ACP Venance Mapala: Kioo kimoja cha Treni ya SGR kinagharimu sio chini ya Milioni 300

Muongo huyu. Amepata wapi hiyo gharama? Ukweli ni kwamba hata huko Germany zinakoundwa hizo train, haijawahi kutokea eti wanabadilisha kioo cha train. Sasa hapa kwetu tunavinja vioo vya train?
Mkuu haujawahi kusafiri na train ya kati?

Mikoa ya Dodoma na Singida ni mikoa hatari sana kwa kurushia train mawe.

Msipofunga vioo kuna hatari ya kupasuliwa vichwa.
 
Kioo ambacho kinazuia risasi ndio kipo bei juu ila sio bei ya huyu Mtanzania na pia vioo vya kawaida tu vya bei kubwa ni ngumu kuvunjika kwa mawe..
 
Tayari wanataka kupiga pesa.., wataanza kuvunja vioo wenyewe kila mwezi mara mbili, wanavuta 600mil.
 
Yuko sahihi. Hapo maana yake amejumlisha gharama zote! Mfano nauli ya kukifuata hicho kioo Ujerumani au Korea Kusini na kurudi, kuna posho ya safari, marupurupu na 10% itakayokatwa ili apewe baada ya kukutana na muuzaji, nk.
 
Behewa moja lina madirisha kama 22 hivi mara shs 300,000,000/=! Vile vioo vimetengezwa kwa madini ya almasi, havivunjiki kirahisi, ila yeye si msemaji wa TRC na ninaamini TRC watasema haizidi £300.00.
 
Mkuu haujawahi kusafiri na train ya kati?

Mikoa ya Dodoma na Singida ni mikoa hatari sana kwa kurushia train mawe.

Msipofunga vioo kuna hatari ya kupasuliwa vichwa
Hilo nalielewa, ila hiyo bei aliyotaja, du! Na labda kama hiyo ndio bei basi ni gharama nafuu kushughulikia wanaorusha mawe kuliko kusuiri wavunje na ku-repair vioo. Kuweka watu wanaolipwa maeneo hayo ambao wanakuwa informers/walinzi dhidi ya wanaorusha mawe haitagharim fedha nyingi kiasi hicho
 
Huyo muongo, spare ya kioo izidi bei ya basi la abiria!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…