Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Katika zama hizi za taarifa za haraka, tumeshuhudia tabia inayozidi kuenea ya “kuiba” mafanikio ya watu kwa misingi ya asili ya wazazi, badala ya ukweli wa uraia na uwakilishi halisi.
Mfano ni leo mwanadada Kelly Doulla, mwanariadha anayewakilisha Italia, lakini anayepewa heshima na umaarufu kwa jina la Cameroon au Afrika mara anaposhinda.
Ni muhimu kutofautisha kati ya urithi wa damu na utambulisho wa kisheria na kitaifa. Mwanadada Kelly alizaliwa, kukulia, na kushiriki mashindano chini ya bendera ya Italia. Kitendo cha kumtaja kama “mcameron” baada ya ushindi ni kupotosha historia na kuinyang’anya nchi inayomlea sifa yake halali.
Vyombo ya habari vya Afrika na mitandao ya kijamii zinapaswa kuacha tabia ya kuchukua tuzo za mtu na kuzigeuza kuwa hadithi za “ushindi wa bara fulani” bila kuzingatia ukweli. Uaminifu wa taarifa unavunjika tunapopuuza pasipoti na bendera, tukikimbilia kuenzi asili pekee.
Mafanikio ya Kelly Doulla ni ushindi wa Italia kama nchi na sio Cameroon. Heshima yake inapaswa kutolewa kwa taifa analoliwakilisha, bila kubadilisha ukweli ili kufurahisha hisia za kizalendo cha mbali. Huu ndio uandishi makini unaostahili kusimamia ukweli.