Pre GE2025 ACT Wazalendo kuiingiza tena mkenge CHADEMA katika chaguzi 2024 na 2025?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,887
Reaction score
7,673
Nimepata taarifa za ndani kabisa kuwa Chama cha ACT Wazalendo ambacho mmoja wa waasisi wake ni kibaraka namba moja wa Chama cha Mapinduzi, wanampango wa kuwashawishi CHADEMA Wasigombee kwenye chaguzi zijazo kutokana na matamko ya viongozi wa CCM kuhusu chaguzi zilizopita.

Hivi karibuni aliyekuwa waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwa Bukoba Mkoani Kagera alitoa kauli tata ambayo wengi wanaamini ndio iliyopelekea akatumbuliwa uwaziri. Na wiki iliyopita aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido yeye aliongea mazito kabisa na wote waliweka wazi au walitanabaisha yanaaminika huenda yanafanyika wakati wa uchaguzi.

Sasa Chama hicho kupitia kwa kiongozi wake mmoja wa juu wanataka kushawishi CHADEMA eti wasusie uchaguzi kama plan B maana Plan A ya kutaka Tamisemi ijiondoe kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa wanahisi kuna dalili kesi iliyopo mahakamani ni kama itapigwa chini.

Wito wangu kwa CHADEMA, Msiingie MKENGE. Hawa jamaa hawaeleweki. Mnaweza kusema msiingie kwenye uchaguzi huku wao wakiingiza timu. Msisahau yaliyowakuta 2020. Kiongozi wao alienda mpaka Ufipa kuema wataandamana nchi nzima kupinga Uchaguzi jioni yake akaonekana na SUTI MPYA ikulu ya Zanzibar akisubiri Maalim Seif aapishwe kwenye umoja wa kitaifa.

Soma Pia: ACT Wazalendo na CHADEMA kukutana kujadili hali ya Siasa nchini

Ina maana alienda ufipa akiwa ameshanunua SUTI ya uapisho na tiketi ya boat/ndege alikuwa nayo mfukoni na hivyo maneno yote yale eti wataandamana sijui hapatatawalika zilikuwa hadaa za kuwaingiza mkenge kina MBOWE. Na Mwamba akaingia mkenge kweli kwa kuwaita chama makini kumbe mchana wapinzani usiku chama tawala.

Nimeshawaonya! hauri zenu
 
Acha zako, ACT iliwaingizaje mkenge CHADEMA 2020? Ule uchaguzi uliharubiwa na CCM , maneno mengine ni kujifariji.
 
Uchaguzi wa 2024/25 unapaswa kuaihirishwa hadi 2030 ili muda huo wa miaka mitano 1. Tupate Katiba mpya itakayoweka utaratibu mpya wa utawala.
2. Tufanye referendum kuamua muundo wa Muungano.
3. Tutengeneze utaratibu mpya wa kupata viongozi kwa kuunda tume ya uchaguzi iliyo huru kweli, aidha mihimili mingine ya Dola iwe na bajeti ya kutosha bila kuwa taasisi za uchawa.
4 Mwisho tutengeneze sera za taifa zitakazofuatwa na vyama vyote vitakavyo sajiliwa na mamlaka huru, sio hizi taasisi zilizo ambukizwa uCCM.
 
Hivyo si vyama upinzani ni saccos za watu
Vingekuwa vyama vya upinzani kweli miaka 30 yote ya upinzani ccm hisingekuwepo madarakani.
 
Ni Lazima CHADEMA na ACT washirikiane kwenye chaguzi ili kupata nguvu ya pamoja iliyo nzuri, Ila kiuhalisia hizi chaguzi zimewakilia vibaya sna wapinzani binafsi sioni wakitoboa, ni heri wafanye maridhiano na mama wajiandae na 2030.
 
Uchaguzi wa 2024/25 unapaswa kuaihirishwa hadi 2030 ili muda huo wa miaka mitano 1. Tupate Katiba mpya itakayoweka utaratibu mpya wa utawala.
2. Tufanye referendum kuamua muundo wa Muungano.
3. Tutengeneze utaratibu mpya wa kupata viongozi kwa kuunda tume ya uchaguzi iliyo huru kweli, aidha mihimili mingine ya Dola iwe na bajeti ya kutosha bila kuwa taasisi za uchawa.
4 Mwisho tutengeneze sera za taifa zitakazofuatwa na vyama vyote vitakavyo sajiliwa na mamlaka huru, sio hizi taasisi zilizo ambukizwa uCCM.

Kwanini hadi 2030 siyo 2026, 27, 28 au 29?
 
2030 kwa sababu inatoa muda wa kutosha kujiandaa bila kutafuta visingizio. Ukosefu wa utashi wa kisiasa na woga wa kukosa ulaji ndio unaotumika na vyama kukwamisha mchakato, vinginevyo inawezekana kufanyika hata 2025.
 
