Achana na Senzo, Barbara huyu dada ana connection balaa

Tunapata Tabu Sana Bila Connection
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Kwa sasa hivi, hakuna ''sababu za kibiashara'' kwa Simba (au hata Yanga) kuwa na Uwanja wake wa mechi (mfano mkubwa kama wa Mkapa).
Kwa sasa ni sahihi timu hizi kuwa na viwanja vyake vya mazoezi tu.

Niko tayari kwa mjadala mpana ili kulitetea hili.
Timu kama wydad na raja casablanca hawana uwanja, AC milan na Inter milan wanatumia uwanja wa jiji. Same as Bayern munich na liverkusen. Simba kwa sasa haihitaji uwekezaji wa aina hiyo.
 
Wabongo bwana mtu ukiomba kupiga picha na mtu fulani basi mnafahamiana. Halafu kuna connection zingine hazina manufaa kwa timu bali kwa mtu binafsi. Mfano rais wa CAF au FIFA hawezi kuwa na urafiki/ ushirika zaidi na kiongozi wa timu fulani pekee.
Connection yenye manufaa ni za makampuni mbali mbali za kibiashara.
 
Wakati Simba ikifanya mambo kimataifa Utopolo wao wnavurugana makundi yafuatayo:
Viongozi Vs benchi la ufundi.
Mashabiki Vs Marefa.
Yanga gsm Vs Yanga asili.
Wachezaji Wazawa vs Wachezaji Wageni
 
Noma kweli
 
Timu kama wydad na raja casablanca hawana uwanja, AC milan na Inter milan wanatumia uwanja wa jiji. Same as Bayern munich na liverkusen. Simba kwa sasa haihitaji uwekezaji wa aina hiyo.
Ndio mnajifananisha na hao wenzenu wamewekeza Sana sehemu nyingi tofauti na nyie mmewekeza kwenye mapaka
 
Afu ni hii caf champion itakuwaje
Tatizo CAF huwa wanaiga kila kitu toka UEFA, hii CAF Champions League ndio inaenda kupoteza mvuto kabisa, na hizo timu 20 zitakazo shiriki hayo mashindano zitatakiwa kulipia ada ya ushiriki.
 
Kumbe vyura baada ya kufeli kila Mjadala wanaolishwa ujinga sasa wamehamia kwenye Mjadala waliolishwa ujinga eti Simba ina Wachezaji wageni!

Hawa Kenge wamewahi kujiuliza Real Madrid iliyochukua UCL mara 3 mfululizo ilikuwa na Wazawa/Waspain wangapi?

Bale - Benzema - Ronaldo

Kroose - Casemiro - Modric

Marcelo - Ramos - Varane - Cav

Navas​

Kikosi kizima hapo cha Real kina Wazawa wawili tu (Ramos na Cav)
Wakati Simba Kuna Manula, Tshabalala, Kapombe, Mzamiru, Bocco, Dilunga na Nyoni ambao wanacheza mara kwa mara.

Hawa Utopolo haki ya Mungu bora Paka wangu ana akili kuliko wao manake panya hakatizi nyumbani kwangu.
 
Mpango uliopo CAF sasa ni kutengeneza ligi ya timu 20 bora Afrika na Simba itakuwa miongoni mwa timu hizo.
Ili uwe mshiriki wa hiyo ligi inabidi ulipe bilioni 40,hiyo pesa mkiani ipo,maana b 20 tu ya uwekezaji inapigwa dana dana
 
Mwenye cv ya barbara aiweke hapa ili tuilinganishe na ya senzo tumalize mjadala
 

Attachments

  • Screenshot_20210313-111903_Chrome.jpg
    121.1 KB · Views: 1
Halafu nikuibie siri. 'Wanawake wote warembo wako Simba sc'. (Jitafakari)
😂😂
... uko sahihi 101%. Utafiti usio rasmi kuanzia mitaani, kwenye mabaa, kumbi za starehe, hadi viwanjani umeonesha Simba SC ndiyo klabu yenye mashabiki wengi zaidi wa kike nchini na katika hao wengi ni warembo.

Haikuweza kujulikana mara moja kama rangi za Simba zina mvuto zaidi kwa wanawake kuliko za klabu nyingine au la au kama kuna sababu nyingine kuhusiana na trend hiyo ya ajabu! Utafiti wa kina unahijika ili kupata sababu ya wanawake na watoto wadogo wa kike kuipenda sana Simba SC.
 
Senzo mpigaji tu, anakula hela za GSM. Hakuna anachoweza kuwashauri Yanga zaidi ya kuwadanganya atahonga Wachezaji wa Simba wafungishe.

Yaan Senzo, Hersi na Nugaz wapo kwenye chama moja la wapigaji wa hela za GSM kwa mgongo wa Yanga.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Senzo mpigaji tu, anakula hela za GSM. Hakuna anachoweza kuwashauri Yanga zaidi ya kuwadanganya atahonga Wachezaji wa Simba wafungishe.

Yaan Senzo, Hersi na Nugaz wapo kwenye chama moja la wapigaji wa hela za GSM kwa mgongo wa Yanga.
Akili za mswahili
 

Ili tuendelee na mjadala huu ni lazima tuwe kwenye ukurasa mmoja.

1. Unaamini kuwa bi Barbra alienda tu kupiga picha na akina Etoo, Infantino na Motsepe, na kwamba watu hao hawamjui Barbra na hawatamkumbuka kwa lolote ?

2. Unaamini kwamba Barbra alienda kushiriki mkutano huo kwa niaba ya klabu anayoiongoza, ili kujenga ''connection'' na CAF, FIFA na wadau wengine wa soka katika ulingo wa kimataifa. Ila connection hizo hazina msaada wowote kwa klabu yake (Simba Sports Club) ?

Ni lipi unalisimamia kati ya hayo mawili hapo juu mkuu ?

Nikifahamu hilo, nitakua katika mazingira mazuri ya ama kujadiliana, kukufundisha au kufundishwa nawewe.

Karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…