ACT Wazalendo kama CHADEMA na wengine pia wanataka Katiba Mpya

ACT Wazalendo kama CHADEMA na wengine pia wanataka Katiba Mpya

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Amesikika Abdul Nondo katika kipindi cha Medani za Siasa Star TV kwa niaba ya ACT, kwamba hata wao wanataka mno katiba mpya.

Pamoja na tofauti zilizopo yumkini Chadema au NCCR au CUF na ACT wanaweza kufikia hatima inayoweza kutuletea sote raha.

Ikumbukwe umoja ni nguvu. Bila kusahau adui yetu anayo furaha mno tunapokuwa tukiparurana wenyewe kwa wenyewe. Sembuse hata pasipokuwa na sababu?

Kwanini Mwamba (au Lissu) na Zitto kwenye mazungumzo one to one (bila ya mashabiki) liwashinde hili?

Kwanini Mbatia, Zitto au Lipumba na Zitto one to one ushabiki pembeni lisiwezekane hili?

Kwanini pasipatikane hata viongozi wa dini ku mediate hili?

Katiba Mpya mbona ipo na tukitaka inapatikana ndani ya muda tunaotaka sisi?

Kwanini karuhusu tofauti zetu ndogo ndogo kutupiga upofu kiasi hiki?

Enyi vyama vya siasa hebu tutendeeni haki sisi wananchi kwa kuweka tofauti zenu pembeni.

Tunataka Katiba mpya sasa na tunajua CCM (kwa sababu zilizo wazi) hawana nia njema kwenye hili.

Source:

Hao ACT siwaamini wana ndimi mbili.

Kuwa engage kwenye highest level behind the scene yaweza kuja na matunda. Nani ajuaye:

IMG_20220327_163423_540.jpg

Mandela aliwa engage hata kina Buthelezi
 
ACT ni chama cha kipekee Tanzania kilicho mstari wa mbele katika kuonyesha nia na njia ya kutumika katika Siasa za nyakati hizi, nazo ni kupinga Sera na kutoa mbadala wa Sera.

Lakini kwa hili la Katiba walichemsha pale walipotaka kuonyesha unyenyekevu katika swala hili kwa kudai "Tume huru kwanza" Waligwaya hapo.

Sasa wamekurupushwa na wanaanza'flip flop'
Nawasii wajiepushe na siasa hizo.
Katiba mpya tu, hakuna cha marekebisho.
 
Haitawezekana kwa sababu kila mmoja anaendeshwa na tamaa binafsi ya Shekeli.

Kila mmoja ana hoja yake binafsi mfukoni kwa maslahi yake binafsi.

Hata huko kwa viongozi wa Dini.
Baadhi yao sio wasafi ki-viile.
Nguvu na tamaa ya shekeli inayowasumbua wanasiasa ndio hiyohiyo inayowasumbua viongozi wa Dini hadi kupelekea kutimuana makanisani na kucharazana viboko misikitini.

Kila mmoja anaihitaji katiba mpya kwa maoni ya upenyo wake binafsi anaouwaza kumtoa huko mbeleni.

Hiyo ndiyo Si-hasa au Poll tick!
 
yaani chadema waanze kukaa meza moja na CUF hii ya Lipumba?? seriuos
 
Sawa.Ila Zitto unapaswa kuwa naye makini.Makini hasa.

Siasa ni pamoja na compromise. Tuache ushabiki na pia tuache kuonyeshana mashaka.

Mh. Mbowe au Lissu hawashindwi kufikia compromise na Zitto zenye tija tukiwataka wafanye hivyo.

Ikumbukwe CCM na Mukandara wakiachiwa hii tume yao peke yao, tunapata katiba mpya kama tunavyotaka sisi.
 
yaani chadema waanze kukaa meza moja na CUF hii ya Lipumba?? seriuos

Mandela alikaa meza moja na makaburu achilia mbali kina Buthelezi.

Tutu anayatambua haya:

IMG_20220327_163423_540.jpg

Ila mwenye kukaanga mbuyu wewe?

IMG_20220327_172732_377.jpg

Kwani wewe chama gani ndugu?
 
Haitawezekana kwa sababu kila mmoja anaendeshwa na tamaa binafsi ya Shekeli.

Kila mmoja ana hoja yake binafsi mfukoni kwa maslahi yake binafsi.

Hata huko kwa viongozi wa Dini.
Baadhi yao sio wasafi ki-viile.
Nguvu na tamaa ya shekeli inayowasumbua wanasiasa ndio hiyohiyo inayowasumbua viongozi wa Dini hadi kupelekea kutimuana makanisani na kucharazana viboko misikitini.

Kila mmoja anaihitaji katiba mpya kwa maoni ya upenyo wake binafsi anaouwaza kumtoa huko mbeleni.

