Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA UMMA
1. Kutokujaza fomu kwa ukamilifu bila kuelezea kwa undani ukamilifu huo kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi.
2. Wagombea kutenguliwa kwa madai ya kwamba wao si wakazi wa maeneo wanayotaka kugombea. Madai haya yametolewa bila ushahidi wa kutosha.
3. Wagombea kuenguliwa kwa madai ya kukosa kazi bila ushahidi wa kisheria wa kuthibitisha madai hayo.
Jana katika taarifa yetu tulimthahadharisha Waziri wa TAMISEMI Ndugu Mohamed Mchengerwa juu ya kuwepo hujuma na hila zinazopangwa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kama viashiria vya kuvuruga uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024. Tunatoa wito ufuatao;
1. Tunamtaka Waziri wa TAMISEMI kama mamlaka ya mwisho ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kuwarejesha wagombea wote wa ACT Wazalendo ambao wamekatwa katika mchakato wa Serikali za Mitaa. Ni muhimu kwa TAMISEMI kuhakikisha kuwa wagombea wanatendewa haki ili kila mgombea mwenye sifa apate nafasi ya kugombea na kuchaguliwa kwa misingi ya kanuni.
2. Tumetoa maelekezo kwa wagombea wetu wote walienguliwa kukata rufaa kwa mujibu wa kanuni na muongozo wa Uchaguzi dhidi ya maamuzi mabovu yaliyofanywa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi nchini.
Rahma Mwita,
Msemaji wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ACT Wazalendo.
8 Novemba 2024