ACT Wazalendo kama CHADEMA na wengine pia wanataka Katiba Mpya


Je AYATOLLAH ZITO ZUBERI KABWE anakubaliana na msimamo wa Bwana Abdul Nondo.
 

Bwana Pohamba ningeshangaa sana kutokukuona kwenye uzi huu.

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Inafahamika kuwa jitihada yoyote ya vyama kukaribiana, ni habari mbaya mno kwenu.

Bwana Phillipo Bukililo usinichukie ndugu yangu ninakusalimia tu. Yaani ni kama ninavyo wasalimu bwana Sang'udi au bwana mwengeso tu.
 
Pohamba amekwambia ukweli, hivi vilio havina msingi wa kudai katiba mpya. Inatumika kama hasira ya wanaharakati.

SSH atakuwa akiwarusha hivi hivi mpaka baada ya yeye kuwa ametoka ikulu.
 
ACT ni chama cha kipekee Tanzania kilicho mstari wa mbele katika kuonyesha nia na njia ya kutumika katika Siasa za nyakati hizi, nazo ni kupinga Sera na kutoa mbadala wa Sera.

Lakini kwa hili la Katiba walichemsha pale walipotaka kuonyesha unyenyekevu katika swala hili kwa kudai "Tume huru kwanza" Waligwaya hapo.

Sasa wamekurupushwa na wanaanza'flip flop'
Nawasii wajiepushe na siasa hizo.
Katiba mpya tu, hakuna cha marekebisho.
Braza Uzuri wa Uraiani 'Uchawi' ni sifa. "Waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba"
Nchi hii sote ji yetu.

Tugange ya mustakhabali wa Nchi.
 

Mustakabala wa nchi hii uko pema zaidi katika umoja wetu
 
Dar es Salaam. Chama cha Wananchi (CUF) kimemteua Hamad Masoud Hamad kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, akichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Haroub Mohamed Shamis.

Masoud ameteuliwa kushika wadhifa huo, akitokea Chama cha ACT Wazalendo alikokuwa akilalamika kuchezewa rafu katika uchaguzi aliogombea nafasi ya Mwenyekiti, ambapo Juma Haji Duni ndiye aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo.

Baraza hilo pia limewateua Kona Vuai Haji na Juma Shaaban Nkumbi kuwa wajumbe wa baraza kuu huku nafasi nyingine zilizo wazi zikipangwa kujazwa katika kikao kijacho cha baraza kuu.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 28 jijini hapa na Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba wakati wa kutangaza maazimio ya ajenda 14 zilizotokana na mkutano wa baraza hilo, ikiwamo mabadiliko ya uongozi, hali ya ngumu ya maisha, vita vya Urusi na Ukraine na hali ya kisiasa.

“Baraza Kuu limemshukuru Haroub Mohamed Shamis kwa kazi kubwa aliyofanya kama Katibu Mkuu katika kipindi kigumu baada ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama, hayati Khalifa Suleiman Khalifa na kukiwezesha chama hicho kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu wa 2020,” amesema Lipumba.

Azimio lingine la baraza hilo ni pampoja na kuweka kando masharti ya Ibara ya 116 kifungu kidogo cha 6 yaliyopo kwenye Katiba ya chama hicho ya mwaka 1992 Toleo la 2019, yanayozuia mwanachama mpya kugombea nafasi ya uongozi hadi atakapokuwa ametimiza miezi sita.

Baraza hilo pia limeondoa kikwazo hicho ili kuhakikisha wanachama wanaorejea ndani ya chama hicho kushiriki katika ujenzi wa chama hicho huku likitangaza kuanza kwa uchaguzi wa ndani kati ya Mei 14 mwaka huu hadi Oktoba 2023.
 

Ni hatua njema. Kutereza si kuanguka:

 
Dogo bado njaa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…