ACT Wazalendo kuzindua Mikutano ya Hadhara Februari 19

ACT Wazalendo kuzindua Mikutano ya Hadhara Februari 19

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Siku moja baada ya CHADEMA kuzindua mikutano ya hadhara jijini Mwanza, Chama cha ACT Wazalendo nacho kimetangaza kuanza mikutano yake Februari 19, 2023 jijini Dar es Salaam.

Akisoma maamizio ya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi jana Dar es Salaam, katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema, "katika awamu ya kwanza programu ya kitaifa ya mikutano ya hadhara inajumuisha mikoa ya Dar es Salaam Februari 19 Unguja, 26 Februari Pemba, Machi 4 Tanga na Pwani ni Machi 9."

"Pia Lindi mkutano tutafanya Machi 10, Mtwara Machi 11, mkoa wa kichama Selous Machi 12, Tabora Machi 14-15 na Kigoma Machi 16-18."

Kuhusu awamu ya pili ya mikutano hiyo, Shaibu amesema itatangazwa baadaye akibainisha kuwa ajenda zitakazotawala mikutano ya ACT Wazalendo ni hali ya maisha ya wananchi na mageuzi ya mifumo ya kidemokrasia nchini na kitambilisha ahadi za chama hicho.

"Chama kinatambua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi, namna watawala wameshindwa kuzitatua, sisi tutaonesha sera mbadala za kutatua changamoto hizo,"amesema.

Amesema kabla ya kuzindua mikutano ya hadhara, Februari 18, 2023 watazindua kaulimbiu ya chama hicho.

MWANANCHI
 
Ado Shaibu akagombea ubunge wa Africa Mashariki. Wabunge wa CCM wakampigia makofi akajua amepata kiti. Kumbe wanamsanifu na kumchinjia baharini.
 
Chama cha zito,zito anawatumia wa pemba kama toilet pepa.
 
Huu muungano wa Wasaliti ulishapoteza Dira tangia kuanzishwa kwake,nawasikitikia sana Wafuasi wa Maalim Seif kumezwa na hiki Chama na kushindwa kukishauri kuacha kupambana na CHADEMA na kupambana na CCM.

Poleni sana Jussa na wenzako,mkiendelea kukaa humo hivyohivyo na kushindwa kuamka hatma yenu ya kisiasa iko hatarini sana.
 
Mhhhhh fyuuu. Upinzani gani. Njaa tupu. Endeleeni kutangaza li chama lenye mwelekeo wa kidini. Kichapo kipo pale pale. Siwezi kupoteza muda wa kwenda kusiliza sera za chama kilichojaa udini. Ni CCM tu hadi 2050.
 
Mhhhhh fyuuu. Upinzani gani. Njaa tupu. Endeleeni kutangaza li chama lenye mwelekeo wa kidini. Kichapo kipo pale pale. Siwezi kupoteza muda wa kwenda kusiliza sera za chama kilichojaa udini. Ni CCM tu hadi 2050.

Hicho chama ndio mana kimpo pwani na visiwani nje ya hapo hakina wafuasi labda kigoma kijijini kwao zito.
 
Back
Top Bottom