Acheni kuchimba mashimo na kuyaacha wazi kwa muda mrefu.

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖Mhadhara (76)✍️
Katika pita pita zangu kwenye mikoa ya Mbeya na Songwe nimefanikiwa kugundua kero inayohatarisha maisha ya watu hasa watoto wadogo.

Wenyeji wa mikoa tajwa mnapenda sana kuchimba mashimo marefu (kwa matumizi ya visima, vyoo, maji taka, n.k) na kuyaacha wazi kwa muda mrefu, wengine hawafuniki vizuri mashimo. Mvua zikinyesha hayo mashimo mnayoyaacha wazi yanajaa maji hali inayohatarisha maisha ya watoto.

USHAURI 1: Viongozi wa ngazi ya mtaa na kata kwenye mikutano yenu na wananchi ni vizuri kutoa elimu kwa wananchi wenu kuhusu tabia ya watu wanaochimba mashimo na kuyaacha wazi kwa muda mrefu au kutoyafunika vizuri.

USHAURI 2: Ukichimba shimo kwa ajili ya matumizi ya choo, kisima, maji taka, n.k hakikisha unafunika haraka ili kuepusha madhara kwa watoto kuliko kuacha wazi shimo kwa kipindi kirefu au kutofunika vizuri hali itayohatarisha uhai wa watoto na hata watu wazima.

RIGHT MARKER,
DAR ES SALAAM.
 

Attachments

  • 1736069073011.jpg
    198.8 KB · Views: 4
Watu wanachimba mashimo na viongozi wa mtaa wapo tu wanaangalia
 
Licha ya madhara ya kimwili kuna madhara ya kiroho pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…