Acheni ujinga, kejeli humu, JF hawakukosea kuweka Jukwaa la Love Connect

Teh teh wasamehe bure..watu tumepata wachumba hum sas hivi tunasomesha
 
Sio wachumba tuu, unakuta mtu anaomba ushaur wa jambo ambalo linaweza likamkuta mtu yyt, lkn mijitu inayoandka post ikiwa chooni inaanza kejeli, inakera kinoma, mfn asubuh hii hii kuna mshkaji tu kaomba aelekezwe shule flan iv ipo huko bukoba amapangiwa huko, kuuliza tu hali ya mambo ilivyo kule ili labda ajipange kabla hajaenda mijitu ikaanza kutengeneza perception zao na kuanza kumshambulia, Ifke mda humu namo tukague vyeti
 
Ooooh this is nice.Mtu anaponda wanaosaka wachumba lakini aksante akiamka anaweka bundle kwa jili ya hili jukwaa.Sasa ajabu na kweli Majukwaa yapo mia kidogo hajafungua la mapishi akajifunze kalmati na vitumbua anabakii 'nakushauri ndugu yangu usitafute wachumba humu utaliwa hela..Ebo wa mtaani aombi hela..Hakuna uchumba uliovunjikwa wa watu waliosoma pamoja?waliokulia mtaa mmoja??yaani Elimu ni Ukombozi wa fikra!
 
Watu wanashindwa kuelewa dunia imekuwa ndogo sana kwa technology iliyopo sasa. Social media inatajirisha watu social media ni ajira kwa wengi kwa nini social media isiwe njia ya kuunganisha watu wakafahamiana wakapendana wakaoana. Kuna watu wana kejeli kama sio matusi badala ya msaada au kutiana moyo. Tubadilike kutafuta mchumba mwenzi mke mume rafiki ndani ya JF sio jambo la ajabu tutumie akili zetu vizuri tulizopewa na Mungu na tulizoongezewa mashuleni. Ukiona mada haikuhusu potezea walianzisha jukwaa hizi si vichaa au walevi ! Kuna Love Connect za kulipia pesa nyingi sasa hii ya bure kejeli nyiiiingiWell said mtoa mada.
 
[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…