John Gregory
JF-Expert Member
- Jul 14, 2019
- 1,137
- 2,147
Hii ni story Inayomhusu kijana aliyepambana katika harakati za kutimiza ndoto zake, akiwa bado mwanafunzi wa chuo akapata mwanamke waliyefunga naye ndoa. Mwanamke huyo alikuwa na mchango mkubwa wa hali na mali ambapo aliuza mpaka nyumba ya urithi ya familia pamoja na kutumia pesa zote alizorithi kwa wazazi wake.
Mwishowe alimkatia tamaa kwamba hataweza kutimiza ndoto yake, akaomba talaka waachane, na isivyo bahati wakati tu anatalikiana, Ndoto za dogo zikatimia!
Hali hii ikamfanya mwanadada achanganyikiwe na akili za kulipiza kisasi cha damu zikamuandama!
Picha iko hivi;
Melinda Moore (pichani), Mdada mzuri na mrembo, anakutana na mwanafunzi wa uhandisi Robert, Kijana tall dark na handsome wote wakiwa wanafunzi wa chuo kikuu, anakutana naye katika mazingira yasiyo rafiki baada ya Robert kumparamia na kumgonga bega Melinda kwa bahati mbaya walipokuwa wakipishana kwa haraka kukimbia mvua iliyokuwa ikipiga kwa nguvu, Jambo lililopelekea Melinda kuangusha vitabu vyake maana alikuwa akitoka darasani kujisomea, huku mvua ikiendelea kunyesha, kwa hasira alimfokea sana Robert. Baadaye siku hiyo, Robert anamtembelea Melinda chumbani kwake ili kurudisha karatasi ambazo zilichanganyika katika ugomvi siku alipopishana na kumgonga bega bahati mbaya. Huo ukawa mwanzo wa kufahamiana, Hasa ukizingatia Robert alikuwa na akili darasani akawa anamsaidia Melinda kimasomo.
Siku zikaenda, Hatimaye siku moja Melinda akaletewa taarifa ya kufiwa na mama yake mzazi. Robert akazidi kuwa naye bega kwa bega, Hatimaye baadaye baada ya kufarijiana, Melinda anamtembelea Robert kwenye kibanda chake anachoishi kimasikini, na Bwana mdogo Robert anafanikiwa kula tunda kimasihara 😀
Hatimaye Melinda anaamua kumnunulia Robert gari jipya. Licha ya kuwa hajaomba gari, aliipokea.Baadaye Robert anamuelezea Melinda changamoto yake ya ada, Melinda anaamua kumlipia Robert ada .Baada ya mapenzi yao kuzidi, kuna siku Robert hakumpigia simu Melinda siku nzima, Jambo ambalo halikuwa la kawaida. Melinda anaamua kumpigia simu. Robert anaanza kujiuma uma, jambo lililompa Melinda mashaka, Melinda akaamua kwenda haraka na kisiri siri mpaka mahali anapoishi Robert kwa lengo la kumfumania.
Lahaula! kumbe kweli bwana! Melinda anamfuma Robert akiwa na Diana Wells, mwanamke mwingine ambaye ni classmate, wakiwa uchi wakivunja amri ya sita!. Akiwa na hasira, Melinda anaendesha gari lake kwa nguvu na kugonga kibanda cha Robert. Anashuka kwa hasira anaharibu gari la Robert kwa tofali kabla ya kuzimia kutokana na jeraha alilopata baada ya kuendesha gari na kugonga nyumba ya Robert kwa nguvu. Melinda anakimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu ya dharura, baadaye anapewa taarifa kuwa amekuwa tasa kutokana na majeraha.
Baada ya wiki kadhaa Robert anamtembelea Melinda hospital anaomba msamaha na Melinda anamsamehe Robert, wanapatana na kuoana, licha ya pingamizi kutoka kwa dada zake, June na Brenda. Brenda anamuonya Melinda asimwambie Robert kuhusu kiasi cha pesa alichoachiwa na mama yao.
Jambo ambalo lilikuwa gumu kwa Melinda, kwani baada ya masomo Robert hakupata kazi na wala hakuweka juhudi yoyote kwenye kutafuta kazi, kwa sababu aliamua kujikita katika kuendeleza uvumbuzi wake wa Betri ya upepo (Gayle force wind).Hivyo hakuwa na mchango wowote hapo nyumbani, kwa waswahili tunasema Robert alikuwa Mario kwa Melinda, kwani Melinda alifanikiwa kupata kazi hivyo ndiye aliyegharamikia kila kitu hapo nyumbani, kuanzia umeme,chakula,mavazi nk. mpaka gharama za vifaa vya utafiti wa jamaa yeye ndiye aliyegharamia huku jamaa akiwa hana hata dalili ya kutafuta mbinu au njia mbadala kama kibiashara au kikazi cha kujishikiza ili kujipatia kipato bali aliendelea kukomaa na project yake.
