Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
DODOMA - JULAI 19, 2021
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI
ACHUKUA RUSHWA ILI MWANAFUNZI ASIENDE SHULE
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma leo Julai 19, 2021 inatarajia kumfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma Bw. Maliselo Kapampa Saveli (29) na kumfungulia mashtaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya mwaka 2019.
Bw. Saveli ambaye ni Kaimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mafurungu na pia ni Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Ilangali kilichopo Kata ya Manda wilaya ya Chamwino aliomba rushwa ya shilingi 600,000 na kupokea shilingi 400,000 kutoka kwa mtoa taarifa wetu ili asimchukulie hatua kwa kitendo cha utoro wa mtoto wake ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mafurungu.
Elimu ni ufunguo wa maisha na Serikali yetu inafanya juhudi kubwa kuimarisha mazingira ya utoaji elimu ikidhamiria kuwa huduma bora za elimu ziwafikie wananchi wote. Kitendo cha Mwalimu mmoja kudiriki kuomba na kupokea rushwa ili kukwamisha malengo hayo ikiwa ni pamoja na kuenenda kinyume na taaluma yake kwa kukwamisha badala ya kuchochea elimu ni kitendo dhalili na ni kinyume na mienendo ya walimu wengi wa mkoa wetu wa Dodoma.
Tunawataka walimu na wazazi wa wanafunzi mkoani Dodoma kuendelea kusisitiza umuhimu wa elimu na kamwe kutojiingiza kwenye vitendo vya rushwa na tabia nyingine za utovu wa maadili kwani RUSHWA HAILIPI.
Imetolewa na:
Sosthenes Kibwengo
Mkuu wa TAKUKURU (M) Dodoma
Simu: 0738150070