mkuu,
 
Nakuja mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…