Hiyo ndiyo Si-hasa au Poll tick!

Inafahamika ma CCM mkiona kuna uwezekano wa watanzania kuja pamoja dhidi yenu hufura kwa hasira.

CCM unapata wapi uhalali wa kuwashauri upinzani dhidi yenu?
 
ACT ni chama cha kipekee Tanzania kilicho mstari wa mbele katika kuonyesha nia na njia ya kutumika katika Siasa za nyakati hizi, nazo ni kupinga Sera na kutoa mbadala wa Sera.

Lakini kwa hili la Katiba walichemsha pale walipotaka kuonyesha unyenyekevu katika swala hili kwa kudai "Tume huru kwanza" Waligwaya hapo.

Sasa wamekurupushwa na wanaanza'flip flop'
Nawasii wajiepushe na siasa hizo.
Katiba mpya tu, hakuna cha marekebisho.

Vyama vya upinzani vitakapo watambua wakaanga mbuyu na kujitenga nao matatizo ya nchi hii yatakuwa yamekwisha.

Vyama hivi ni vyema vikajikita na mambo mengine nyuma ya pazia.

Uraiani wachawi ni wengi yumkini na wewe ni mmoja wao.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
hapa ni lazima wachangie wenye vyama??
we jamaa vipi, mbona nakuonaga kama mtu smart sana.

Kwani wapi umeona hayo ya kuwa wanaotakiwa kuchangia kuwa ni wenye vyama peke yao ndugu?

Hata hivyo mbona wala si nadra kwa mtu kumpenda mtoto kuliko mama yake?
 
jamani ni bora kulalamikia nini kiingizwe katika katiba mpya kuliko kudai katiba mpya bila kujua nini kiingizwe hukko. nini haswa kero zetu zikiingizwa katika katiba tuu basi homa itapungua na tunaweza kurudi dancini? mwisho wa siku utaambiwa na mwenyekiti wa kukusanya maoni ya kuwa , watu wengi wanataka serikali ya tanganyika na kuwe na sekali tatu. lakini huambiwi yale mazuri ya kukomesha rushwa ambayo INdia, Isreal na Brazil wameyaweka ktk katiba zao. wewe unadhani serikali tatu au tanganyika ikirudi bila ya kufuta kipengere cha kinga ya kushakiwa raisi, kilio chako cha uzembe na rushwa kwa wadhamini kitapungua? lets us grow up and wise up!
 
Kwani wapi umeona hayo ya kuwa wanaotakiwa kuchangia kuwa ni wenye vyama peke yao ndugu?

Hata hivyo mbona wala si nadra kwa mtu kumpenda mtoto kuliko mama yake?
sio wewe uliyeniuliza mm chama gani?
 
jamani ni bora kulalamikia nini kiingizwe katika katiba mpya kuliko kudai katiba mpya bila kujua nini kiingizwe hukko. nini haswa kero zetu zikiingizwa katika katiba tuu basi homa itapungua na tunaweza kurudi dancini? mwisho wa siku utaambiwa na mwenyekiti wa kukusanya maoni ya kuwa , watu wengi wanataka serikali ya tanganyika na kuwe na sekali tatu. lakini huambiwi yale mazuri ya kukomesha rushwa ambayo INdia, Isreal na Brazil wameyaweka ktk katiba zao. wewe unadhani serikali tatu au tanganyika ikirudi bila ya kufuta kipengere cha kinga ya kushakiwa raisi, kilio chako cha uzembe na rushwa kwa wadhamini kitapungua? lets us grow up and wise up!

Mkuu katiba ni suala la kitalaamu siyo kama unavyoliongelea. Unadhani kwanini CCM hawataki katiba mpya?

Kumbuka kulikuwa na katiba ya Warioba, bora kabisa. Wakaja CCM na katiba pendekezwa iliyosusiwa na ukawa.

Tambua ya msingi haya:

IMG_20220325_185419_284.jpg

Sina hakika kama haya nayo unayajua:

IMG_20220324_225211_042.jpg

Wewe huhitaji kabisa kuhakikishiwa hata haki zako tu ndugu?
 
sio wewe uliyeniuliza mm chama gani?

Kuulizwa chama inahusiana nini na kuchangia mada ndugu?

Kwani una mashaka labda ya kuonekana kupenda chama kuliko wenye chama?
 
Hakuna Mwanasiasa au kikundi cha kisiasa Bongo chenye mikakati na ujanja wa kushinikiza Serikali kuwa na Katiba mpya kabla ya 2030

Ukiona Kelele zote za katiba ya sasa kuwa haifai ukifuatilia utagundua hayo 'mapungufu' ni kwmy maeneo ya madaraka madaraka na vyeo vyeo tu hakuna lolote la msingi hasa linalohitaji Katiba mpya
 
Back
Top Bottom