Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kuwa kitaweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, kikidai kuwa uteuzi wake haukufuata Katiba na Kanuni za chama hicho
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 14 Septemba 2025 jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo, mchakato uliompitisha Dkt. Samia kugombea urais ulikuwa wa “kinyemela” na haukuwa na uhalali wa kikatiba ndani ya chama chake
“Umma wa Watanzania unafahamu wazi kuwa uteuzi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan haukufuata Katiba na Kanuni za CCM. Hakuwahi kuchukua fomu, hakudhaminiwa na wanachama, hakupendekezwa na Kamati Kuu wala Halmashauri Kuu ya CCM, na hakuwahi kushindanishwa na mgombea yeyote. Hivyo, uteuzi wake ni batili,” amesema Shangwe
ACT Wazalendo imeeleza kuwa hakuna kikao cha kikatiba cha CCM kilichowahi kupitisha ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea urais, jambo linalofanya uteuzi wa Dkt. Samia kuvunja Katiba ya nchi pamoja na Sheria ya Vyama vya Siasa
Chama hicho kimesema kitalifanyia kazi pingamizi hilo kwa mujibu wa taratibu za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika muda uliowekwa
Kauli hiyo imefuata baada ya Chama cha ACT Wazalendo kutoa taarifa kuwa Mgombea Urais wa Chama hicho Luhaga Mpina anakabiliwa na mapingamizi kwa mara nyingine tena kuhusu uteui wake kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali na wagombea wa Urais wa NRA na AAFP
Soma pia GE2025 - Mgombea Urais ACT Wazalendo Luhaga Mpina, awekewa mapingamizi ya uteuzi wake na Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wagombea urais NRA na AAFP

Chanzo: Jambo TV