Acheni Ushamba, Hakuna gari za kike wala za kiume

Gari za kike ni zile zinazogaiwa bure tu kama zipo
kama gari inanunuliwa kwa pesa na pesa haina jinsia basi gari za kike hakuna..
Unaweza kukuta mtu ana Vits ya milioni 24 na mwingine ana Benz ya milioni 10
sasa 'uanaume' ni upi hapo?

Kula tano the boss , na like za kutosha

Ukishakuwa maskini tu hasa kiakili,kifikra utatumia udhaifu huo kuponda hali na mali za watu wengine
 
Tatizo lenu nyie watanzania ni vilaza kuanzia viongozi hivi nchi hata bulb ya gari imeshindwa kutengeneza sembuse kiwanda cha Tyre kilikufa leo hii mnaanza kubagua magari eti hili la kiume lile ni la kike!!!! Na mtu utakuta hajawahi kumiliki hata baiskeli kibaya zaidi hata mavi hana kwani uwe na mavi lazima uwe umekula ukashiba Aibu
 
Sasa mkuu...

Kweli umkute mtu kama WASIRA kwenye vitz inakuja hiyo.????
 
Leo umponde mtu na vitz yake waqt historia inaonyesha katika ukoo wenu mtu wa mwisho kumiliki chombo cha usafiri alikuwa marehemu babu yako alikuwa na avon baiskeli,kila mtu ana uwezo wake ila ukifuata kasumba unapotea.
 
Nenda Kinondoni uone waleee wa vidole juu wanavyomiliki
Dada NADIA hapo chini.Kwani hujui Kama NADIA jina la Mwanamke?
 
Najazia tena.
Sie huku Zanzibar na Hata Dar es Salaam,Tanga na ukanda mwingine wa Pwani.
Jina IPSUM,limo kwenye utamkwaji wa Jina la kike.

Wanawake wengi ukanda huo wana majina ya IPTSUM,ila ukitamka unaita IPSUM.

Sasa kina dada kaka wenye IPSUM kazi kwenu hapo chini,na ndio maana mundo wake ni sawa na DADA NADIA.

Dada IPSUM huyu hapa

 
Naendelea
Japan maranyingi hutumia majina ya watu wenye magari,sasa mwenye Jinsi utajijua.

Nikiendelea na kuja Na DADA SPACIOZA,kwa ufupi SPACIO

Majina ya SPACIOZA wengie tunawajua na wengine tumesoma nao.
Sasa huitwa kwa ufupi SPACIO

DADA SPACIO huyu hapa,
Naomba msinilaumu sio mie ni Japan huko,Maana wameona watu hawajitambui kwamba kuna magari ya kike na kiume.
Wakaona labda waweke majina ili watu wajue lakini wapi,au mnataka hadi waweke chupi za kike kwenye gari ndio mjue la kike.

Mdada SPACIOZA (SPACIO) huyuuu,Tena ana HIPS,duhh yaani wajapani hatari kweli,wanaweka hadi HIPS ili watu tujue la kike,lakini wapi.
 
Maneno ya wakosaji tu,acha mimi nijichange nijichukulie ka-ALTEZZA kangu soon!
 
Utakuta booonge la baba mtu kilo 120 ndani ya Nissan march au vitz.!!
 
Ni kweli hakuna gari ya kike na kiume lakini kwa gari nyingine za nyongeza kama passo, vits na vingine kwa kweli ziko ki dada zaidi.
 
Muda umepita ila imebidi nicheke tu.
 
mambo hayo yapo tanzania tu magari ya kike na kiume sijawahi kusikia nje ya nchi maneno hayo
 
mambo hayo yapo tanzania tu magari ya kike na kiume sijawahi kusikia nje ya nchi maneno hayo
Yapo ila kwa uchache sana. Ingia forum zao.
Sema hapa kwetu mtu atamponda anayeendesha ist kuwa ni ya kike huku yeye hana gari.😀
 
Hii mada imekuaje ikafa. Watu waliacha kununua gari za kike au wameelimika kwamba hakuna la kike gari ni gari? Hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…