ACT: Tunaitaka Serikali ya JMT, kuacha utowaji wa Leseni kwa eneo la Fungu Mbaraka na Bahari Kuu upande wa Zanzibar

mkuu kwani Fungu Mbaraka ni bahari? sisi tunazungumza kisiwa wewe unaleta refrence ya Ocean
Ndio kabisa kwa ukaribu wa coastline ya bara na Zanzibar, bara wana strong claim ya kisiwa kushinda Zanzibar.

Halafu wazanzibari mnafurahisha sana hivi unadhani kuna mtu atakują kujenga refinery ya LNG tena Zanzibar, wakati bara inajengwa.

Hiki ndio kitakachotokea hata sehemu za Zanzibar zikibainika zina commercial wells, refinery inatafanyika bara, serikali ya bara itawatoza hela kwa sababu mafuta sio maswala ya muungano.

Sasa kwa akili zenu huko mbele mtasema sisi nchi moja kwanini mtutoze kutumia refinery baada ya kuona mapato mtakayopata ni kiduchu.

Akili za viongozi wa ACT ni fupi sana, akitokea mtu wa kuuvunja huo muungano ndio akili zao zitakaa sawa.
 
Kutokea Tanganyika hadi fungubaraka ni km7 hadi nane hivo wao kutokea Tanganyika wako km42 wanatakiwa wapige hesabu halafu watulie ,
Waanze kwanza kuipigia kelele Mnemba wakimaliza waje kwenye hicho kisiwa
 
Zanzibar ilitolewa mikononi mwa Ujerumani ya Africa Mashariki (Tanganyika) kwenye mkataba wa heligoland treaty

Wazanzibar wajue Miaka 50 ijayo hakutakuw na Zanzibar kama nchi
 
Nimesikia mara kadhaa kuwa mafuta na gesi asilia ni jambo la Muungano na nilisoma mahala kuwa viliongezwa kuwa jambo la 15 la Muungano mwaka 1968. Je ni lini vimeacha kuwa vya Muungano?
 

Mkuu mbona unajizonga sana? claims za nini? Katiba ya Tanganyika before union mipaka yake ilikua ipoje na ya Zanzibar before union mipaka yake ilikuwa ipoje? hicho ndicho cha kutatua huo mgogoro
 
Mkuu usitafune maneno, Fungu mbaraka ni ya Zanzibar au Tanganyika? tupe jibu
Ibara ya kwanza ya Katiba ya JMT inasema “1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano".
Ibara ya pili ya katiba ya JMT inasema
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Hivyo Zanzibar haina eneo, haina mipaka, Fungu Mbaraka ni eneo la JMT.
P
 
Nini maana ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ikiwa kuna sehemu ndani ya nchi haina mamlaka!?
Huu muungano kwa sasa upo kisiasa lakini naona hapa kuna nchi mbili tofauti, Bora katiba ya serikali tatu ingepitishwa tu ili ziwepo mali za watanganyika na wazanzibari na mali za wote, na sio wazanzibari wana vya kwao halafu vyetu huku bara mali zetu ziwe za wote hii haiko sawa
 

..vigogo walioko katika mamlaka hawataathirika bila kujali muungano upo, au haupo.

..tena inawezekana uwepo wa muungano unawanyima nafasi ya kuiba na kufisadi vya kutosha.
 
..vigogo walioko katika mamlaka hawataathirika bila kujali muungano upo, au haupo.

..tena inawezekana uwepo wa muungano unawanyima nafasi ya kuiba na kufisadi vya kutosha.
Kuiba nayo si inataka mapato, kitu pekee nje ya utalii itakuwa kuruhusu wachina kwenda kuvua samaki.

Vinginevyo hamna kitu zaidi ya hadithi za kuombea kuwa ‘safe haven’ ya wakwepa kodi; kama Bahamas ambayo ni karibu na US ndio maana watu wanafungua makampuni hewa huko. Zanzibar ni mbali sana.

OMO ana nadharia za ajabu sana kichwani kwake, kesho utasikia refinery iajiri theluthi moja wa Zanzibar.

Ni watu ambao predictable (me, me, me).
 

Sijazungumzia JMT nimezungumzia Tanganyika mkuu
 

..wazanzibar wana haki ya kujitetea, na kujinufaisha, ndani ya muungano.

..watanganyika tujilaumu wenyewe kwa kushindwa kutetea haki na maslahi yetu
 
..wazanzibar wana haki ya kujitetea, na kujinufaisha, ndani ya muungano.

..watanganyika tujilaumu wenyewe kwa kushindwa kutetea haki na maslahi yetu
Nadhani huko mbele wakileta za kuleta huo muungano utavunjwa hata wabara washaanza kuchoka.

Uvumilivu nadhani ni kwa malengo ya kuwa accommodate tujione watu wamoja.

Ila I am sure kuna watu washaanza kuwachoka, kwa sasa wanakopa kushinda income revenue yao; bara kama guarantor vinginevyo wao wenyewe hawana uchumi wa kukopa hovyo kama wanavyofanya sasa.

Waki-default bara ndio inalipa na sidhani hata hivi sasa CAG akikagua kama wanaleta hela zao malipo on time.

Watu kama OMO wanaona rahisi kwa sababu ya uvumilivu wa bara tu.
 
Tena akina OMO wamepata nguvu kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote.
Wanamtaka Rais Samia asiruhusu kuingilia mambo yao ya mafuta na gesi tu, mengine apeleke huko kama ilivyo sasa

Rasilimali za Tanganyika ni za wote tena zikitumika Zanzibar kuliko eneo jingine lolote la Tanganyika.
Chochote cha Tanganyika kwa jina la Tanzania ni chao pia, lakini chao ni chao.

Sioni tatizo wakipigania rasilimali zao, tunachohitaji ni Tanganyika ili isimamie masilahi yake.
Kama kuna ulazima tuwe na muungano! kama Wazaznibar wanataka maana Mtanganyika hana cha kupoteza !
 
Wazee wenye sentiments za muungano upande wa bara wapo lala salama.

Huko mbele sioni watu wakukubali kuburuzwa na kuendelea kuwachekea. Labda huko CCM wawe wanalea kweli walinda muungano wa kesho.

Mafuta vitalu vingi ni unitisation, mara nyingi wanaofanya exploration na wanaotumia ni tofauti. Vyovyote vitaishia kwa either Shell, Equinor na Exxon Mobil. Kwa jinsi mambo yanavyofanyika kwengine duniani.

Sasa ngoja wa ujue ukweli huo, hao hao waliopiga makelele mafuta sio maswala ya muungano. Wakibaini refinery inafanyika Tanzania; utasikia hadithi zao mpya, awataki kulipia charges zozote na wapewe ajira.

Predictable
 
Zikichape kidogo akishinda zenji achimbe wese akishinda Tanganyika amiliki kisiwa afukue wese,,,,,tumechoka vitisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…