Acheni upotoshaji: Kelly Doulla ni Muitaliano, sio Mcameroon

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Katika zama hizi za taarifa za haraka, tumeshuhudia tabia inayozidi kuenea ya “kuiba” mafanikio ya watu kwa misingi ya asili ya wazazi, badala ya ukweli wa uraia na uwakilishi halisi.

Mfano ni leo mwanadada Kelly Doulla, mwanariadha anayewakilisha Italia, lakini anayepewa heshima na umaarufu kwa jina la Cameroon au Afrika mara anaposhinda.

Ni muhimu kutofautisha kati ya urithi wa damu na utambulisho wa kisheria na kitaifa. Mwanadada Kelly alizaliwa, kukulia, na kushiriki mashindano chini ya bendera ya Italia. Kitendo cha kumtaja kama “mcameron” baada ya ushindi ni kupotosha historia na kuinyang’anya nchi inayomlea sifa yake halali.

Vyombo ya habari vya Afrika na mitandao ya kijamii zinapaswa kuacha tabia ya kuchukua tuzo za mtu na kuzigeuza kuwa hadithi za “ushindi wa bara fulani” bila kuzingatia ukweli. Uaminifu wa taarifa unavunjika tunapopuuza pasipoti na bendera, tukikimbilia kuenzi asili pekee.

Mafanikio ya Kelly Doulla ni ushindi wa Italia kama nchi na sio Cameroon. Heshima yake inapaswa kutolewa kwa taifa analoliwakilisha, bila kubadilisha ukweli ili kufurahisha hisia za kizalendo cha mbali. Huu ndio uandishi makini unaostahili kusimamia ukweli.
 
Hakuna Muitaliano ' mweusi ' ... Wote ma black wanajipendekeza

Huyo ukianza kurejea kizazi chake kwenda nyuma Babu Wa Babu yake utakuta kama sio mcameroon ni mmatumbi Wa mpitimbi
 
Hakuna Muitaliano ' mweusi ' ... Wote ma black wanajipendekeza

Huyo ukianza kurejea kizazi chake kwenda nyuma Babu Wa Babu yake utakuta kama sio mcameroon ni mmatumbi Wa mpitimbi
Kwamba Mohammed Dewji ni Mhindi!? Sio Mtanzania?
 
Kuna vijana wa hovyo watakuja kuzikagua hizo picha za hiyo mwanariadha, halafu watakuja na mjadala tofauti kabisa na ule ambao unajadiliwa hapa. Labda kama wamebadilika siku hizi.
Vijana wenye mchango mdogo kwa taifa
 
Taifa Stars inaposhinda ni juhudi za mama,ila ikifungwa tunapewa zigo sisi
 
Taifa Stars inaposhinda ni juhudi za mama,ila ikifungwa tunapewa zigo sisi
Taifa Stars akimfunga Morocco ni timu ya Sa100 ila akipondwa ni timu ya watanzanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…