ACT Wazalendo: Kufungiwa kwa Gazeti la Mwananchi Mtandaoni ni kuminya Uhuru wa Habari

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MWANANCHI MTANDAONI NI KUMINYA UHURU WA HABARI

ACT Wazalendo tunapinga vikali kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi Mtandaoni na kuitaka Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuondoa zuio hilo ili gazeti liendelee kutoa huduma ya habari kwa umma.

Tumesikitishwa na tunalaani taarifa ya TCRA ya Oktoba 2, 2024 kusitisha leseni ya huduma za maudhui mtandaoni kwa Kampuni ya Mwananchi Communications inayojumuisha; Mwananchi Digital, The Citizen, Mwananchi na Mwanaspoti kwa siku 30. Tunalaani kwa kuwa taarifa hii ni tishio na inaashiria kuendeleza mazingira kandamizi kwa vyombo vya habari ili vizifanye kazi zao kwa uhuru kupitia vifungu kandamizi vinavyotumiwa kuzima uhuru huo.

Kampuni ya Mwananchi ilichapisha video ya katuni inayoonesha hofu za wananchi kuhusu matukio ya utekaji, kupotea na kuuawa kwa wananchi bila ya vyombo vya dola kuchukua hatua. Kulifungia gazeti kwa kufanya kazi yake ni mwendelezo wa Serikali ya CCM kuzuia na kuvidhibiti vyombo vya habari kufanya kazi kwa weledi.

Serikali inajaribu kuviziba mdomo vyombo vya habari vinavyoeleza changamoto halisi za Watanzania na kujaribu kuvitaka vibadili uelekeo wa kuhabarisha ili viingie kwenye uelekeo wa kutoa habari zinazoifurahisha Serikali pekee, jambo ambalo ni hatari sana.

Matukio ya kukamatwa kwa waandishi, kuzuia kwa vyombo vya habari na hili la kufungiwa kwa Mwananchi Mtandaoni inaonesha bado uhuru wa habari haujaimarika na hautabiriki licha ya mahubiri ya R4 za Rais Samia.

Hivyobasi, tunatoa wito kwa Watanzania wote tusimame ili kutetea na kulinda uhuru wa vyombo vya habari na waandishi. Tunaitaka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuondoa zuio lake kwa Kampuni ya Mwananchi Communications ili iendelee kutoa huduma kwa umma.

Rahma A. Mwita
Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ACT Wazalendo
03 Oktoba, 2024

Mwita.png

Pia soma
 
WhatsApp Image 2024-10-03 at 11.43.58_1a6a1041.jpg
KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MWANANCHI MTANDAONI NI KUMINYA UHURU WA HABARI

ACT Wazalendo
tunapinga vikali kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi Mtandaoni na kuitaka Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuondoa zuio hilo ili gazeti liendelee kutoa huduma ya habari kwa umma.

Tumesikitishwa na tunalaani taarifa ya TCRA ya Oktoba 2, 2024 kusitisha leseni ya huduma za maudhui mtandaoni kwa Kampuni ya Mwananchi Communications inayojumuisha; Mwananchi Digital, The Citizen, Mwananchi na Mwanaspoti kwa siku 30. Tunalaani kwa kuwa taarifa hii ni tishio na inaashiria kuendeleza mazingira kandamizi kwa vyombo vya habari ili vizifanye kazi zao kwa uhuru kupitia vifungu kandamizi vinavyotumiwa kuzima uhuru huo.

Kampuni ya Mwananchi ilichapisha video ya katuni inayoonesha hofu za wananchi kuhusu matukio ya utekaji, kupotea na kuuawa kwa wananchi bila ya vyombo vya dola kuchukua hatua. Kulifungia gazeti kwa kufanya kazi yake ni mwendelezo wa Serikali ya CCM kuzuia na kuvidhibiti vyombo vya habari kufanya kazi kwa weledi.

Serikali inajaribu kuviziba mdomo vyombo vya habari vinavyoeleza changamoto halisi za Watanzania na kujaribu kuvitaka vibadili uelekeo wa kuhabarisha ili viingie kwenye uelekeo wa kutoa habari zinazoifurahisha Serikali pekee, jambo ambalo ni hatari sana.

Matukio ya kukamatwa kwa waandishi, kuzuia kwa vyombo vya habari na hili la kufungiwa kwa Mwananchi Mtandaoni inaonesha bado uhuru wa habari haujaimarika na hautabiriki licha ya mahubiri ya R4 za Rais Samia.

Hivyobasi, tunatoa wito kwa Watanzania wote tusimame ili kutetea na kulinda uhuru wa vyombo vya habari na waandishi. Tunaitaka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuondoa zuio lake kwa Kampuni ya Mwananchi Communications ili iendelee kutoa huduma kwa umma.

Rahma A. Mwita
Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ACT Wazalendo
03 Oktoba, 2024

Screenshot 2024-10-03 135150.png
 
Chama cha ACT Wazalendo kimepinga vikali kufungiwa kwa maudhui ya mtandaoni ya kampuni ya Mwananchi Communication Limited hivyo kutoa wito kwa serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuondoa zuio hilo ili MCL iendelee kuchapisha maudhui ya mtandaoni kama ilivyokuwa awali
View attachment 3114121
IMG-20241003-WA0064.jpg
 
Samia ni dikteta wa kwanza mwanamke asiye na aibu, wapenda haki na amani lazima tushikamane tumpinge kwa namna na gharama yoyote
 
...subirini tutawafungia sana!
Hivi sasa tunajadiliana namna ya kuwafungia hata wale waliompinga Zuchu kusema mitano tena.
.....Vipi basata hamuwezi kufanya jambo hapo?.....mbona mpo kimya?
 
Back
Top Bottom