ACT Wazalendo: Bajeti haijaonesha kama itaenda kutibu kitendawili cha kikokotoo

ACT Wazalendo: Bajeti haijaonesha kama itaenda kutibu kitendawili cha kikokotoo

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
katika uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali 2025-2026 uliofanywa na ACT Wazalendo, leo wameonesha namna ambavyo bado serikali haijaweka wazi namna wanaenda kulitibu suala la kikokotoo kwa wastaafu nchini.

"Suala la kikokotoo cha Wastaafu kinaendelea kuwa kitanzi kwa watumishi wanaomaliza muda wao. Watumishi kama Polisi, waalimu, watumishi wa afya na watendaji wengine wa serikali na serikta binafsi wanaendelea kuwa na kilio kisichokua na majibu kutoka kwa Serikali.

Serikali haijafanya marekebisho ya kikokotoo cha wastaafu kinacholalamikiwa cha 40 na 35 kwa wafanyakazi wa wanaochangia mifuko ya PSSSF na NSSSF mtawalia.

Hatua hii inapelekea wafanyakazi na watumishi kupata malipo yao ya mkupuo kwa kupunjwa. Serikali ya CCM bado inaendelea kutumia kanuni zilizopitishwa mwaka 2022 zinazompunguzia mstaafu mafao yake kwa kuwalaghai kuwa itawasidia walakini inaendelea kuwakandamiza kupitia vipengele vinne.

Kipengele cha kwanza ni hiyo asilimia ambayo inapunguza mafao kwa wastani wa asilimia 60

Kipengele kingine, kigawo (Kikiokotoo) cha 1/580 badala ya kutumia 1/540 kinampunguzia mfanyakazi zaidi ya asilimia 7.

Utaratibu wa kutumia wastani wa mishahara mitatu ya juu badala ya kutumia mshahara wa mwisho inaporomosha mafao ya mstaafu kwa asilimia 7.2

Kupunguzwa miaka ya kuhudumiwa na pensheni kutoka miaka 15-5 hadi miaka 12.5 inapoteza maana ya pensheni na kuwajaza hofu wastaafu.

Pili hatua hii inaendeleza ubaguzi miongoni mwa wafanyakazi. Kuwabagua wafanyakazi kutoka sekta binafsi wanaohudumiwa na NSSSF ni kufanya makosa yanayojirudia.

Mfumo wa hifadhi ya jamii husaidia kulinda maisha ya watu na kutoa uhakika wa kuishi vizuri unapokutwa na majanga au kupoteza uwezo wa kufanya kazi kwa namna yoyote ile. Hatupaswi kuwaadhibu wazee wetu kwa kukubali kanuni hizi kandamizi zinazoenda kuwapunja mafao yao na kufupisha muda wa kuwahudumia na kuwakadiria kifo mapema zaidi.

Aidha, tunaendelea kupinga uamuzi wowote wa serikali kung'ang'ania shilingi za wafanyakazi kwa kuwaingizia kwenye mchezo wa "lesser devil“

Tunaitaka serikali kurejesha kanuni za kabla ya 2018 ambazo zinatoa mafao ya malipo ya mkupuo kwa 50% kikokotoo kuwa ni 1/540, umri wa kuishi baada ya kustaafu kuwa muda wote atakaoishi."


 
katika uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali 2025-2026 uliofanywa na ACT Wazalendo, leo wameonesha namna ambavyo bado serikali haijaweka wazi namna wanaenda kulitibu suala la kikokotoo kwa wastaafu nchini.
Wanamjali Yao tuu!
 
Back
Top Bottom