ACT: Hatutafuata Maelekezo ya Msajili kumtengua Mpina kuwania Urais, tutafungua kesi Mahakamani

Hivi unavyosema utamgomea Msajili

Hiyo Fomu ya URais inatolewa na Nani kama sio huyo huyo Msajili

Lissu alipokuwa anahubiri reforms, mlidhani ni za CDM pekee eeh

Kwa kifupi jipangeni kumpata mgombea mwingine wa Chama chenu

Otherwise, msimamisheni Zitto wenu
 
ni lini ACT walisema hawataki reforms?
 
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea taarifa kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya uamuzi wake wa kutengua ugombea wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama inaipitia kwa umakini hatua hii ya Msajili wa Vyama vya Siasa na katika wakati muafaka tutatoa mwelekeo wetu wa kina.

MSIMAMO WA AWALI
Wakati uchambuzi wa awali ukiendelea kufanyika tunapenda kutoa msimamo wetu wa awali juu ya suala hili kama ifuatavyo;

1. Chama cha ACT Wazalendo kinaweka msimamo kuwa hakitofuata maelekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya suala hili kwa sababu katika mazingira ambayo mchakato wa uchaguzi umeshaanza, Tume ya Uchaguzi imeshatoa fomu na wagombea wakiendelea na taratibu za ujazaji na urejeshaji wa fomu, Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia mchakato huo isipokuwa kwa njia ya pingamizi.

Mgombea wetu wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Luhaga Joelson Mpina amechukua fomu, amezijaza, amezunguka nchi nzima kusaka wadhamini, amekula kiapo mahakamani na kukamilisha taratibu zote zinazohusu ukamilishaji wa fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo tarehe 26 Agosti 2025 fomu hizo zimehakikiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kesho saa 7.00 mchana zitawasilishwa Ofisi ya Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya uteuzi.

2. Chama cha ACT Wazalendo kitafungua kesi Mahakama Kuu kupinga hatua hii ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Katika kesi hiyo, Chama kitaweka zuio (injunction) dhidi ya utekelezwaji wa uamuzi huu hadi kesi ya msingi isikilizwe.

Ado Shaibu,
Katibu Mkuu, ACT Wazalendo
26 Agosti 2025

Pia soma ~
ACT: Tumepokea barua ya Msajili kuhusu Mpina, tutafungau kesi Mahakamani
Kwa hili ACT wako sawa ,kama msajili anatengua mgombea wa ACT, amtengue wa ccm pia upumbavu ufike mwisho sasa
 
Uchaguzi uliopita Mbona Huyu mkurugenzi hakumtengua marehemu Membe alipogombea Urais? Au sheria imebadirishwa safari hii?
 
Wakikaidi chama kifungiwe kufanya siasa au kifutwe
 
Stupid kabisa. Si walisema mhuni asusiwi. Sasa wapambane na mhuni. Stupid kabisa.
 
Hivi unavyosema utamgomea Msajili

Hiyo Fomu ya URais inatolewa na Nani kama sio huyo huyo Msajili

Lissu alipokuwa anahubiri reforms, mlidhani ni za CDM pekee eeh

Kwa kifupi jipangeni kumpata mgombea mwingine wa Chama chenu

Otherwise, msimamisheni Zitto wenu

Sidhani kama wa muda wa kuteua mgombea mwingine. Muda wa kuchukua fomu umeisha
 
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea taarifa kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya uamuzi wake wa kutengua ugombea wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama inaipitia kwa umakini hatua hii ya Msajili wa Vyama vya Siasa na katika wakati muafaka tutatoa mwelekeo wetu wa kina.

MSIMAMO WA AWALI
Wakati uchambuzi wa awali ukiendelea kufanyika tunapenda kutoa msimamo wetu wa awali juu ya suala hili kama ifuatavyo;

1. Chama cha ACT Wazalendo kinaweka msimamo kuwa hakitofuata maelekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya suala hili kwa sababu katika mazingira ambayo mchakato wa uchaguzi umeshaanza, Tume ya Uchaguzi imeshatoa fomu na wagombea wakiendelea na taratibu za ujazaji na urejeshaji wa fomu, Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia mchakato huo isipokuwa kwa njia ya pingamizi.

Mgombea wetu wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Luhaga Joelson Mpina amechukua fomu, amezijaza, amezunguka nchi nzima kusaka wadhamini, amekula kiapo mahakamani na kukamilisha taratibu zote zinazohusu ukamilishaji wa fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo tarehe 26 Agosti 2025 fomu hizo zimehakikiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kesho saa 7.00 mchana zitawasilishwa Ofisi ya Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya uteuzi.

2. Chama cha ACT Wazalendo kitafungua kesi Mahakama Kuu kupinga hatua hii ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Katika kesi hiyo, Chama kitaweka zuio (injunction) dhidi ya utekelezwaji wa uamuzi huu hadi kesi ya msingi isikilizwe.

Ado Shaibu,
Katibu Mkuu, ACT Wazalendo
26 Agosti 2025

Pia soma ~
ACT: Tumepokea barua ya Msajili kuhusu Mpina, tutafungau kesi Mahakamani
The game is over, hizo nyingine ni abracadabra tu.
 
Mumlinde mgombea wenu wa "ulais" kama mtakavyolinda "kula" zenyu.Mpambano uendelee!
 
Back
Top Bottom