Acheni Ushamba, Hakuna gari za kike wala za kiume

Unakuta kidume cha mbegu miraba sita anaendesha Vero-sa kwanza jina lenyewe utata!

Alafu seat za nyuma unakuta midoli kibao!
Labda yawezekana hicho kidume ni fundi magari kinafanya test. You never know!
 
Alafu seat za nyuma unakuta midoli kibao!
Labda yawezekana hicho kidume ni fundi magari kinafanya test. You never know!
Ulivyoweka utafikiri bongo nchi tajiri kweli, kumbe kanchi kenyewe masikini wa kutupwa watu wanashindia mlo mmoja na dollar 1 ni sawa na Tshs 2000 na soon itafika 3000..kuweni na uhalisia sio maisha ya artifial..hapa , mbaya zaidi ni third world country na akili za wananchi wake ndio kama zako.
 
Ahahaha,aisee humu kuna watu wamepanic ile mbaya,na inawezekana mleta post yumo njiani kununua,ila anasikilizia mood za watu kwanza.

Inawezekana watu tukawa tunaenda kwenye point moja kwa moja kwamba ya kike lazima iandikwe.
Hivi nani hajui kama kuna Baiskeli za kike na kiume,na nani hajui kama kuna Pikipiki za kike na kiume.Na zote hazijaandikwa kwamba is for Male or Female.
Ni sawa na mwanaume kuendesha gari ya pink au kuvaa nguo ya pink,lazima uwe kituko.Lakini je nani kasema kwamba Pink ni rangi za kike au wapi pameandikwa.
Cha kuzingatia hapa ni kwamba nimfumo ambao sie wenyewe tumeamua iwe hivyo,nandio ulivyo.
Na wale mliotoka kidogo miji ya watu ulaya ni kwamba mwanaume ukivaa nguo ya Pink usishangae ukaona unapata salama nyingi sana,ukisalimiwa na wenyeji huku wewe hata hujui kinachoendelea na kujiona kwamba umekirimiwa sana na wageni kumbe wao wanaujumbe mwingine na wewe unaujumbe mwingine kimavazi.

Na jinsi dunia inavyoenda kwa kasi,basi wewe nenda kesho Kariakoo,Kaangalie chupi,halafu uniambie kama kuna chupi zimeandikwa za kike au za kiume.Ila kitakachokufanya ujue hii chupi ya kike na kiume ni Shape yake tu.Sasa kwenye Gari is the same.
Ukweli sipendi kubeza hili,lakini Vitz na wenzie zimekaa kidada,sio siri.
Sasa kama mnasubiri kila kitu kiandikwe haya tuendeleeni
 
Gari za kike ni zile zinazogaiwa bure tu kama zipo
kama gari inanunuliwa kwa pesa na pesa haina jinsia basi gari za kike hakuna..
Unaweza kukuta mtu ana Vits ya milioni 24 na mwingine ana Benz ya milioni 10
sasa 'uanaume' ni upi hapo?

Ni kweli kabisa mkuu watu wamekariri.
 

Kwani wewe hicho ki - Passo chako umejaza midoli?
 

Jf ni kiboko kweli kweli.
 

mie wala sikatai kuwepo vitu vya kike au vya kiume, tabia za kike au za kiume n.k. Umenivika kilemba cha ukoka kuniambia si tusi kuitwa mwanamke. Labda kwenye jamii yako. Kwenye jamii yangu mwanamke ni kitu cha kudharaulika kwa mwanaume kiasi kwamba mwanaume akitaka kumkashifu mwenzake akimwambia "we si mwanamke" au "wewe si mama tu" panachimbika. Umesema mwanamme akiendesha gari la pinki ni kujidhalilisha kwa kuwa ni rangi ya kike, lakini mwanamke akiendesha gari la bluu haambiwi anadhalilika kwa kuendesha gari yenye rangi ya bluu - ya kiume. Kwa nini iwe hivyo kama uanamke ni heshima? Hata neno "kike" hapa limetumika kumdharau mwanaume anayeendesha magari madogo ya bei "rahisi". By the way rangi za pinki na bluu hutumika kutofautisha watoto wa kike na wa kiume. Tukishakuwa watu wazima maana ya hizo rangi inakufa. Tena shati la pinki kwa mwanaume linavutia sana, tena sana. Kwa hiyo haya ni maswala ya kimtazamo tu.

Mwanamke kutaka asionekane "tusi" au dhalili si kutaka usawa unaousema wewe wa dunia ya siku hizi, bali kutaka tu heshima ya kibidanamu kama ambavyo makundi mengine ya kijamii kama maskini au watu wa rangi fulani wanataka wapewe heshima kama wanadamu. Ndo hayo tu kaka. Wala hakuna haja ya mjadala.
 
Mtashika sana bomba za daladala,pamoja na kuomba lift,Range Rover,na Vitz zote zinakwenda shell,asilimia 80% ya wachangiaji hapa ni #DALADALa
 
Tena ni bora mwanaume ukaendesha bajaj kuliko hivyo vigari....vya......
 

Mkuu kama unataka kuona magari nenda LA, Vegas strip au Miami south beach
 
Yalikuwa yanaitwa "Juliana" na hata ugonjwa wenyewe mtu akiwa nao utakuta watu wanasema "anaumwa Juliana"
 
Mkuu kama unataka kuona magari nenda LA, Vegas strip au Miami south beach

Jamaa kanikumbusha east Sussex, brighton, niliona vitz kwa mara ya kwanza yani wanaita yaris. Nilivyorudi bongo nami nikanunua
 

Anaeshindia dollar moja kwa siku hafikirii gari achilia mbali kununua! Na wewe una akili kama wazungu wasiowahi kutoka nchini mwao?! Ukiifikiria TZ inakujia picha ya watu wa dollar moja kwa siku!?
 
Jamaa kanikumbusha east Sussex, brighton, niliona vitz kwa mara ya kwanza yani wanaita yaris. Nilivyorudi bongo nami nikanunua

Umenikumbusha mbali! Brighton & Hove! Mi nilikuwa Eastbourne hapo.
 
Rrondo vijana hawajuhi maisha ya wazungu, tv ni issue kuangalia
 
Hii inanikumbusha siku moja naendesha Vitz ambayo haina AC so vioo viko chini..nikakutana na mdada kwenye foleni ya Tabata akanikatia jichoo akasema ''kaka ungekuwa mwanamke hilo gari lingekupendeza kweli'' sikupata la kumjibu papo kwa papo mpaka dkk 5 baadae.Nilichofanya ni kwenda kuweka tint nyeusi na kuendelea kuinjoi ka-vitz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…