Hivi anaposema Tanganyika inaionea Zanzibar ni muongo au ni wewe unajitia upofu na uziwi?
Tanganyika ina watu milioni 60, Zanzibar ina 1.2 na kati yao nusu wanaishi Tanganyika.
Eneo na Uchumi wa Tanganyika huwezi kuweka katika mizani.
Mkoa mpya wa Simiyu ni mKubwa kuliko Zanzibar kwa kila kitu
Makusanyo ya kodi Zanzibar kwa 2023 ilikuwa Bilioni 58 kwa mwezi.
Kiasi hicho ni kampuni 3 tu za Tanganyika.
Hivi inapokuja, kwa mfano, misaada kwa Tanzania halafu Zanzibar isipewe chochote sio kuionea?!
Misaada inayopewa ni fadhila. Fikiria kwamba kuna misaada ya Trillioni 1, kwa mujibu wa OMO zigawanywe Bilioni 500 kila upande. Hivi hapa kuna fikra kweli ! Lakini pia Misaada ni Fadhila kwasababu hizi;
1. Zanzibar inapewa 10% ya Bajeti yake kwa kinachoitwa ''GBS'' kutoka Tanganyika. Muulize Mh. Saada Mkuya
2. Zanzibar haina gharama za Bajeti katika Wizara ya Ulinzi, Mambo ya ndani, Mambo ya nje, Muungano na Taasisi zote za Muungano. Maeneo hayo yanagharamiwa na Bajeti ya Tanganyika inayoitwa Tanzania.
3. Watumishi wa JMT Zbar ina 21 wanalipwa mishahara, mafao na pensheni kutoka Bajeti ya Tanganyika.
4. Tanganyika imeajiri Wazanzibar wengi kuliko SMZ ''Uzanzibar'' inawalipa hata kwa nafasi zisizo Muungano.
5. Nusu ya Wazanzibar wanaooishi Tanganyika wanatumia resource za Tanganyika Bure! elimu na Afya
6. Wabunge wa Zbar wanapewa fedha za mfuko wa Jimbo kutoka Bajeti ya Tanganyika
7. Wabunge wa Zbar Dodoma ni wengi kukliko 50 wa Baraza la wawakilishi, wanalipwa na Tanganyika
8. Balozi za Tanzania zinahudumiwa na Bajeti ya Tanganyika
9. Tanganyika ndio nchi iliyotoa fursa za Biashara na ajira za informal sector kwa Zbar kukiko pengine
10. Wbar wakiwemo wa ACT walipata elimu Bure Tanganyika wakati wa Nyerere , na hata leo HESLB inadhamini Wazanzibar wengi kuliko ZHESL. Nionyeshe nchi nyingine inayotoa udhamini kuliko Tanganyika
11. Hata umeme ! umeme Zanzibar inapewa Bure!
Orodha inaendelea, nikuulize misaada inayoletwa (fira za kimasikini sana) unaweza kufidia hayo hapo juu
Swala la kutoa maoni ya kugawana misaada ya 50% kwako ni la kudharau? Kwake halikuwa la kudharau; alikuwa anamaanisha.
Ni hoja ya kipuuzi !nimejibu hapo juu. Watu laki 6 wagawane sawa na watu milioni 60.
Yes laki 6 kwasababu lakini 6 wengine wanaishia Tanganyika kwa gharama za Tanganyika
Hapa ndo imeandikwa kinagaubaga kwamba kutakuwa na JMT na Zanzibar. Huenda unazungumza kwa kubahatisha.
Muungano ulikuwa
April 26 1964. Jina Tanzania lilikuja
November 1, 1964
Mkataba wa Muungano haukutaja Tanzania kwasababu haikuwepo. Umeelewa?
Hoja hazitolewi kwa kubahatisha.
Mkataba wa Muungano ulitaja Republic of Tanganyika and Republic of Zanzibar.
April 26 ,1964
Umeelewa!
Mimi nimekuambia hayo unayoandika mengine tayari ni ya muungano, ingawa sikukushtua lkn moja wapo ni la Elimu ya juu ambalo ni la muungano.
Elimu ya Juu si kati ya 11 ya Mkataba wa Muungano.
In fact waliozua hoja ni Wazanzibar wakisema imeingizwa kinyemela mwaka 1971.
Ni kweli ndio maana tunahoji kwanini kuwe na Wizara ya Elimu ya Juu Tanzania na Elimu ya Juu Zanzibar?
Jibu ni rahisi, ili Zanzibar waweze kunufaika na fursa zinazotokana na Tanganyika!
Haionekani kwamba unajifunza. Kile unchokiita upuuzi wa "tutavunja muungano" wala huwa hayasemwi.
Tulioishi nyakati hizo, Wazanzibar wakitaka kitu wanasema ''msipofanya abcd'' tunavunja Muungano!
Watanganyika walikuwa kimya na wengine hawakujua Zbar wanapewa fursa gani.
Siku hizi Watanganyika wameamka, wanasema '' hata leo hewala''
Nikuulize
Zawadini , Tanganyika itapoteza nini Zanzibar ikiondoka kwenye muungano!
Huyo Gavana alishawahi kukuambia pia kuwa BOT haiilipi Zanzibar mgao wa mapato yanayotoka BOT?
Zanzibar ilipewa 4.5% , Samia ameongeza hadi 9 % kwa ushahidi wa Mwenezi wa CCM Zanzibar Bw. Mbeto.
Kumbuka BoT ni Uchumi wa Tanganyika, wanachopewa ni zawadi kwasababu hawana mchango wowote katika ukuaji wa BoT! Wana mtaji lakini tu hawakukuza. In fact ni nafuu kuwalipa gharama za mtaji kuliko kuwapa 9% kwasababu ni gharama kwa Tanganyika
Gavana Ndulu (R.I.P) alisimama mbele ya Umma na kueleza bila siri. Mara ya Mwisho Zanzibar ilichangia Muungano ikiwemo ukuaji wa BoT miaka 45! iliyopita
Mkuu nikukumbushe tu kwamba bunge ni la JMT na linaendeshwa na JMT kutokana na mapato ya JMT yanayopatikana kutoka vyanzo mbali vikiwemo kodi na ushuru, faida ya BOT na vingine. Hivi vyote vinalipwa na Watanzania na wengine wanaopaswa kulipa.
Kwa Taarifa 98% ya mambo ndani ya Bunge ni ya Tanganyika ikiwemo Bajeti.
Wabunge wa Zanzibar wapo tu , hawana sababu zozote za kuwepo.
Bajeti zinazowahusu W'bar : Ulinzi, Mambo ya ndani, Nje, na Muungano. Baada ya hapo wanatakiwa waondoke wapunguze mzigo wa posho.
Inawa wahusu nini kujadili Tamisemi, Utalii, Elimu, Afya, Madini, n.k.
Kodi za Zanzibar hata zile za TRA hazivuki Bahari zinabaki huko.
Hata ushuru wa VISA za Watalii zinabaki huko lakini Wafanyakazi wa Uhamiaji wanalipwa na Tanganyika
Tuonyeshe kutoka Bajeti ya Zanzibar wapi inaonyesha mchango katika JMT
Tuonyeshe Taasisi gani inatoza ushuru au kodi Zanzibar na kuleta Tanganyika.
Nimekaa pale