2030 kwa sababu inatoa muda wa kutosha kujiandaa bila kutafuta visingizio. Ukosefu wa utashi wa kisiasa na woga wa kukosa ulaji ndio unaotmika na vyama kukwamisha mchakato, vinginevyo inawezekana kufanyika hata 2025.
Abduli punguza tamaa
 
Nimepata taarifa za ndani kabisa kuwa Chama cha ACT Wazalendo ambacho mmoja wa waasisi wake ni kibaraka namba moja wa Chama cha Mapinduzi, wanampango wa kuwashawishi CHADEMA Wasigombee kwenye chaguzi zijazo kutokana na matamko ya viongozi wa CCM kuhusu chaguzi zilizopita.

Hivi karibuni aliyekuwa waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwa Bukoba Mkoani Kagera alitoa kauli tata ambayo wengi wanaamini ndio iliyopelekea akatumbuliwa uwaziri. Na wiki iliyopita aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido yeye aliongea mazito kabisa na wote waliweka wazi au walitanabaisha yanaaminika huenda yanafanyika wakati wa uchaguzi.

Sasa Chama hicho kupitia kwa kiongozi wake mmoja wa juu wanataka kushawishi CHADEMA eti wasusie uchaguzi kama plan B maana Plan A ya kutaka Tamisemi ijiondoe kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa wanahisi kuna dalili kesi iliyopo mahakamani ni kama itapigwa chini.

Wito wangu kwa CHADEMA, Msiingie MKENGE. Hawa jamaa hawaeleweki. Mnaweza kusema msiingie kwenye uchaguzi huku wao wakiingiza timu. Msisahau yaliyowakuta 2020. Kiongozi wao alienda mpaka Ufipa kuema wataandamana nchi nzima kupinga Uchaguzi jioni yake akaonekana na SUTI MPYA ikulu ya Zanzibar akisubiri Maalim Seif aapishwe kwenye umoja wa kitaifa.

Soma Pia: ACT Wazalendo na CHADEMA kukutana kujadili hali ya Siasa nchini

Ina maana alienda ufipa akiwa ameshanunua SUTI ya uapisho na tiketi ya boat/ndege alikuwa nayo mfukoni na hivyo maneno yote yale eti wataandamana sijui hapatatawalika zilikuwa hadaa za kuwaingiza mkenge kina MBOWE. Na Mwamba akaingia mkenge kweli kwa kuwaita chama makini kumbe mchana wapinzani usiku chama tawala.

Nimeshawaonya! hauri zenu
Ccm safari hii ,hawachomoki , mwendazake na ubabe wake ata uko aliko atakua anaisimulia chadema,

This time ifanye ifanyavyo inaondoka , kila rangi wataiona we subiri ,mda mwalim
 
2030 kwa sababu inatoa muda wa kutosha kujiandaa bila kutafuta visingizio. Ukosefu wa utashi wa kisiasa na woga wa kukosa ulaji ndio unaotumika na vyama kukwamisha mchakato, vinginevyo inawezekana kufanyika hata 2025.

Hii scale yako 2030 kigezo chake tafadhali.
 
Ni hivi: Tujipe miaka mitano kuanzia sasa bila kufanya uchaguzi ili tuweke mambo yote makubwa na muhimu sawa. 2030 tukiwa tumejipanga tufanye uchaguzi mkuu ulio huru na wa haki bila ujanja ujanja.
 
Wengine tunadhani tujipe si zaidi ya miaka 2.

Kulikoni wewe ungependa kutulazimisha kuwa isipungue 5?

Kwani wewe na yeye mmejiapiza liwalo na liwe, ni angalau mitano mingine?
 
Acha zako, ACT iliwaingizaje mkenge CHADEMA 2020? Ule uchaguzi uliharubiwa na CCM , maneno mengine ni kujifariji.
2015 wakati wa UKAWA aliweka Anna Mughwira kugombea Urais ili kujaribu kugawanya kura, akashindwa (Alifadhiliwa na Kikwete), hata wapinzani waliposusia bunge ili kupinga Dkt Shein Kuingia bungeni baada ya kumdhulumu Urais Maalim Seif wakati wa Uzinduzi wa Bunge, ni Zitto Pekee aliyebakia kwenye bunge lile lililobariki Uchafu wa Salum Jecha

2020 alirudia huo uharamia wake kwa kushirikiana na Membe, Japo alipingwa na Maalim Seif, Membe akawa hana ujanja.