Robert anazungumza na Melinda kuweka rehani nyumba yao ya urithi ili aweze kupata hela ya kuendelea na utafiti wa project yake ya betri ya upepo ambayo amekuwa akiihangaikia akiibuni kwa miaka mingi kwa matumaini ya kuiuza kwa mwekezaji mkuu na tajiri, Prescott ambaye ni mmliki wa kampuni kadhaa ikiwemo Prescott inc. Diana Wells (Classmate aliyefumaniwa kipindi wako chuo), ambaye sasa anafanya kazi kama msaidizi wa Prescott, anakutana kwa bahati nzuri au mbaya na Robert akiwa ametoka kufukuzwa na walinzi alipojaribu kuonana na Prescott.Robert anampa taarifa Diana, kwamba yeye ameshaoa muda mrefu na mke wake ni yuleyule Melinda, Hivyo Robert anamuomba Diana wakutane kufanya mazungumzo kwa lengo la kumuomba afanye juu chini ili aweze kuonana na Prescott na kumuelezea kuhusu project yake. Diana anamkatalia mara ya kwanza, Robert anamsisitiza si suala la mapenzi, bali ni strictly business. Hatimaye Diana anakubali na anapanga kuonana na Robert baada ya kazi. Wakati huo Robert akifanya kazi kama dereva wa lori la delivery, kazi aliyopatiwa na kulazimishwa kufanya na familia ya Melinda baada ya kuonekana anamtesa ndugu yao!. Familia ya Melinda wanampa kazi ya udereva Robert ili waweze kurudisha mkopo baada ya kuweka nyumba ya urithi rehani.
*************************************************************************************************************
Hatimaye Robert na Diana wanakutana na wanazungumza, ila kwa bahati mbaya Diana anadondosha na kusahau pochi yake kwenye Lori la Robert. Baadaye June na Brenda wanampa taarifa Melinda kuhusu pochi ya Diana waliyoikuta kwenye lori la Robert, June na Brenda wanamwambia Melinda kwamba Robert anamcheat. Jambo ambalo halikuwa kweli (Tangu Robert alipomsaliti Melinda na kusamehewa kisha kufunga ndoa, Robert alimpenda sana mke wake na hakuwa na nia hata kidogo kumsaliti mke wake, hata Diana alilifahamu hilo na hata walipokutana mazungumzo yalihusu project yake na namna ya kumfikia Prescott)
Akiwa njiani akiendesha lori katika kazi yake mpya ya delivery, Robert anapigiwa simu na Diana akisema Prescott anataka kufikiria upya mpango wake. Robert anashtuka na kupaki lori pembeni ili wazungumze. Diana anamueleza kwamba Prescott amekubali njoo uzungumze naye! Haraka Robert anageuza lori na kuahirisha delivery aliyokuwa ameagizwa akaelekea nyumbani ili kuchukua prototype ya betri kuipeleka kwa Prescott. Robert anafika nyumbani anakuta prototype ambayo alikuwa ameikatia tamaa na kuitupa kwenye dustbin ikibebwa na wazoa taka tayari kwenda kutupwa, haraka akawazuia wasitupe akaichukua, Mara Melinda huyu hapa akiwa na pochi yenye picha na vitambulisho vya Diana ambavyo alidondosha kwa bahati mbaya kwenye lori la Robert, Melinda alianza maneno na kumrushia ngumi Robert, mara Familia ya Melinda (Brenda na June) na wakaingia, hajakaa sawa mashemeji wa familia (waume wa dada za Melinda ambao walimpatia hiyo kazi) wakafika wakimtaka arejeshe funguo na kumnyang'anya lori kwa kushindwa kazi, Kwa kifupi paliibuka tafrani kubwa sana.
Robert anawasili kwa Prescott kwa kuchelewa baada ya kunyang'anywa gari na kulazimika kupanda daladala. Prescott anamueleza Robert kwamba yupo tayari kutoa $800,000 kununua project yake, ni pesa nyingi ambayo ingetosha kulipa deni la benki na kurudisha nyumba ya urithi ambayo tayari ilishachukuliwa na benki baada ya kushindwa kurejesha mkopo. lakini Robert hakuwa tayari kuuza kazi yake bali anataka kuwapa leseni ya teknolojia hiyo na yeye awe sehemu ya project yake. Hivyo pamoja na shida alizonazo na ushawishi wa kiwango hicho kikubwa cha fedha kilichowekwa mezani na tajiri Prescott, Robert anakataa kuuza project yake.
