Acheni kutembea na wake za watu

chongoe

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2019
Posts
1,183
Reaction score
2,871
Habari zenu wakuu niende kwenye mada moja kwa moja siku mbili zilizopita ikiwa nipo bandarini mida ya saa tatu usiku baada ya kupakia mizigo kwenye ikiwa nasubiria maji ya usiku ili nisafiri kabla ya kuondoka nikaona niende nikachakate kidogo mbusu maana nahodha kila bandali hakosi jiko.

Nikawaacha vijana wangu baharia pale Pwani mi nikapandisha juu wakati natembea nikakutana na watu watatu mmoja akiwa amebe kiroba ila kikubwa kabla hawajanipita nikawasalimia jamaa aliitikia mmoja tu mara ghafla nikasikia sauti kutoka kwenye kiroba kaka nisaidie wanaenda kunitosa hawa baharini jamaa kwa mstuko wakatupa lile roba wakaziokota mbio mimi nikaliendea lile roba kulifungua nakutana na jamaa yuko hoi bin taaban namuuliza kulikoni akaniambia kuwa amefumaniwa na mke wa mtu kwaiyo wamempiga na ilikuwa akatoswe baharin acheni wake za watu.
 
Baharia Chongoe za siku mwamba?

Haya masahibu hayo ni huko Mafia ama?
 
Duuuh mafuta ya Kassa tena?!! 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…