Huyu mtu si wa kuaminika hata Chembe
 
Ccm safari hii ,hawachomoki , mwendazake na ubabe wake ata uko aliko atakua anaisimulia chadema,

This time ifanye ifanyavyo inaondoka , kila rangi wataiona we subiri ,mda mwalim
Magufuli wakati wa kampeni 2020 aliaminishwa na NAPE kuwa LISSU hawezi simama hata dakika moja, kilichotokea hakuamini kila akihema ubongo wake ukawa unatamka LISSU-cdm, LISSU-cdm, LISSU-cdm akaanza kuumwa nchi ikakatwa mapande ya uchaguzi Pwani-samia, kusini-kasim, Kati-ndugai, magharibi-pinda n.k, yeye hoi bin taabani, alijikata sana kuonyesha haumwi waapiii mwisho akawa haonekani, wapiga kampeni wake akiwamo kasimu akiwa kavaa kanzu na salama aleku tena siku ya Ijumaa kule iringa akatudanganya kuwa marehemu anapiga kazi na anawasalimu watz!

Yaani Magu asiwasalimie watz yeye mwenyewe hadi atume mtu? Mara tukasikia R.I.P!
Sasa mama abdul anataka amtunishie misuli LISSU nawatahadharisha CCM tumieni busara kuepuka yaliyopita maana siyo KWA SPANA ZA LISSU, msidhani LISSU ataogopa kushukiwa viungo vya pwani, Magu na ukali wake alifumuliwa hakubakizwa! Oyoooo mie simo
 
Nimepata taarifa za ndani kabisa kuwa Chama cha ACT Wazalendo ambacho mmoja wa waasisi wake ni kibaraka namba moja wa Chama cha Mapinduzi, wanampango wa kuwashawishi CHADEMA Wasigombee kwenye chaguzi zijazo kutokana na matamko ya viongozi wa CCM kuhusu chaguzi zilizopita.

Hivi karibuni aliyekuwa waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwa Bukoba Mkoani Kagera alitoa kauli tata ambayo wengi wanaamini ndio iliyopelekea akatumbuliwa uwaziri. Na wiki iliyopita aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido yeye aliongea mazito kabisa na wote waliweka wazi au walitanabaisha yanaaminika huenda yanafanyika wakati wa uchaguzi.

Sasa Chama hicho kupitia kwa kiongozi wake mmoja wa juu wanataka kushawishi CHADEMA eti wasusie uchaguzi kama plan B maana Plan A ya kutaka Tamisemi ijiondoe kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa wanahisi kuna dalili kesi iliyopo mahakamani ni kama itapigwa chini.

Wito wangu kwa CHADEMA, Msiingie MKENGE. Hawa jamaa hawaeleweki. Mnaweza kusema msiingie kwenye uchaguzi huku wao wakiingiza timu. Msisahau yaliyowakuta 2020. Kiongozi wao alienda mpaka Ufipa kuema wataandamana nchi nzima kupinga Uchaguzi jioni yake akaonekana na SUTI MPYA ikulu ya Zanzibar akisubiri Maalim Seif aapishwe kwenye umoja wa kitaifa.

Soma Pia: ACT Wazalendo na CHADEMA kukutana kujadili hali ya Siasa nchini

Ina maana alienda ufipa akiwa ameshanunua SUTI ya uapisho na tiketi ya boat/ndege alikuwa nayo mfukoni na hivyo maneno yote yale eti wataandamana sijui hapatatawalika zilikuwa hadaa za kuwaingiza mkenge kina MBOWE. Na Mwamba akaingia mkenge kweli kwa kuwaita chama makini kumbe mchana wapinzani usiku chama tawala.

Nimeshawaonya! hauri zenu
Nyingine ni kuungana na kuweka mgombea mmoja CHADEMA msikubali kabisa mwami ni kibaraka ilitakiwa waungane tangu 2019/20.Mwami mjanja sana
 
Kulikoni wewe ungependa kutulazimisha kuwa isipungue 5?
😆 Kwanza silazimishi mtu, hayo ni maoni yangu kila ninapotathmini mwenendo wa siasa za nchi hii. Kwa mtazamo wako unaona kuna dalili za kufanikisha lolote ndani ya hiyo miaka miwili? ....
Huoni kuwa kuna ucheleweshaji wa makusudi unaofanywa na wenye mamlaka ili hali iendelee kama ilivyo?

Mimi nadhani na kuamini kuwa utawala uliopo utusaidie kuvuka kipindi hiki cha mpito bila kukimbilia kufanya uchaguzi ambao baadhi ya watu wanadhani wameisha shinda hata kabla ya uchaguzi wenyewe kufanyika.

Ili kuvunja huu utaratibu wa hovyo kiutawala, tujipe muda wa kutosha Ili tutoke na kitu kinachoungwa mkono na wengi bila manung'uniko.
 
Back
Top Bottom