ACP Mwanyasi aongoza maofisa wa polisi K'njaro kutoa pole msiba wa ajuza wa miaka 120

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Habari Kutoka Dawati la habari polisi Kilimanjaro

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kupitia Polisi Jamii kwa kushirikiana na Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto, limetembelea familia ya marehemu Elizabeth Yohana Simba na kutoa pole kufuatia kifo chake akiwa na umri wa miaka 120, katika Kijiji cha Njari, Kata ya Uru Kaskazini, Wilaya ya Moshi.

Ziara hiyo iliyofanyika Oktoba 29, 2026, iliongozwa na Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Lazaro Mwanyasi, akiambatana na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto Mkoa huo, SSP Asia Matauka, pamoja na SP J. Kabelwa.

Akizungumza na familia ya marehemu, ACP Mwanyasi aliwasilisha salamu za pole kutoka Jeshi la Polisi na kueleza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na jamii, kwa kuzingatia falsafa ya kuwa Polisi ni Jamii na Jamii ni Polisi.

Aidha, familia ilihimizwa kumuombea marehemu na kuendelea kuyaenzi mema aliyoyafanya wakati wa uhai wake, kama sehemu ya kudumisha kumbukumbu na urithi mwema aliouacha.

Marehemu Bibi Elizabeth Yohana Simba ameacha watoto watano, wajukuu 34, vitukuu 64 na vilembwe 24, ambao wamepata fursa ya kushuhudia maisha yake marefu.

Katika ziara hiyo, Jeshi la Polisi pia lilikabidhi mkono wa pole kwa familia ya marehemu kama ishara ya kuwapa faraja na kuonesha mshikamano katika kipindi hicho kigumu.

Kwa upande wao, wanafamilia waliishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwatembelea, kuwapa pole na kuonesha kujali katika kipindi cha majonzi.

Ziara hiyo inaendelea kuonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii katika masuala ya kijamii, ikiwa ni pamoja na kujenga ukaribu, mshikamano na kuimarisha mahusiano nje ya shughuli za kawaida za kiusalama.
 
Attachments

  • IMG-20261030-WA0237.jpg
    IMG-20261030-WA0237.jpg
    285.1 KB · Views: 2
  • IMG-20261030-WA0238.jpg
    IMG-20261030-WA0238.jpg
    345.2 KB · Views: 2
  • IMG-20261030-WA0240.jpg
    IMG-20261030-WA0240.jpg
    342.6 KB · Views: 1
  • IMG-20261030-WA0236.jpg
    IMG-20261030-WA0236.jpg
    289 KB · Views: 2
  • IMG-20261030-WA0239.jpg
    IMG-20261030-WA0239.jpg
    294.6 KB · Views: 2
Kwa mauwaji wanayofanya hovyo hovyo na uonevu kwa wananchi mwambie akitoboa hata nusu ya hiyo ashukuru sana!
 
Habari Kutoka Dawati la habari polisi Kilimanjaro

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kupitia Polisi Jamii kwa kushirikiana na Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto, limetembelea familia ya marehemu Elizabeth Yohana Simba na kutoa pole kufuatia kifo chake akiwa na umri wa miaka 120, katika Kijiji cha Njari, Kata ya Uru Kaskazini, Wilaya ya Moshi.

Ziara hiyo iliyofanyika Oktoba 29, 2026, iliongozwa na Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Lazaro Mwanyasi, akiambatana na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto Mkoa huo, SSP Asia Matauka, pamoja na SP J. Kabelwa.

Akizungumza na familia ya marehemu, ACP Mwanyasi aliwasilisha salamu za pole kutoka Jeshi la Polisi na kueleza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na jamii, kwa kuzingatia falsafa ya kuwa Polisi ni Jamii na Jamii ni Polisi.

Aidha, familia ilihimizwa kumuombea marehemu na kuendelea kuyaenzi mema aliyoyafanya wakati wa uhai wake, kama sehemu ya kudumisha kumbukumbu na urithi mwema aliouacha.

Marehemu Bibi Elizabeth Yohana Simba ameacha watoto watano, wajukuu 34, vitukuu 64 na vilembwe 24, ambao wamepata fursa ya kushuhudia maisha yake marefu.

Katika ziara hiyo, Jeshi la Polisi pia lilikabidhi mkono wa pole kwa familia ya marehemu kama ishara ya kuwapa faraja na kuonesha mshikamano katika kipindi hicho kigumu.

Kwa upande wao, wanafamilia waliishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwatembelea, kuwapa pole na kuonesha kujali katika kipindi cha majonzi.

Ziara hiyo inaendelea kuonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii katika masuala ya kijamii, ikiwa ni pamoja na kujenga ukaribu, mshikamano na kuimarisha mahusiano nje ya shughuli za kawaida za kiusalama.
Huyu afande kavaaje kofia?
 
Back
Top Bottom