Unafiki mbaya sana....
Utasikia:-
"So sad"
"Jamani inaumiza sana"
"Mwili wangu wote umesisimka"
Simply because ni Mtoto wa Kizungu.
Ni unafiki wa kipuuzi sana. Ndio maana hata viongozi wetu wanatuongoza kinafiki nafiki.
Unajifanya unajali sana mtoto mmoja wa kizungu anaye ugua Cancer.. Wakati watoto wa kiafrika huku barani Africa wanakufa kila kukicha.....
View attachment 447106
Tuacheni unafiki wa kujipendekeza.
Katika kipindi/muda ambacho Dogo Bradley ametabiriwa kuishi kabla hajakutana na Kifo chake, bila shaka yapata watoto takribani 20 wa kiafrika watafariki. Je hao 20 si muhimu zaidi.
Au mnamaanisha tuonyeshe kuumizwa sana na mtoto Bradley kwa kuwa yeye ni wa kizungu? Halafu tuwapotezee hawa wakwetu kwa sababu kifo kwao ni kawaida?
Mkuu nahisi hujui maana ya unafki... ungekuwa unajua maana ya neno unafki usingekuja na uzi wa namna hii. ngoja nikupe sifa moja kuu ya mnafiki...
Mnafiki ni mtu ambaye hayupo real, atafanya jambo X huku moyon mwake anaamin katika jambo Y, aina hii ya watu wanapatikana CCM... sasa turudi kwenye mada..
unadhani watu walioguswa na habari za huyo mtoto wa kizungu ni wanafki? unadhani ndani ya mioyo yao hawajaguswa na hiyo habari?
mkuu hawa watu wapo real sana, wameumizwa sana, wengine wamelia sana na wengine wamefunga kwa ajili ya maombi.
Badala ya kuwaita wanafki ni bora ukawaonea huruma, hawa ni watumwa wa kifikra, wametekwa akili na wazungu na katika hili wazungu wamefanikiwa sana.
Lengo la wazungu limetimia, kuna mtu anamnyanyasa mtoto wake wa kambo, hampendi kabisa anamnyima chakula, anamyima elimu bora ila hili la mtoto wa kizungu limemuumiza mno na limemfanya akose usingizi.
Huyi mtu sio mnafiki ni mpumbavu, punguwani, mshamba, lofa, bwege, hayawani tu.
nasubiri mapovu ya wadau