*************************************************************************************************************
Robert anarejea nyumbani akiwa amekata tamaa, anawakuta Melinda, dada zake pamoja na mashemeji wakiwa kimya kwa hasira na kumtafakari. Robert anaenda kwa mke wake Melinda, anajaribu kumuelezea na kumsisitiza kwamba hakuwahi na hatokaa amcheat na anampenda sana, anamuelezea kwamba Prescott alitaka kumpa dola 800,000 ila amekataa kuuza kazi yake. Melinda na familia yake wanamshangaa kukataa ofa hiyo wakati benki tayari imeshatoa vyombo vyao nje ili kupiga mnada nyumba yao ya urithi, Melinda anawasikiliza ndugu zake, anakataa kumuamini Robert akisema ni uongo na hana mazungumzo zaidi zaidi ya jambo moja tu, Talaka. Yes! Melinda akadai talaka yake, Robert akafukuzwa na ndugu wa Melinda na nyumba ikafungwa na kuchukuliwa na benki. Melinda akahamia kwa dada zake, Robert hakuwa na pakwenda akajipatia kazi ya kuosha vyombo kwenye mgahawa mmoja, ambapo usiku alijilaza kwenye moja ya vyumba duni vya mgahawa huo.
Melinda alianza kudate na wanaume wengine, Siku moja wakati Melinda akidate na mwanaume mmoja wakiwa katika mgahawa anaofanya kazi Robert, alimuona kwa mbali, hasira zikampanda akiwaza gharama kubwa alizotumia kuanzia kumsomesha Robert na ku'fund' project yake leo anaishia kuwa muosha vyombo kwenye mgahawa! 😀 . Hatimaye Familia ya Melinda na mwanasheria wao wakiwa mbele ya hakimu, Robert akaitwa aje atie saini hati ya talaka, Robert huku akitokwa machozi alimueleza mke wake Melinda jinsi anavyompenda, na kwamba hayupo tayari kumpa talaka waachane, kwamba amejitahidi kadri ya uwezo wake kutimiza malengo na ndoto zake lakini imekuwa ngumu hivyo anaomba amsamehe asichukue uamuzi huo, Lakini ombi lake halikufua dafu kwani Melinda na familia yake walishadhamiria kuachana kabisa na Robert. Mwisho talaka ikasainiwa na Robert akaondoka akisema hahitaji chochote kutoka katika mgawano wa mali kama ilivyo desturi pale wanandoa wanapotalikiana hugawana mali, lakini Robert aliondoka kama alivyo huku akitokwa machozi.
***************************************************************************************************************
Akiwa katika shughuli zake za kuosha vyombo mgahawani, Robert anapokea simu, Diana anamuuliza mahali alipo, Robert anamueleza kwa sasa hana pa kuishi, alishatalikiana na mke wake na anafanya kazi katika mgahawa kama muosha vyombo. Diana anamuonea huruma, anaamua kumpa hifadhi na kumrudia tajiri Prescott ili aweze kutizama kwa mara nyingine ombi la Robert. Siku moja asubuhi Robert akiwa anawahi katika shughuli zake za mgahawani, Diana anampatia habari njema, anampatia files za mikataba ya mamilioni ya dola iliyosainiwa na tajiri Prescott, Kwamba amekubali kufanya partnership na project yake, hivyo hatimiliki itabaki kuwa yake na watafanya kazi pamoja na Prescott. Robert anabubujikwa na machozi akimshukuru Diana.
Baada ya muda kupita, Robert wakati huo ameshakuwa milionea mkubwa (thamani ya mkataba ilikuwa ni zaidi ya dola milioni 150) aliamua kumtembelea Ex-wife wake Melinda kazini kwake. Alifika kisha akasimama mlangoni akiwa ameshika ua jekundu lenye manukato safi akiwa amevalia suti maridadi na nadhifu. Melinda alipomuona Robert, kwa dharau akainuka kwenda kumsikiliza akijua ni usumbufu wake kama kawaida, Robert akamsalimia, Melinda akajibu kwa nyodo, akimsisitiza kuwa yupo busy hivyo anampatia dakika 10 tu aseme shida iliyomleta huku akimsisitiza kwamba hawawezi kurudiana tena hivyo asijisumbue kuazima suti za gharama na kununua maua ya gharama kumfurahisha maana haitawezekana kamwe kurudiana, Baada ya Robert kumsikiliza na kuvumilia vichambo alivyokuwa akipatiwa na Ex wife wake Melinda, alimpa taarifa Melinda kwamba project yake imefanikiwa na yupo katika biashara na Prescott, hivyo ameona ni vyema kurudi kwa ajili ya kumshukuru kwa mchango wake katika kutimiza ndoto yake, akazama mfukoni akatoa cheki ya dola milioni 10 akampatia Melinda, akampatia lile ua jekundu lenye manukato mazuri akisindikiza na kiss nzuri katika paji la uso 😀 akamwambia samahani nimetumia zaidi ya dakika 10 ulizonipatia, akiwa anataka kuondoka, akakumbuka jambo, akazama tena mfukoni akatoa funguo akampatia Melinda, akamwambia huo ni ufunguo wa nyumba ya urithi wa familia yako iliyopigwa mnada na benki baada ya kushindwa kurejesha ule mkopo, akamwambia nimeinunua na nimeifanyia ukarabati na kuiboresha zaidi, kisha akamalizia 'Goodbye Melinda'
Weeee! Unajua nini kilifuata? 😀😀😀