Lwiva
JF-Expert Member
- Apr 17, 2015
- 15,416
- 22,334
Naona mjalaana kavaa saa yake ya mamilioni ya shilingi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona mjalaana kavaa saa yake ya mamilioni ya shilingi
Naanza kukumbuka alipofungulia magazeti "alisema" ukiniparua na Mimi nitakupatia " ah hapana chawa wangu wata kuparua @ 4R , Resilience, Reform , ReconciliationKUFUNGIWA KWA GAZETI LA MWANANCHI MTANDAONI NI KUMINYA UHURU WA HABARI
ACT Wazalendo tunapinga vikali kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi Mtandaoni na kuitaka Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuondoa zuio hilo ili gazeti liendelee kutoa huduma ya habari kwa umma.
Tumesikitishwa na tunalaani taarifa ya TCRA ya Oktoba 2, 2024 kusitisha leseni ya huduma za maudhui mtandaoni kwa Kampuni ya Mwananchi Communications inayojumuisha; Mwananchi Digital, The Citizen, Mwananchi na Mwanaspoti kwa siku 30. Tunalaani kwa kuwa taarifa hii ni tishio na inaashiria kuendeleza mazingira kandamizi kwa vyombo vya habari ili vizifanye kazi zao kwa uhuru kupitia vifungu kandamizi vinavyotumiwa kuzima uhuru huo.
Kampuni ya Mwananchi ilichapisha video ya katuni inayoonesha hofu za wananchi kuhusu matukio ya utekaji, kupotea na kuuawa kwa wananchi bila ya vyombo vya dola kuchukua hatua. Kulifungia gazeti kwa kufanya kazi yake ni mwendelezo wa Serikali ya CCM kuzuia na kuvidhibiti vyombo vya habari kufanya kazi kwa weledi.
Serikali inajaribu kuviziba mdomo vyombo vya habari vinavyoeleza changamoto halisi za Watanzania na kujaribu kuvitaka vibadili uelekeo wa kuhabarisha ili viingie kwenye uelekeo wa kutoa habari zinazoifurahisha Serikali pekee, jambo ambalo ni hatari sana.
Matukio ya kukamatwa kwa waandishi, kuzuia kwa vyombo vya habari na hili la kufungiwa kwa Mwananchi Mtandaoni inaonesha bado uhuru wa habari haujaimarika na hautabiriki licha ya mahubiri ya R4 za Rais Samia.
Hivyobasi, tunatoa wito kwa Watanzania wote tusimame ili kutetea na kulinda uhuru wa vyombo vya habari na waandishi. Tunaitaka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuondoa zuio lake kwa Kampuni ya Mwananchi Communications ili iendelee kutoa huduma kwa umma.
Rahma A. Mwita
Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ACT Wazalendo
03 Oktoba, 2024
Pia soma
Sababu ni hii picha 🙄🙄🙄 kama ni hii picha basi ninayo fafanuzi yake kuhusu walio chukizwa nayo siyo samia tu bali raia wote feki walio shika serikali